Edo Kumwembe na mhariri Mwananchi muwaombe radhi wakazi wa mkoa wa Mara

nimesoma hiyo makala ya eddo nikabaki nashangaa,hivi mamlaka husika hazilioni hili gazeti wakalifungia?yani serikali ya mkoa inatumia pesa nyingi kuwashawishi investors kuwekeza mkoa wa mara huku kuna mataahira mengine yanahamasisha watu wasiende mara!
kumbe yule jamaa kichwani empty kabisa.
Wewe kila kitu unawaza kufungia
Mbona Tanzanite halijafungiwa?
 
Kwani Edo ni mwandishi wa habari?
Binafsi yangu sijawahi kumuelewa Edo.na nilishamu unfollow Instagram
 
mara hatujafikia hatua ya kununua ardhi,ardhi ipo tele, sisi ni wafugaji,tunafuata majani popopte yalipo, kama huko mnauza ardhi mnapaswa kuwaelimisha na siyo kusimanga.Ardhi kitu gani bhana huku kwetu ipo tele

Hivi unaweza je kukuta mtu kajiwekea kaeneo kake ka eka 1 alafu nyie mnavamia mnagawana vipnde vya Hatua kumi kumi?
 
Njoo sasa uone upumbavu wa wakurya wenzio huku ukonga hasa majohe!

Hivi unaweza je kukuta mtu kajiwekea kaeneo kake ka eka 1 alafu nyie mnavamia mnagawana vipnde vya Hatua kumi kumi?
. Kama si upumbavu ni nini?
Si nasikia hata ardhi ya machame haikuwa yao waifukuza watu waliokuwa hapo na kuchukua ardhi. Kuchukua ardhi ya mtu mwingine ni ushujaa
 
Edo kumwembe ni fala sana ukitaka kujua ni mshamba angalia hata uandishi wake ni wa kijuha sana kwa kuwa amechokoza nyuki ni mda wa kuanika madhambi yake yote apate kujijua kuwa ni mtu mshamba na mjinga sana
Mkuu na wewe huwa unakimbilia mkuki au panga ukinyimwa bia?
 
sasa wewe ndiye wakili wake?
wakati anajibu post yangu mbona hakusema hayo wewe unayokimbia nayo?

watu asilimia kubwa hasa wengi
wa huko kaskazini
wanapenda ligi na kutusema vibaya watu wa mkoa wa Mara
Kisa??
USTAARABU WETU
UUNGWANA WETU
HEKIMA TULIZONAZO
UPOLE WETU PIA

wamehamisha ofisi za mbuga kwenda kwao
SISI TUPO KIMYA
wamehamisha shughuli za kijeshi pale Fort Ikoma kwenda Monduli
SISI TUPO KIMYA

sasa wanahisi sisi ni wajinga sana
But hatupo hivyo wanavyofikiria wao
sio rahisi usikie mikoa ya kusini huko wakiusema vibaya mkoa wa Mara
Kwa lipi hasa?
But hawa majirani zetu
wengi wao ila sio wote ndiyo wanafanya hivyo
sasa hao ni rahisi mno kuwagundua!

umeelewa sasa rafiki?
Haya karibu nawe mkoa wa Mara
ukawe balozi mzuri wa mkoa huu mzuri!

Mimi simtetei yeye, napinga generalization dhidi ya mkoa wowote, maana ni ujinga na ni kichocheo cha ubaguzi, kama wewe una generalize mambo kuhusu mkoa fulani using'ake wengine wanapofanya generalization pia

Umesema watu wa Kusini hawawezi kuwasema mbona Edo mbona ni mtu wa Kusini? Crimea amewaita wapumbavu mbona sio wa Kaskazini?
Balozi mzuri wa mkoa wako unapaswa kuwa wewe
Upo bitter sana na mkoa wa Arusha, pole
 
Nadhani anayetakiwa kubalika ni huyo Edo mwenyewe, na pia ndo anayetakiwa kujiuliza "yeye binafsi yukoje" na siyo watu wa Mara wakoje. Kwanza anaonekana ana dharau sana kwa watu wa Mara, hakika hiyo makala yake ina maudhi sana kwa wana Mara.
 
nimesoma hiyo makala ya eddo nikabaki nashangaa,hivi mamlaka husika hazilioni hili gazeti wakalifungia?yani serikali ya mkoa inatumia pesa nyingi kuwashawishi investors kuwekeza mkoa wa mara huku kuna mataahira mengine yanahamasisha watu wasiende mara!
kumbe yule jamaa kichwani empty kabisa.
Watu wa Mara mumeumia ila ndio Ukweli nyie ni watata Sana mlitakiwa muwe na inchi yenu kama Somalia
 
