Dkt. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake

Mkuu kuna HOLOCUST kubwa mno inawamaliza wananchi wetu kila siku. Tofauti ni kwamba yenyewe tumeishaikubali kwamba iwepo tuu. Njaa, vita, magonjwa, umaskini nk..mi nadhani hiyo nayo ni holocust au genocide kabisa (ukiita ile ya Rwanda iliyomaliza watu million moja kwamba ni Genocide, je haya niliyoyataja hapa yanamaliza wangapi kwa mwaka?) sema tuu basi..tunaamua kutumia maneno pale tunapotaka ya-fit mawazo yetu. Bush akisema Iran, N Korea na Syria ni axis of evil..sisi tunasema Njaa, magonjwa na umaskini ndo axis of evil wa mwafrika!

Masanja,

Sasa umenena, naona hata hivo vijisent vya safari za ulaya na US kwa rais vingesaidia hata njaa ya wananchi.
 
gm said:
Jokakuu,
Kama Nyerere alichukia adhabu ya kunyongwa angeiondoa lakini katika historia nafikiri sijakutana na sehemu inayosema alijaribu hata kuiondoa hii katiba, kama bunge lingegoma kupitisha angetumia executive power, sina uhakika kama katika katiba yetu tuna executive power ila nafikiri inawezekana.

gm,

..binafsi nimekuwa nikijiuliza kwanini Mwalimu hakuifuta adhabu ya kifo? it was just a matter of directing the AG to table the motion in the parliament.

..sasa maadamu Mwalimu aliitumia kwa NADRA hukumu hiyo, nalazimika ku-speculate kwamba kuna SPECIAL CASES ambazo aliona hukumu hiyo inapaswa kutumika.

..kwa upande mwingine inawezekana Mwalimu hakuchukua hatua kuifuta sheria ya kunyonga kwa kuzingatia hisia za wa-Tanzania.

..inawezekana kabisa wa-Tanzania hatukumshawishi Mwalimu[Mwinyi,Mkapa,Kikwete] kwamba sheria hii ya kunyonga ilikuwa ikitukera.
 
gm,

..kwa upande mwingine inawezekana Mwalimu hakuchukua hatua kuifuta sheria ya kunyonga kwa kuzingatia hisia za wa-Tanzania. .

Mkuu you have made my day....... TANGU LINI VIONGOZI WETU WAKAZINGATIA HISIA AU MATAKWA YETU SISI WANANCHI?;-)
 
Mkuu you have made my day....... TANGU LINI VIONGOZI WETU WAKAZINGATIA HISIA AU MATAKWA YETU SISI WANANCHI?;-)

Masanja,

Kama viongozi wetu hawawasikilizi washauri wao je watawasikiliza wananchi? nafikiri tatizo ni kuwa viongozi wanakuwa na kasumba kuwa they are the final authority and wao ndio wanapaswa kusikilizwa and not the other way round.
 
Masanja,

..hivi unaweza kusema kwa uhakika kabisa kwamba wa-Tanzania wanakereka na kuwepo kwa sheria ya adhabu ya kunyonga?

..je, kulikuwa na harakati zozote zile za wadau, kudai kufutwa kwa sheria za adhabu ya kunyonga, na Mwalimu akawa kikwazo kwa harakati hizo?

..i have been very critical kuhusu utawala wa Mwalimu, lakini nachelea kumtwika dhamana, na lawama za kuendelea kuwepo kwa sheria ya adhabu ya kunyonga.
 
jokaKuu,
Nimeisoma hii quote inaendana kabisa na unachokisema:
"The most effectual means of preventing the perversion of power into tyranny are to illuminate the minds of the people." Thomas Jefferson
 
Naomba kuweka swali lanyongeza hii inayoitwa Historia ya Tanzania imeanza lini Rasmi naoma kuelimishwa na kabla ya hapo ni kipi tunaweza kukiongelea naomba mchango utakao elimisha wengine kama mie ambao tumekuwa katika mashaka na historia yetu kwani miaka siomingi tangia kuzaliwa kwa Tanzania sasa kabla ya hapo nini kilikuwa
 
Jf imekuwa ni mahali pa kupashana habari na kuweza pia kuzungumzia mambo ya historia yetu na mwelekeo wa nchi. Kuna Huyu bwana anajulikana kama marehemu Dr Kleruu, mie nimekuwa nikimsikia katika wimbo wa Mbaraka Mwinshehe kuwa alikuwa mwanamapinduzi, Je kuna yeyote anaweza kutupatia taarifa kumhususu huyu Dr Kleruu alikuwa nani hasa na uana mapainduzi wake ulikuwa vipi katika historia na siasa za Tanzania?

