Duh kumbe wanawake wakiwezeshwa wanaweza

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,921
31,161
Rais Jakaya Kikwete akiwa na maafisa waandamizi wanawake wa JWTZ.kulia ni Major General Lilian Kingazi na kushoto ni Major General Grace Mwakipunda.Hongera sana akina Mama wote wa Tanzania Major General Lilian na Grace wanawakilisha vyema.

Duh kuna rafiki yangu mjeshi kanitonya Major General Grace Mwakipunda kwa sasa ndiye mkuu wa utumishi JWTZ.
 
huo ushikaji wa mikono na hicho kicheko cha huyo Jenerali...
 
huo ushikaji wa mikono na hicho kicheko cha huyo Jenerali...

Mkuu Kituko mbona mnapenda kuwadhalilisha wanawake angekuwa mwanaume msingesema.

mbona huo mdomo ameupanua kishangingi halafu anaangalia penye dush... au anaitamani.

Heshima kwa kina Mama.

MH....hili pozi la huyu mjeda wa kulia limeniacha na maswali kama buku hivi.............

Yaani wachangiaji wote hamkuona kitu kingine zaidi pozi duh mfumo dume umetuharibu.
 
Last edited by a moderator:
Huyu jamaa hata wajeshi, tena maJenerali....anawashika mikono kama wale wanamipasho wa CCM wanaojipendekeza kupata uBunge wa 'vitanda' maalum! hii sio heshima ya kiJeshi, ukizingatia naye ni mjeshi!
 
Na usisahau kuna mwanamama anarusha Jet Fighter, sijui kama yupo hapo? nimemsahau jina lake.
 
Huyu jamaa hata wajeshi, tena maJenerali....anawashika mikono kama wale wanamipasho wa CCM wanaojipendekeza kupata uBunge wa 'vitanda' maalum! hii sio heshima ya kiJeshi, ukizingatia naye ni mjeshi!

........ni kweli kabisa, kwa mjeda mwenye sare na anaongea na amiri jeshi, hii sio nidhamu timamu !
 
Ngoja nimwalike TUMBIRI Dr mtarajiwa atumwagie nasaha zake.
 
Last edited by a moderator:
Ngongo - Asante sana kwa hii taarifa. Nilikosa kuiona kwenye vyombo vya habari. Hongereni sana wakina mama...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kituko mbona mnapenda kuwadhalilisha wanawake angekuwa mwanaume msingesema.

Heshima kwa kina Mama.

Yaani wachangiaji wote hamkuona kitu kingine zaidi pozi duh mfumo dume umetuharibu.
ukiona komenti zaidi ya moja zinafanana ujue kuna kaukweli kidogo.japo sio lazima.
 
Hongera Meja Jenarali Grace Mwakipunda na Lilian Kingazi kwa kufikia cheo hicho Miaka 41 Jeshini si mchezo hakika mmehimiri mikiki mikiki mingi.
 
Major General Grace Mwakipunda na Lilian Kingazi hongereni sana. Major General wa kwanza hapa Tanzania mwanamke alikuwa Zawadi Madawili sijui kama bado yuko kazini au alishastaafu.
 
Back
Top Bottom