Edo yupo sahihi.Coverave ya taarifa za mkoa wa Mara zimepungua kwa kuwa saizi Camera zote zimehamia ikulu na kwenye ccm.matukio ya maana yanayojitokeza nchini hayapewi kipaombele.Naamini bado Mara matukio hayo yapo ila hayaripotiwi kama awamu ilopita.
Lakin hakuna mkoa au watu ambao ni purely perfect.Mkoa wa Mara lazima wakubali kubadilika,hata sisi wa mikoa Mingine tuna la kujifunza zuri tu kutoka Mara.Ila mkiambiwa mabaya yenu msione ni tusi maana ni kawaida yenu ninyi sisiemu mkiambiwa ukweli mnaona kama ni tusi lakin sio tusi.
NB:maneno ya edo yanaweza kuwa na udhaifu lakin 90%ni kweli tupu
Mara ni kwa hovyo Sana hawa jamaa ubabe tu ustaarabu kwao ni ndoto
 
Mara nyingi nimewasikia watu wa Mkoa wa Mara wakijisifia kwa ubabe na ukatili! Hivyo wakati umefika waanze kujisifia kwa mema na ukarimu!

Kwa mfano Tanga wanajisifia wa ukarimu "Waja leo waondoka leo"; Kagera wanajisifia kwa elimu "Ishomile"; Mbeya na Songwe wanajisifia kwa heshima nk
 
tatizo la kumwembe huwa anajiona sahihi kuliko watu wote hata ukisomamakala zake za mpira ni hivyohivyo ni asili yake hawezi kuacha
 
Edo kumwembe ni mshamba na limbukeni fulani lakini kwa kuwa amezungukwa na vijana tegemezi wa bia toka kwake wameogopo kumkosoa, lakini kupitia JF atapata somo kuwa watu wanamjua kulivyo anavyofikiria
 
Mara nyingi nimewasikia watu wa Mkoa wa Mara wakijisifia kwa ubabe na ukatili! Hivyo wakati umefika waanze kujisifia kwa mema na ukarimu!

Kwa mfano Tanga wanajisifia wa ukarimu "Waja leo waondoka leo"; Kagera wanajisifia kwa elimu "Ishomile"; Mbeya na Songwe wanajisifia kwa heshima nk
Waja leo waondoka leo siyo ukarimu bali waja leo ukae week, mwezi ndiyo ukarimu olijino, kule mara ukarimu upo tena siyo wachoyo wanapenda wageni hizo story za kukuririshwa na Edo kumwembe vijiweni achana nazo
 
Mara ni kwa hovyo Sana hawa jamaa ubabe tu ustaarabu kwao ni ndoto
Kwenu ndipo kwa hovyo Mbona wizi kuchinjana kurogana kumeshamiri pambana na kwenu kwanza maliza ushirikina wenu ndipo ushabikie uzushi wa boss wako Edo kumwembe.
 
Watu wa Mara mumeumia ila ndio Ukweli nyie ni watata Sana mlitakiwa muwe na inchi yenu kama Somalia
Acha hizo nitajie mkoa usiokuwa na uhalifu majambazi wezi, taja wilaya yenye malaika watupu isiyo na Polisi wala Mahakama nchini
 
EDO KUMWEMBE NA MHARIRI MWANANCHI MUWAOMBE RADHI WAKAZI WA MKOA WA MARA

Nimesoma Makala ya Edo Kumwembe, ijulikanayo kama UCHOKOZI WA EDO, kwenye ukurasa wa 22 wa gazeti la Mwananchi, toleo na: 6938 (ISSN 0856-7573) la Tarehe 5 Agosti 2019, yenye kichwa cha habari: MKOA WA MARA NITAENDELEA KUUSIKIA REDIONI.

Katika Makala hii fupi, Mwandishi Edo Kumwembe ametumia visa kadhaa vya uhalifu vinavyotokea mkoa wa Mara kuhoji je Mkoa wa Mara uko Tanzania?, akaendelea kuandika “kwa nini watu wake wako hivyo? Pia kaandika “Kila unapofungua redio au televisheni kusikia taarifa ya habari unakutana na mambo mawili. Kama sio kukamatwa na bangi, basi utasikia mauaji yaliyohusisha silaha kali ama panga au mshale. Mara imekwama wapi?”.