Naomba kuweka swali lanyongeza hii inayoitwa Historia ya Tanzania imeanza lini Rasmi naoma kuelimishwa na kabla ya hapo ni kipi tunaweza kukiongelea naomba mchango utakao elimisha wengine kama mie...
 
Naomba kuweka swali lanyongeza hii inayoitwa Historia ya Tanzania imeanza lini Rasmi naoma kuelimishwa na kabla ya hapo ni kipi tunaweza kukiongelea naomba mchango utakao elimisha wengine kama mie...

Spear,

Katika mjadala huu tumekuwa tunazungumzia sana historia ya Dr. Kleruu na uanamapinduzi wake kama ulivyoimbwa na Marehemu Mbaraka Mwinshehe, kuna baadhi yetu hatukujua kabisa huyu Dr. Kleruu alikuwa nani katika tanzania iliyopita ambayo ndio inakuwa historia hapo. Kama unazungumzia Tanzania kama Tanzania au Tanganyika hatukuweza kuweka limit kuwa tanzania tunayoizungumzia ni ipi bora tumepeana habari na historia ya mambo ambayo yalitokea wakati wengine hatujui hata mwelekeo wa nchi yetu ulianzia wapi hadi kufikia tulipo.

Labda kwa kuongezea ungetuelezea wewe kwa uelewa wako historia ya Tanzania ni ipi na inaanzia wapi?
 
Mwanzoni mwa miaka ya 1970 Mwamwindi alikabiliwa na shitaka la kumwua Dr Wilbert Kleruu, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa wakati huo.

Mshitakiwa Mwamwindi alijitetea kuwa alipokuwa anamwua marehemu Kleruu alirukwa na akili akapotewa na fahamu ya kuweza kuelewa kile alichokuwa anakitenda. Jaji Onyiuke alikataa hoja hiyo kwa kutilia maanani kwamba baada ya mshitakiwa kughadhibishwa ndipo alipokwenda ndani kuchukua bunduki ambayo aliitumia kumwua marehemu

Inasimuliwa, kuwa Dr. Wilbert Kleruu alifikia hata hatua ya kuanza kudhihaki makaburi ya mababu zake Mwamwindi akimwambia Mwamwindi: “Humu ndimo mlimozika mirija yenu”. Mwamwindi alikasirika sana. Akaficha hasira yake kutoka makaburini wakaongozana na Kleruu hadi nje ya nyumba yake. Akamwomba kiongozi huyo abaki nje, yeye akaingia ndani.

Mke wake Mwamwindi alimwona mume wake akichukua bunduki na kusimama dirishani. Mama huyo alidhani mume wake anakwenda kuwinda nguruwe. Kumbe, Mwamwindi alitokea dirishani. Mwamwindi akamlenga sawa kichwani Mkuu wa Mkoa na kumpiga risasi. Kisha akabeba mwili wa Mkuu wa Mkoa na kuuweka nyuma ya boneti ya gari alilojia mkuu huyo wa mkoa. Mwamwindi akaendesha gari hilo hadi kituo cha polisi Iringa. Akaripoti kwa kutamka; " Nendeni mkamchukue mbwa wenu nyuma ya gari!".

Tukio lile bado linatuachia maswali? Je, ni kwanini Dr Kleruu alikwenda nyumbani kwa Mwamwindi siku ya Jumapili?

Je, yawezekana Mwamwindi na Dr Kleruu walikuwa na ugomvi mwingine kabla ya tukio?

Waliopata kusikia simulizi zaidi ya tukio lile watusimulie.
 
Kuna tetesi za kuibiwa mke na mkuu huyo.....ila kama ni kweli basi leruu alikuwa na moyo yaani waiba mke tena watembelea nyumba hiyo hiyo lol.....ila binafsi naamini mwamwindi alikuwa adui wa utekelezaji wa azimio la Arusha...adui wa mipango ya maendeleo ya nchi ya kufikirika

mix with yours
 
kuna tetesi za kuibiwa mke na mkuu huyo.....ila kama ni kweli basi leruu alikuwa na moyo yaani waiba mke tena watembelea nyumba hiyo hiyo lol.....ila binafsi naamini mwamwindi alikuwa adui wa utekelezaji wa azimio la arusha...adui wa mipango ya maendeleo ya nchi ya kufikirika

mix with yours
kuiba mke wa mtu kumbe ni hatari hivyo!! Nasikia kuna mwanasiasa mmoja mashuhuri nae kaiba mke wa mtu hivi karibuni sasa kumbe anahatarisha maisha yake ki hivyo!
 
