Dunia imebadilika, wazazi tusichukulie kwa wepesi masuala ya mirathi kwa watoto wetu

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,205
5,334
Kuna simulizi moja ya kusikitisha ya mzee mmoja ambaye alitokea kuhudumu katika nyadhifa za juu serikalini akiwa kama mwakilishi wa wananchi wa jimbo moja la mkoa wa nchini.

Mzee huyu mwenye jina linalofanana sana na kiungo kimojawapo cha mwili wa binadamu, kipindi cha uhai wake alifanikiwa kumiliki taasisi moja iliyojihusisha sana na mambo ya kutetea haki za walioonewa, nakujizolea umaarufu na ubobezi mkubwa katika taaluma hiyo akiajiri wataalamu wengi nakujiongezea ukwasi mkubwa sana.

Kuna historia kipindi cha miaka ya nyuma mzee huyu tajiri alihusishwa na dili moja la uporaji wa fedha za benki tegemeo ya kufikirika ambapo ili kupoteza maboya (kipindi hicho bosi wa kwanza wa kufikirika akiwa binamu yake) benki ilitiwa njiti na mzee wa watu akatorokea ughaibuni.

Ila baada ya kufika ughaibuni siku zote mjini shule akamsaliti bosi kwenye mgao na akasepa na kibunda chote, bosi akaja kugundua baadae kuwa umdhaniae siye ndiye ikabidi hatoe zuio la binamu mtu kutokutia tena maguu katika mipaka ya kufikirika mpaka bosi atakapoiaga dunia,

Shetani hawatupi wezi wake na siku hazigandi hatimaye bosi kipenzi cha wengi akauvuta na mzee yule akawa hana budi kurejea kwenye ardhi ya nyumbani, punde aliporudi akatimba pale pale bosi alipokuwa na akatangaza nia ya kuwa mwakilishi wa jimbo lile na baadae kuanza kurudisha fadhila(dizaini kama nafsi ya usaliti ilikuwa ikimsuta) alizitumia fedha zile kujenga shule kadhaa za kisasa alizozibatiza majina ya watawala wa kabila lake na barabara ya lami katika jimbo hilo masikini la mkoa wa nchini na kuikabidhi serikalini.

Turudi kwenye ubuyu, kama tujuavyo siku hazigandi hatimaye uzee ukabisha hodi na maradhi humo humo ndani mzee akaona mali zile kuwaachia wanae (pengine ni ile dhambi ya ubatili wa pesa zile tokea mwanzo) si poa bora aanze kuwagawia wenye uhitaji nazo maana hana muda mrefu anasepa.

Dunia ni ndogo punde watoto wa kibosile huko ughaibuni wakapata taarifa kuwa baba yenu kule kufikirika ameshaanza kugawa urithi kwa watu baki, wengine washaanza kupewa hadi mashamba na mali kadhaa.

Kama ujuavyo pesa haijawahi kumwacha mtu salama, wana wakamshawishi mzee awafuate ughaibuni kwa ajili ya matibabu, mzee bila hiyana akakwea pipa bila ya wasiwasi wowote akiamini watoto wana nia njema hatimaye akawasili alipotorokea enzi zile akiomba lolote litokee (kwa bosi) hili arudi kupaona nyumbani.

Kama ujuavyo safari ya ndege haikawii punde akatua ughaibuni na kulakiwa na lockdown moja matata safari hii si tena usitoke kurudi kufikirika bali utosogeza mguu kokote bila tamko letu, kimasihara mzee akapigwa pini la kimateka, wana wakampeleka kwenye kituo cha kulelea wazee na passport yake akapokonywa, mzee akawa mpweke vya kutosha akililia kurudi nyumbani walahu hata kama ni mauti yamfike akiwa kufikirika lakini pasipo mafanikio mzee aliendelea kuugulia kwa majuto.

Siku zote hakuna kinachokauka mapema zaidi ya machozi, japo macho ubaki mekundu na usoni ishara ya majonzi, hatimaye mzee akaaga dunia akiwa huko huko ughaibuni ndipo zengwe likaanza katika familia, watoto wakifight kila mmoja kula mgao wake kwanza ndipo mwili wa mzee uruhusiwe kutoka ughaibuni na kutua kufikirika kutunzwa kwenye nyumba ya milele, siku zikaendelea kukatika toka siku moja hatimae wiki kadhaa huku sintofahamu ikitawala.

NB: STORI HII NI YA KUBUNI NA WALA HAIUSIANI NA TUKIO LOLOTE LILE LA KWELI (Fictional story & characters)
 
Ngoja nisubiri muendelezo kama ile suti kubwa ya yule mzee alietoa ile staili ya vifungo kupishana

Hivi nimewaza nini na ukiherehere wangu
 
Huyo mzee likuwa na akili sana alijua kuwa hana watoto wenye akili. Bora utafute mtu bali umpe mali ukijua ataiendeleza kuliko kumoa mtoto asiye na akili kisa ni damu yako.
 
Jamani hivi ule msiba uliisha salama kweli maana hiyo kabila naijuwa akili zao ( mke wa marehemu + watoto na ndugu wa marehemu) 🔥🔥🔥
GENTAMYCIME tunaonba mrejesho.
 
Huyo mzee likuwa na akili sana alijua kuwa hana watoto wenye akili. Bora utafute mtu bali umpe mali ukijua ataiendeleza kuliko kumoa mtoto asiye na akili kisa ni damu yako.
Lakini kumbuka kuwa hayo maamuzi yake uliyodai ni ya busara ndiyo yaliyochangia pakubwa afe kifo cha mapema tena cha simanzi, upweke na majuto mbali na ardhi ya taifa lake kama mbwa.

Je bado uko miongoni mwa wale wazazi wanaoshikilia dhana ya kutoshirikisha familia katika maamuzi ya msingi kama mirathi, kwa kuamini wako sahihi kuamua chochote kile kwa kuwa fedha na mali ni zao peke yao?
 
Alikufa hivyo kwa sababu ya watoto wasiokuwa na akili. Ukifanikiwa kwenye maisha mali muachie mtoto mwenye mali sio siyo unamuachia mtu kampuni hata kusomesha watoto wake hawezi.
 
Back
Top Bottom