Pia katika hitimisho la Makala yake kaandika “Kuna mikoa sijawahi kugusa hii nchi. Mara, Singida, Tabora, Kigoma, Rukwa na michache mingineyo. Natamani siku moja nifike nifanye utalii wa ndani. Hata hivyo kati ya mikoa yote hii, naomba mkoa wa Mara niendelee kuusikia redioni tu kuutazama katika televisheni, naomba wageni mnaokwenda huko mniwakilishe”. Mwisho wa kunukuu baadhi ya sehemu katika makala hii.

Ukiisoma makala hii, utagundua kuwa Edo Kumwembe, kwa kukusudia au kwa bahati mbaya lengo kubwa la makala yake ni kuwaonyesha Watanzania na watu wengine wa dunia kuwa mkoa wa Mara kwanza haustahili kuwepo Tanzania, ama tabia zinazofanyika hazipatikani sehemu nyingine Tanzania, hivyo unakosa sifa ya kuwepo ndani ya Tanzania. Lakini pia kamaanisha kwa nini watu wake wako hivyo? Tafsiri yake rahisi ni kuwa watu wote wa mkoa wa Mara ni katili, wakamatwa na bangi, na wauaji, je huu ndio ukweli kuhusu mkoa wetu?

Pia katika hitimisho Edo kaandika kuwa yuko tayari kutembelea mikoa yote ila sio mkoa wa Mara, yeye kama mwandishi ambaye maandishi yake yanasomwa na watu wengi, wengine miongoni mwao wanakusudia kuutembelea mkoa wa Mara kwa ajili ya Utalii (Butiama, Serengeti n.k), Biashara, Makazi, Elimu, au shughuli za kijamii kama kuoa/kuolewa na nyinginezo. Maana yake ni kuwa anawapa hawa watu tahadhari kuwa mkoa huu haufai kutembelewa na watu wake sio watu wema.

Akumbuke mbuga ya Wanyama kubwa Afrika nzima ni Serengeti, moja ya mapato makubwa kwa Taifa na Mkoa kwa ujumla ni hifadhi hii ya Serengeti, anapotokea mwandishi asiye na maarifa ya kupima anachoandika na athari zake kiuchumi, kijamii ni hatari sana kwa umoja wetu kama Taifa, hali inayoonyesha ubaguzi wa waziwazi dhidi ya jamii ya sisi watu wa mkoa wa Mara.

Je ni kweli kila unapofungua redio utakutana na habari za mauaji na kukamatwa na bangi pekee? Huu ni upotoshaji wa wazi na huenda mwandishi huyu ana malengo makubwa kuutangaza mkoa huu kama sehemu isiyofaa hapa Tanzania. Kama jamii ya watu wa mkoa wa Mara wasingekuwa na habari yoyote njema, au isingekuwa na watu wazuri au wema je ingeweza kuzaa, kuzalisha, kulea na kumkuza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa letu, na mtu aliyepigania usawa duniani, na kuendesha harakati za ukombozi wa nchi mbalimbali toka Utumwani na kutawaliwa na Wakoloni? Kiongozi ambaye hadi leo kanisa la Roman Catholic limemtangaza kuwa ni Mwenye Kheri na wana mchakato kumfanya kuwa miongoni mwa Watakatifu wa kanisa lao (kwa mujibu wa taratibu zao).

Juzi limetokea tukio baya, la mtu kumuua mkewe hadi kumchoma kwa moto, je tukio hili limefanywa na mtu wa mkoa wa Mara? Laiti lingefanywa na mtu wa mkoa wa Mara basi Edo na watu wenye nia kama yake wangeandika makala kwa mwaka mzima kuhusu tukio lake. Je ukatili wa kijinsia au wa aina yoyote kwa hapa Tanzania hufanyika tu mkoa wa Mara? Jibu ni rahisi tu kuwa hapana. Uhalifu wa watu katika jamii hauwezi kuubinafsisha uwe wa mkoa mzima au wa watu wote wa mkoa wa Mara.

Tumewahi sikia matukio kama ya uchunwaji wa watu Ngozi mkoa wa Mbeya, lakini hakuna aliyeandika huu mkoa je upo Tanzania na pia haufai kutembelewa. Hivi juzi kulikuwa na wahuni wanachinja Watoto huko Njombe, hakuna aliyesema watu wa Njombe wa namna gani au kuhoji kuwa kweli mkoa huo uko Tanzania? Yametukia matukio mabaya katika baadhi ya mikoa kama mauaji ya Vikongwe na wenzetu wenye ulemavu wa Ngozi, matukio ambayo ni mabaya na sijawahi sikia yakitokea mkoa wa Mara, lakini sikumuona Edo au mwandishi yeyote kuyahusisha matukio haya na watu wote wa mikoa hiyo wala kuhoji je mikoa hiyo iko Tanzania?