Mwaka 1971 hadi mwaka 1972 kulikuwa na operesheni vijiji ambapo watu walitakiwa kuhamia kwenye vijiji vya ujamaa. Mwamwindi alikuwa mmja wa wale waliokataa kuhamia vijijini. Siku ya Krismas mwaka 1971 (au 1972 hivi), Dr. Kreluu aliwatembelea wale waliokuwa wamekataa kuhamia vijijini na ndipo alipokumbana na hiyo dhahama. Kwa vile Kreluu alikufa, mpaka leo haijulikani walikosana nini na Mwamwindi kwa vile maelezo ya mwamwindi yaliyopitakana wakati anajitetea na hakukuwa na mtu mwingine wa kuyathibitiha. Kesi ya Mwamwindi iliendeswa mwaka 1973 na alinyongwa mwaka 1974 huko Dodoma.
 
Tembeleeni mjengwa blog ameielezea vizuri sana habari hii na wachangiaji wake pia wamejitahidi sana kutoa ufafanuzi.
 
JIBU: Mimi nilikuwa nasoma shule ya sekondari ya Mkwawa (Lutengano tulikuwa naye) wakati Dr Kleruu alipopigwa risasi na mzee Mwamindi. Naomba nisaidie kuchangia majibu ya maswali yaliyoulizwa hapa juu.

SABABU: Dr Kleruu, ambaye alikuwa Mkuu wa mkoa mwenye umri wa miaka 35 wakati huo, alimwita Mzee Mwamindi na kumtukana na kumkaripia mzee Mwamindi mbele ya wafanyakazi wa Marehemu Mwamindi.

Kleruu alimwambia mzee Mwamindi kuwa Mwamindi ni bepari, kupe na mnyonyaji. (Huu ndio ushahidi uliojitokeza mahakamani). Kleruu aliongeza kuwa serikali inamnyang'anya Mwamindi shamba lake na kulifanya shamba la ujamaa na kuwa serikali itataifisha baadhi ya nyumba za mzee huyo. Mzee Mwamindi alichukua bunduki yake iliyokuwa katika landrover yake na kumpiga risasi Kleruu aliyekufa hapo hapo. Mzee Mwamindi aliupakia mwili wa Kleruu katika landrover yake na kwenda moja kwa moja kituo cha polisi ambapo aliwaeleza ukweli polisi. Polisi walimkamata na kumtia ndani mzee huyo mkulima.

MATOKEO YA KESI: Mwamindi alikiri kosa na kuhukumiwa kunyongwa. Rais Nyerere aliidhinisha adhabu hiyo na, mwaka uliofuatia, Mzee Mwamindi alinyongwa.

REACTION YA WENYEJI WA IRINGA: ijapokuwa nilikuwa na miaka 17, nakumbuka kuwa watu wengi wa Iringa hawakufurahia hukumu hiyo.

KWA NINI?: kwa jamii ya wahehe, jamii yetu - kimila - haina huruma na watu aina mbili
(1) Watu wanaofumaniwa na wake za watu , na
(2) mtu ambaye ana umri sawa na watoto wako kukutukana na kukuvunjia heshima hadharani. Hiyo ni "no no!".

Pia nakumbuka kuwa, miaka miwili au mitatu kabla ya hapo, huko Friend's Corner, kuna mtu mmoja alimbaka na kumuua msichana mmoja lakini adhabu yake ya kifo ilifutwa. Nakumbuka kuwa kuna watu ambao walilalamika kuwa kwa nini mbakaji na muuaji asinyongwe, lakini mzee aliyempiga risasi RC aliyemtukana hadharani anyongwe. (Jibu wakati huo lilikuwa ni kwamba kesi moja ilikuwa ya jinai na kesi ya pili ilihusu maslahi ya Taifa na umma)Ndugu Maggid natoa kumbukumbu hizi ili kutoa perception ya wenyeji wa Iringa enzi hizo (karibu miaka 40 iliyopita). Hizo ni facts za kihistoria zilizojitokeza kortini na magazetini wakati huo. Huu ndio mchango wangu. Mwana-Isimani.

