Nundu_Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 811
- 349
Maisha yote ya mtu hayatenganishwi na yanategemea imani. Kwa maneno mengine, maisha ni imani. Ye yote anayeishi duniani maisha yake ni imani yake.
Hatahivyo, swali ni kwamba imani ni nini? Imani ni kwa nani au nini:tunaamini nini? Duniani kuna imani zaidi ya moja au mbali mbali?
Kuhusu imani ni nini. Kadiri ya Waebrania, 11:1 anaeleza maana ya imani kuwa ni kuwa na uthabiti katika vitu tunavyovitumainia, na hakika ya mambo yasioonekana.
Imani ni uthabiti na uhakika katika vitu tunavyovitumainia na mambo yasioonekana. Maneno "uthabiti" na "uhakika" yana maana ya 'uelewa'.
Uelewa maana yake ni ufahamu wa kina wa mambo, maaarifa na elimu ya vitu. Tukisema Petro ana imani maana yake Petro ana ufahamu wa kina wa mambo, maarifa na elimu ya vitu.
Kwa msingi huo, katika maana yake pana, imani ni kipaji anachokuwa nacho mtu kinachomwezesha kufahamu kwa kina na bayana vitu tunavyovitumainia na mambo yasioonekana. Kwa hiyo imani ni uwezo wa hali ya juu wa akili.
Watu kwa mfano, hawawezi kumchagua mtu ambaye hawamfahamu kwa kina awe mtunza fedha wa kikundi chao. Hawamwamini mtu ambaye bado hawajamfahamu kwa kina ni nani: maisha yake, historia yake na ya ukoo wake; tabia na mwenendo wake awatunzie fedha zao.
Wanaposema tunamwamini Petro awe mtunza fedha wa kikundi chetu maana yake wanamfahamu kwa kina kwamba lolote litakalotokea sasa na baadae, fedha yao itakuwa na itabaki salama.
Kumwamini Petro awe mtunza fedha wa kikundi ni suala la utafiti mwingi kuchunguza kwa kina Petro ni nani: tabia yake, historia ya ukoo wake na maisha yake ya uchumi na kijamii.
Imani mbali ya kuwa ni kipaji, kwa wengine ni suala la elimu: kujifunza na kuchunguza kwa kina tabia na maumbile ya vitu na mambo mbalimbali.
Imani ni ufahamu wa juu wa akili hivyo isichanganywe na ufahamu wa kawaida tunaoupata kwa kupitia milango mitano ya fahamu: pua, macho, masikio, ngozi na ulimi.
Imani ni mambo ya akili hivyo ni kinyume cha hisia au miguso. Kwa sababu hii kwamba imani iko kwenye akili, inafanyika na akili haiwezekani imani kuwa zaidi ya moja au mbali mbali.
Imani inatoka kwa akili inafanya na kufafanua kazi za kiakili. Hii maana yake ni kuwa imani haitenganishwi na kazi za kiakili.
Kama ilivyo akili haifanyi makosa au uchungu pia imani haifanyi makosa na haisababishi uchungu, majeraha au uharibifu.
Kazi za kiakili ni uumbaji, uhai, imani, maarifa, elimu, uvumbuzi, kufafanua mafundisho ya imani na maadili, mfumo, na maendeleo.
Duniani kazi za kiakili ni kwa njia ya imani. Lakini tofauti na tunavyoweza kufahamu imani bila kutengana na akili haifanyi makosa na haisababishi uchungu, majeraha au uharibifu.
Imani ni kwa akili. Kinyume na akili sio imani. Imani sio kwa kingine chochote isipokuwa kwa akili. Kwa sababu hiyo imani ni moja duniani. Duniani hakuna imani zaidi ya moja au mbali mbali.
Ikiwa inatoka kwa akili, imani sawa na akili haifanyi makosa na haisababishi uharibifu, uchungu au majeraha.
Kingine chochote kinachofanya makosa au kusababisha uchungu, uharibifu au majeraha; hiyo sio akili pia hiyo sio imani.