Dr. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

Saturday, 14 December 2013 ·

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa mpya baada ya kueleza kuwa kitakapofanikiwa kushika dola kitaruhu Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) kutengeneza mitambo ya kutengenezea pombe aina ya gongo. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini alisema kama gongo itatengenezwa kwa mitambo maalum itaondoa mianya ya rushwa kwa polisi ambao wamekuwa wakiwakamata wanaotengeneza kwa kificho na kuwafanya vitega uchumi vyao.

"Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi," alisema.

Mitambo hiyo itakayotengenezwa na SIDO itakapouzwa itaiingizia mapato serikali pia wauzaji wa gongo watafanya biashara hiyo kwa amani tofauti na sasa ambapo wanaifanya kwa kificho na wakikamatwa fedha zote wananufaika polisi.

Dk. Slaa alisema hata suala la kukamata watu wanaotengeneza silaha linapaswa kuangaliwa upya kwani wanaokamatwa wakifanya kazi hiyo wangekuwa wanashikiliwa kwa muda na baadaye wanapelekwa katika kiwanda cha serikali cha kutengenezea silaha ili watuhumiwa hao wapeleke ujuzi huo huko badala ya kuwafunga jela.

Dk. Slaa alisema matatizo yote yanatokana na wasomi kutofikiri namna ya kuisogea nchi mbele kimaendeleo.

"Nchi hii imelala, imechoka sababu waliopewa madaraka wamelala, wamejisahau hawatambui kuwa wamepewa nafasi hizo ili kuwatumikia wananchi," alisema.


CHANZO: NIPASHE

Mpaka hili vumbi la Zito lipite tutasikia mengi. Aliowaonaje wakazi wa Kasulu?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Nchini Kenya gongo (chang'aa) ni halali! Na watu wanalipa kodi..dk una akili sana
 
Nimesikitishwa na kauli ya kiongozi huyu wa Chadema kwamba wakishika dola wataruhusu na kuhalalisha utengenezaji wa pombe haramu ya gongo.
NDO UPEO WA MAWAZO YA DK umefika hapa?

Ukisikia matumizi mabaya ya muda ndiyo hayo, yaani mkuu unapoteza muda wako kwa kukaa na kumsikiliza mtu ambaye hana hata chembe ya busara ktk ubongo wake! Hili zee ni janga la Taifa, katu sitakubali kuongozwa na mtu kama hili zee.
 
Ukisikia matumizi mabaya ya muda ndiyo hayo, yaani mkuu unapoteza muda wako kwa kukaa na kumsikiliza mtu ambaye hana hata chembe ya busara ktk ubongo wake! Hili zee ni janga la Taifa, katu sitakubali kuongozwa na mtu kama hili zee.

Tusipomsikiliza tutamuelewaje mkuu?
Nina mashaka kuna siku atakuja na sera za Uchangudoa urasimishwe.
 
safi sana,kwanini tusitumie vya kwetu....mbona konyagi mnakunywa na TFDA imekiri kuwa inaharibu afya za watu
 
Nadhani huna hoja mzee bali matusi, dharau na kiburi bora nikuache na maisha yako!!!!!

Ngolombwe;
Haki siku zote huishi/hudumu,
Ukweli kwa mwenye kiburi siku zote huona ni matusi au uonevu,

Nimekuuliza katika viwango vya uelewa, sasa tusi lipo wapi ama ndo upeo wako hapo?

Kama pana matusi Mods ndo kazi yao kusimamia ilani humu,

Sasa kama huna jibu la maana katika swali la maana bora kukaa kimya si kulalamika lalamika,
Kwani nani atakufuata kukulazimisha ujibu?
 
Wachaga washamuambukiza ulevi Padri wa watu. Kusuhubiana na rafiki muovu ni jambo la hatari sana, asipokuchomea nguo bahati. Slaa kapangishe kwingine ila kwenye saccoss ya mtei umebugi men.
 
Dr slaa anavuta bangi chooni hii sio akili ya kawaida! Akitoka kuruhusu gongo atasema hat bangi iwe halali kama sigara
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom