Dr. Slaa; Tafadhali Uliza kwa SAUTI KUU haya!

Nasikitika kuwa hana sauti tena ya kuuliza hayo maswali?

Amebanwa sana kazi nyingi na hivi sasa mshahara hautoshi, and mchumba amekuw very demanding!

Naona umekuwa msemaji wa Dr.Slaa
Pole ana mchumba, lakini jitahiditahidi anaweza badilisha mawazo ukawa wewe ambaye sio demanding
 
Tunashukuru mkuu kwa kutushirikisha ni muhimu nasi tukaelewa nini umeuliza,na kama tz tumeshalipa hilo deni kwa haraka namna hiyo ni lazima tujue kuwa kuna wahusika wakuu wa hii nchi wana chao hapo thats why wanaharakisha deni lilipwe
Tambwe hiza ni kama konda wa daradara tu,leo atasema gari hili ni upepo bwana speed mia kesho atasema gari lile bwana kama mkokoteni ingwaje jana alilisifia,so tambwe anacheza na maisha yetu hatufai kabisaaaaaaa
watz tusimame kidete kupambana na hao wanao tuchezea kama wajinga vile

mapinduziiii daimaaaaa:kev::car::suspicious:
 
LHRC walipoenda kuulizia waliambiwa kesi imefunguliwa. Kesi hiyo ni No. 4 ya 2010. Ndipo walipoamua kuweka pingamizi. Lakini cha kushangaza baada ya kufuatilia wameambiwa kesi hiyo haipo waende Mahakama Kuu Masjala ya Kawaida!! Walipofika huko ndio wakakuta attachments zinazoonyesha mwenendo wa kesi ya ICC ambazo Rex ndio wamepeleka mahakamani kwa madai kwamba wametumiwa kwa DHL!

Hapa kuna maswali mengi sana. Kwa nini hili suala liwe na usiri mkubwa hivi? Ina maana hawa wenzetu haliwahusu? Hawana uchungu nalo? Wanataka tulipe?
Kwa nini hawatusaidii? Suala hili limebaki ni la wananchi ambao kilio chao ni sawa na kumulika giza nene na tochi!

Yaani, sina hata hamu ya kunywa bia yangu. Nani mtetezi wa serikali?
 
Yaani, sina hata hamu ya kunywa bia yangu. Nani mtetezi wa serikali?

Gurudumu, hawa jamaa wanalipa. Mahakama imetoa maoni yake (Msajili Bongole) kwamba wanaweza kulipana nje ya mahakama. Najiuliza je hiyo hela haikatwi kodi? Na kwa nini wasiipeleke mahakamani angalau walipe filing fee kabla haijalipwa? Angalau itapungua kidogo! Sitashangaa lakini wasipohangaika na kodi na fee za mahakama! Hata kama ni kidogo zinatosha kujenga maternity ward kwenye kata yangu yenye wananchi zaidi ya elfu 15 ambao kina mama wake hawana maternity ward for almost 40 years!

Tufanyeje? Nimekaa na rafiki yangu mmoja ananiambia 'siku nikimiliki bastola utasikia. Ningekuwa na bastola halafu polisi wawe wanavunja kioo cha gari kama walivyokuwa wanafanya arusha naua'......nikimuangalia machoni naona yuko serious. Anaongea ametulia na habahatishi!! Hana miaka 35!! Sasa jaribu kufikiria!
 
Sasa bado sijaelewa, hiyo kesi ya LHRC itasikilizwa au?

Kama kesi No. 4 ya 2010 haipo kesi ya LHRC na yenyewe haipo. Kama kesi haipo basi hakuna cha kusikilizwa. Gurudumu, ni ukweli unaouma kwamba hakuna pingamizi kuhusu malipo ya Dowans. Kama hawajapeleka maombi ya kusajili tuzo/hukumu huwezi kupinga!! Kwa hali iliyopo kuna kila dalili serikali italipa na Dowans hawatapeleka maombi ya kusajili tuzo/hukumu!!

Pingamizi pekee ni kuandamana mpaka Tanesco makao makuu na kuwafungia ndani wafanyakazi mpaka Raisi aje!! Unakumbuka enzi za utawala block udsm!
 
Nakumbuka lakini FFU hawakuruhusiwa kuingia main campus! Kwa hiyo atakuja Andengenye siyo JK!

Lakini, seriously, LHRC au Chadema hawawezi kuomba mahakama kuweka stop order ya malipo hadi hukumu hiyo ya ICC isajiliwe mahakama kuu?

Kwa hiyo lile tamko la wale wazee wa CC lilikusudia kututuliza wakati wao wanaendelea kulipa Dowans bila harakati zozote? Ndiyo maana walianza kwa kusema ni shurti kulipa?
 
Kwa uelewa wangu wa sheria hilo haliwezekani. Kikubwa ni utayari wa kisiasa. Sidhani kama viongozi wetu wana nia ya kutokulipa. Kwa maneno yao na vitendo vyao hawaoni tabu kulipa. Haiwanyimi usingizi kabisa. Mimi na wewe na wengineo ni kelele za mlango!!

Kungekuwa na nia ya dhati ya kutotaka kulipa basi tungeiona! Hapa tumekaangwa ndugu yangu! Naona kila dalili za kufika mwisho katika hili!
 
Nini nafasi ya bunge?
 
Back
Top Bottom