Kiufupi nikuelimishe ndugu Edo, uhalifu upo dunia nzima, ndio maana kuna majeshi, mahakama, pia magereza. Nchi ya Marekani kwa mfano, kwa mwaka huu matukio ya matumizi ya bunduki, toka Januari hadi Agosti 6, matukio ya watu kupigwa risasi ni 33,307, idadi ya vifo ni 8,837, majeruhi 17,489, Watoto waliojeruhiwa au kuuwawa (umri 0-11) ni 396, vijana miaka 12-17 waliouwawa kujeruhiwa ni 1,813. Chanzo (www.gunviolencearchive.org) haya ni matukio ya mwaka huu tu na bado haujaisha katika taifa kubwa la Marekani, lakini hakuna mwandishi wa huko anayesema Marekani sio sehemu salama ya kuishi. Hii ikujengee uwezo na uelewa juu ya matukio ya uhalifu duniani, na hapa nimekupa mfano mmoja.

Kwa kuwa hauna uelewa kuhusu mkoa wa Mara, kwanza ningependa kukuelimisha kuwa watu wa mkoa wa Mara ni wakarimu, wenye akili, wachapa kazi, wenye upendo, wasio wanafiki, wasiopenda kujivuna, waaminifu, wanaoipenda nchi yetu, na kwa ujumla wenye sifa njema tofauti na ulivyotaka kuwajengea watu hofu kuhusu kuutembelea mkoa wa Mara. Pia mkoa una mambo mengi mazuri, uoto wa asili, Mto Mara, madini ya aina mbalimbali ikiwemo dhahabu na mengine, mbuga za Wanyama Serengeti, Ziwa Victoria, Utalii ikiwepo mahali alipozaliwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere n.k. Hivyo ni mkoa uliobarikiwa na Mungu, tuna ardhi yenye rutuba na kwa mwaka tunalima hadi mara tatu, hapa ni kwa ufupi tu.

Pia nakukaribisha utembelee mkoa wa Mara, ila pia kama utaendelea na moyo wako wa kibaguzi hata usipokuja hakuna utakachokipunguza maana mkoa wetu kwa nyakati tofauti umetembelewa na Watanzania toka sehemu mbalimbali za nchi yetu na viongozi wa nchi mbalimbali duniani. Mkoa wetu umepokea watu maarufu waliokuja kutembelea hifadhi ya Serengeti, watu mashuhuri kama David Beckam, Will Smith, Nicole Isaacs, Terrence J, Bill Gates, Justin Timberlake, Jessica Biel, Oprah Winfrey, Steadman Graham, George Clooney, Amal Alamuddin, Naomi Campbell, Tom Cruise, na wengine wengi.

Hitimisho, kama kicha cha makala hii, kama mkazi na mtu wa Mara nakutaka kwa uzito ule ule ulioutumia kuandika na kwenye kurasa yako utuombe radhi watu wa mkoa wa Mara, ninakupa siku 7 kutoka leo kufanya hivyo wewe, pamoja na Mhariri wa gazeti la Mwananchi ambaye ameruhusu makala kama hii yenye malengo ovu na ya kibaguzi kuchapishwa kwenye gazeti lake. Baada ya siku hizo kupita bila kufanya hivyo nitachukua hatua stahiki dhidi yako na gazeti la Mwanachi.

Mwandishi wa Makala hii ni:
Jina: Deo Meck
Email: dmecky@hotmail.com
Simu: +255715481628

Kwani lipi la ajabu hapo! Sawa tumekusoma na wewe kama tulivyomsoma Edo!!
 
Hata Mimi mkoa huu nitaendelea kuusikia redioni tu
 
Kwa nini uanze ku mjudge huyo uliyemjibu kuwa atakuwa mtu wa kaskazini? Ina maana watu wa kaskazini nao wote wana sifa fulani uliyoiona kwa uliyem quote hadi uanze kumuita ni wa kaskazini?

Yaani unapinga generalization/ stereotyping kuhusu watu wa mkoa wa Mara na kisha unafanya generalization kuhusu watu wa Kaskazini?
Ndiyo shida ya watu wa Mara
 
Back
Top Bottom