Mchango huu nimeutoa kwa bwana mjengwa.
 
Historia ya Isimani imejaa a lot of hardship. Wakulima waliohamia huko walikuta ni pori tuu na wakaclear mashamba na kuanza kulima kwa tabu sana, maji yanachotwa mbali, chakula shida, wanyama pori nao tele, etc.

Babu yangu alikuwa mmojawapo wa wakulima wa mwanzo huko Isimani; mama yangu anasimulia walivyokuwa wanaenda mbali sana kufuata maji ya kunywa na kupikia. Maisha yalikuwa duni na magumu sana. Ikumbukwe hii ni kabla ya sera ya vijiji vya ujamaa, azimio la Arusha nk. Sera hizi zilivyoingia mkoani Iringa, serikali iliwataka watu wote wahamie katika vijiji vya ujamaa na kuwe na communal farming. Hii iliwakuta wakulima wengi mahala pabaya sana manake mashamba waliotoil kuyalima yangechukuliwa kuwa ya vijiji vya ujamaa. Hatimaye walikubali ila ikaonekana kwamba kijiji cha ujamaa Isimani kina mashamba mengi tayari, na wakulima wengine wakakubaliwa waendelee kuyashughulikia mashamba yao zile siku ambazo sio za kijiji, na jumapili ndio siku isiyo ya kijiji na Mwamindi na wakulima wale wa mwanzo kule Isimani wakawa wanatend mashamba yao siku za jumapili.

Kutoka Iringa mjini Kleruu ameamua kwenda Isimani bila ya mlinzi/dereva. Ikumbukwe pia ameshakuwa very unpopular na wanyalukolo na word was out kuwa yeyote atakayempata kwanza ammalize (haya ni maneno ya wanyalukolo wa enzi hizo) Alipopita kwa Mwamindi na akamuona Mwamindi yupo shambani kwake ndipo akamfuata huko huko na kuanza kumkejeli. Inasemekana Kleruu alikuwa ana kifimbo kama kile cha Mwalimu na akaanza kumchomachoma kifuani Mwamindi huku akimwambia"wewe nani kakupa ruhusa kulima jumapili? Si ulitakiwa kulima kwenye shamba la kijiji cha ujamaa tuu?" etc etc.

Mwamindi akaingia ndani akachukua shot gun yake(nadhani ilikuwa zile wanaziita two-two rifle, popular sana enzi hizo) na akatokea kwa nyuma (nyumba za waHehe zina mlango/dirisha mdogo kwa nyuma) na akamtwanga risasi na kikafuata kilichoelezwa hapo juu. Ila alipofika Iringa alikwenda kwanza kwa wake zake na kuwaambia alichofanya ndipo akaenda police station. Kuna mzee mmoja alipishana na Land Rover ya Kleruu na akashangaa kumuona Mwamindi anaendesha, na hapo hapo akajua soo limetokea, akapita shambani kwa Mwamindi na akaelezwa kilichotokea. Vilevile, kule mtaani watu walishangaa Mwamindi anaendesha kari la mkuu wa mkoana limepaki kwake! Waliokuwa wanajua walielewa mara moja nini kimetokea!

Siku ile pale Isimani, the current popular mayor of Iringa was present as a very young boy. Maggid muulize atakupa story yote ya the first political assassination in Tanzania. Ya Karume ilikuwa next the following year, I think.
 
Mwaka 1971 hadi mwaka 1972 kulikuwa na operesheni vijiji ambapo watu walitakiwa kuhamia kwenye vijiji vya ujamaa. Mwamwindi alikuwa mmja wa wale waliokataa kuhamia vijijini. Siku ya Krismas mwaka 1971 (au 1972 hivi), Dr. Kreluu aliwatembelea wale waliokuwa wamekataa kuhamia vijijini na ndipo alipokumbana na hiyo dhahama. Kwa vile Kreluu alikufa, mpaka leo haijulikani walikosana nini na Mwamwindi kwa vile maelezo ya mwamwindi yaliyopitakana wakati anajitetea na hakukuwa na mtu mwingine wa kuyathibitiha. Kesi ya Mwamwindi iliendeswa mwaka 1973 na alinyongwa mwaka 1974 huko Dodoma.

Inapatikana kwenye law report? Ipi?
 
Back
Top Bottom