Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,952
- 6,885
Hakuna mtu anayepinga kuwa Dubai ni matajiri sana ukilinganisha na sisi. Mimi ninachopinga ni hii tabia ya kuona maghorofa ni maendeleo! Hao walioyavumbua (ukiacha yale ya Yemen) waliisha yatilia mashaka hata kabla ya 9/11! hayo majengo ya World Trade Centre yalikuwa yanalaaniwa kwa kutokuwa user friendly hata kabla ya kulipuliwa. Sasa hivi maghorofa mengi ya ajabu yanajengwa katika bara la Asia kwa sababu huko bado wanaona ufahari. kupata kibali kujenga majengo kama haya ulaya si rahisi kwa sababu wanajua adha zake. Hutasikia hata siku moja Norway wanashindana kujenga jengo refu duniani na wala sidhani kama kuna skyscraper ya maana mjini Oslo. Na hawa ni matajiri kuliko hao waarabu! Kwa kifupi, majengo marefu yanapendeza kwenye picha na wala hayavutii kama sehemu ya kuishi. Mfano wa haraka ni hapa nyumbani. Mazingira ya kariakoo kabla ya kuigeuza mini Dubai na ya sasa ni tofauti kabisa. Miji ya Houston, Dallas, Los Angeles hata siku moja haihesabiwi kama miji bora ya kuishi marekani pamoja na maghorofa yao. Ujenzi wa busara kidogo wa maghorofa unaweza kuonekana Seattle, Vancouver na pengine New York.
Hilo la kuwa na gardens Dubai hata Phoenix, Arizona wana golf courses za ajabu. Lakini swali linaloulizwa kila siku ni je ni sustainable kufanya vitu hivi katikati ya jangwa? Ni matumizi bora ya hayo maji adimu kunywesha golf courses na parks?
Lakini, yote tisa, suala hili ni subjective. Kwa wale wanaoona maghorofa ni maendeleo watazidi kuona hivyo na kushangilia ubomoaji wa maeneo ya kati ya jiji la Dar es Salaam na Upanga ili angalau lifanane na Manhattan! wengine tunaamini kuwa Dubai,Abu Dhabi, Beijing, Khartoum,Shanghai na wengine kama hao wanafanya makosa makubwa kuvunja majengo yao ya kiasili na kujenga maghorofa ambayo kwa mtazamo wetu hayana sifa yeyote isipokuwa urefu. Tukubali kutofautiana.