Drama haziishi. Tujuzane huko ulipo sukari inauzwa bei gani?

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Tusikwepe ukweli kwamba kipindi cha mfungo wa mwezi Mtukufu Ramadan, kimekuwa ni kipindi kinachokuja na neema ya unafuu wa maisha kwa jamii hususani hata wale wasiofunga yaani Wagalatia na wasio na dini.

Unafuu wa maisha unatokana na kwamba, Wachuuzi wengi wanachuma rehma na fadhila zitokanazo namwezi huo kwa kufanya ugavi wa mahitaji ya msingi hususan vyakula kwa bei inayokidhi asilimia kubwa ya jamii kumudu.

Lakini, Serikali isiyojali ya Tanzania. imekuwa ikikurupuka usingizini na tambo za kuwaasa wachuuzi washushe bei za vyakula ilihali yenyewe ipo mifukoni mwa wafanyabiashara na wawekezaji wasio na utu wala ubinaadam. Bei ya mafuta ambayo ni funguo muhimu ya mfumuko wa bei imekuwa inapandishwa holela kuwaridhisha wawekezaji huku ikiacha madhara ya mfumuko wa bei wa bidhaa ghafi za vyakula. Tumeona namna ambavyo viongozi waandamizi wa serikali wakipita huku na huko wakisindikizwa na rundo kubwa la waandishi wa habari kujinasibu kuwa OLE WAO WATAKAOONGEZA BEI YA SUKARI... mara wanakuja na bei elekezi kisha wanafanya show mbili tatu za kukamata waagizaji wa sukari kisha senema inaishia hapo.

Uzi huu tupeane update kwenye maeneo yetu, unanunua sukari kwa bei ya Tshs ngapi kwa kilo moja? Na upatikanaji wa sukari upoje eneo lako? Kama hautajali unaweza kutaja wilaya.

Sisi huku tunapoishi, sukari inauzwa TZS 4,500 hadi 5,000 kwa kilo. Hapo naongelea Kigamboni kutokea Vijibweni kuelekea Kibada hadi Toangoma na Kongowe. Hizo ni bei za rejareja. nimezunguka maeneo yote hayo na kukuta bei hiyo ya sukari.

Karibu tujadiliane
 
Tusikwepe ukweli kwamba kipindi cha mfungo wa mwezi Mtukufu Ramadan, kimekuwa ni kipindi kinachokuja na neema ya unafuu wa maisha kwa jamii hususani hata wale wasiofunga yaani Wagalatia na wasio na dini...
3,600
 
Back
Top Bottom