Edo Kumwembe azungumza na Mungu siku ya hukumu

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Yule mchambuzi wa habari za michezo kupitia gazeti la Mwanaspoti ndugu Edo Kumwembe ameandika kupitia ukuta wake wa Facebook kuhusu mazungumzo yake na Mungu ameandika hivi ".....Na katika hukumu yangu Mungu ataniuliza 'Edo nakushtaki kwa kosa la kuwaita Watanzania wenzako wapumbavu, nipe ushahidi'....nitatabasamu kisha nitamjibu 'nilijua hilo siku ulipowapa wengi wao pumzi za kutengeneza katiba yao ambayo ni mwongozo mkuu wa maisha yao ya kidunia baada ya vile vitabu vyako. Wao wakaleta ushabiki wa Simba na Yanga'....Mungu ataniambia kwa upole 'basi kama utaingia motoni nitakupeleka kwa makosa mengine sio hili'.....nitatabasamu na kusubiri mashtaka mengine....."

Karibuni wakuu.
 
Haya basi, Polisi wanalinda mitaa nchi nzima kuhakikisha watu hawalichanichani Bunge la Katiba kwa maandamano, na huku je, watawazuiaje akina Edo Kumwembe kwenye mitaa ya kurasa zao !!!!!!!??????
 
Ni kweli mana naamini kule ndani kuna watu ukiwauliza ntajie hata kifungu kimoja cha katiba unachokikumbuka yeye hajui na anachojua ni kusema naunga mkono hoja na nasupport alichosemamjumbe aliopita.Badala ya kufanya mambo kwa ajili ya wananchi wao wanafanya kwa ajili ya maslahi ya watu wachache.

Kuna vita nyingine hatutakiwi kupigana hata kidogo mana Mungu wetu atatupigania.
 
Ukanjanja bana!

Soka na siasa wapi na wapi?!

Blaza tumia akili na usiwe mpumbavu.Naamini unaweza ukawa umesomea kilimo na ukatoa idea zako katika siasa mana siasa ni uwanja ulio wazi na fikra,hekima na maadili ndio vitakufanya uwe kiongozi bora. Naanza kuamini kweli viongozi hawana makosa ila kuna wananchi ndio wanaokosea kuwaweka madarakani na naamini wewe ni mmoja wao.
 
Yupo sahihi kabisa na nimempa 'like' kule, ila kuna watu povu limewatoka, na ukirusha jiwe gizani ukasikia mtu anagumia ujue limempata. Watanzania tu mambumbumbu na tunaongozwa na ushabiki na mkumbo kuliko uhalisia wa jambo, itatugharimu sana.
 
Yupo sahihi kabisa na nimempa 'like' kule, ila kuna watu povu limewatoka, na ukirusha jiwe gizani ukasikia mtu anagumia ujue limempata. Watanzania tu mambumbumbu na tunaongozwa na ushabiki na mkumbo kuliko uhalisia wa jambo, itatugharimu sana.

Kuna yule Libaba kama sijakosea
 
Back
Top Bottom