Elections 2010 Dr. Slaa awe kiongozi mkuu wa Chadema kuelekea Uchaguzi Mkuu?

CHADEMA wasilaumiwe mambo hayawezi kukaa vizuri mara moja;

Ni mchakato wa muda mrefu. Nafikiri CHADEMA ni vema wakazingatia ushauri.

unamaanisha nini??? tarehe 31 october si mbali,
mpaka sasa hatuwaoni kwenye TV waki campaign
 
hili la Dr Slaa VS Mbowe hata mimi limekuwa linaniumiza kichwa afadhali Mzee Mwanakijiji umelisemea.

kwa sababu Dr. Slaa anapaswa atoe ahadi ambazo anauhakika atazitekeleza bila kusubili au kutegemea viongozi wengine watasemaje.
pia kuna maswali yatakayo elekezwa kwake wakati wa kampeni atawezaje kujibu? anapaswa awe na power hiyo kimsingi
 
Chedema hawawezi kuongoza nchi. Wanaubinafsi na uroho wa madaraka. Mwaka huu wataanguka zaidi hata kuliko 2005.
 
usome kilichoandikwa usisome unachofikiria kimeandikwa.
Don't be biased Geza Ulole ame hit kabisa post yako labda yuko negative na mawazo yako, kasema si lazima Mwenyekiti awe mgombea urais nilitegemea haya maneno uliyomwambia GU utamwambia Nyani Ngabu ambaye yuko off topic kabisa linganisha hizi posts nani yuko off,
quote_icon.png
Originally Posted by Geza Ulole umechoka fikra na mawazo! si lazma Mgombea awe Mwenyekiti au Mwenyekiti awe Mgombea kwani katiba ya Chadema inasemaje? na pia huoni ni mzigo mkubwa wa Dr Slaa (rais Mtarajiwa) kuongoza chama na wakati huohuo kuongoza serikali?

quote_icon.png
Originally Posted by Nyani Ngabu Hata wafanyeje CCM watafunika tu....

Nimeshasema huko nyuma kuwa CCM is a juggernaut. Haiwezi kuanguka mwaka huu, 2015, 2020, au hata 2025. Yahifadhini haya maneno yangu ikiwezekana myawekee sticky nyinyi akina Invisible, Silencer, Painkiller, etc.

Baada ya kusema hayo mimi nafikiri huu sio muda mwafaka kwa chama kilicho kwenye kampeni kuanza kuzungumzia vyeo hata mwenyekiti wa Chadema Mbowe alishawahi kutamka hayo.

Pili naungana na Geza Ulole kuwa mgombea urais si lazima awe Mwenyekiti na si chadema pekee waliofanya hivyo TLP NRA NCCR havijaweka wenyeviti wao kuwa wagombea, hata Obama hakuwa Mwenyekiti wala kiongozi mkuu wa Democrats kama unavyosema.

Kuhusu kiongozi mkuu wa chama hilo linategemea na katiba inasemaje kila chama kina utaratibu wake wa uongozi. Hata CCM unayoisema mgombea wake ndiye m/kiti ina mpango wa kuachama na mtindo huo kwa vile haumpi muda wa kutosha rais kupumzika, yeye aongoze chama yeye huyo huyo awe amiri jeshi na kiongozi wa serikali ni mzigo mzito.

Vile vile si busara kwa mtu mmoja kulundikiwa vyeo kama vile chama hakina watu wengine wenye uwezo. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tunarudi kwenye enzi za zidumu fikra za m/kiti.
 
si lazima wabadilishe mwenyekiti; yaani mwenyekiti anaendelea kuwa Mwenyekiti lakini uongozi wa chama kimtazamo na mwelekeo unatolewa na mgombea wa Urais. Kwa hiyo hawahitaji kubadili Katiba ni makubaliano ya kimantiki tu.

Mzee, kila kitu kwa wakati wake, kwa sasa hivi tuna kazi moja tu kutafuta ridhaa ya wananchi katika nafasi hizi mbili. Tusichanganye mambo. Maana nafasi kwenye chama ni matokeo ya kura vilevile. Tukimaliza hili ni lazima wanachama warudi wapige kura waamue. Na sioni kwa nini isiwezekane kama kwa wenzetu waingereza (nashangaa unaangalia Conservative tu ) kuwa na mwenyekiti wa chama tawala ambaye si raisi! Demokrasia ingejikita vizuri pale Raisi anaweza akarudi kwenye chama na kuambiwa hapo ilani ya chama hujaipeleka sawa. Najua utadakia yale ya Zambia, lakini ni mawazo tu, na ningependa tusiwasukume sukume hawa chadema dakika hizi, mwishoni watapoteza mwelekeo.

Kwa lugha rahisi, Mzee naona unataka kuvuruga hawa halafu kwenye vurugu hilo CCM atavua samaki kibao!!
 
Don't be biased Geza Ulole ame hit kabisa post yako labda yuko negative na mawazo yako, kasema si lazima Mwenyekiti awe mgombea urais nilitegemea haya maneno uliyomwambia GU utamwambia Nyani Ngabu ambaye yuko off topic kabisa linganisha hizi posts nani yuko off,




Baada ya kusema hayo mimi nafikiri huu sio muda mwafaka kwa chama kilicho kwenye kampeni kuanza kuzungumzia vyeo hata mwenyekiti wa Chadema Mbowe alishawahi kutamka hayo.

Pili naungana na Geza Ulole kuwa mgombea urais si lazima awe Mwenyekiti na si chadema pekee waliofanya hivyo TLP NRA NCCR havijaweka wenyeviti wao kuwa wagombea, hata Obama hakuwa Mwenyekiti wala kiongozi mkuu wa Democrats kama unavyosema.

Kuhusu kiongozi mkuu wa chama hilo linategemea na katiba inasemaje kila chama kina utaratibu wake wa uongozi. Hata CCM unayoisema mgombea wake ndiye m/kiti ina mpango wa kuachama na mtindo huo kwa vile haumpi muda wa kutosha rais kupumzika, yeye aongoze chama yeye huyo huyo awe amiri jeshi na kiongozi wa serikali ni mzigo mzito.

Vile vile si busara kwa mtu mmoja kulundikiwa vyeo kama vile chama hakina watu wengine wenye uwezo. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tunarudi kwenye enzi za zidumu fikra za m/kiti.

jamani sijasema Dr. Slaa awe Mwenyekiti na Mgombea wa Urais!!!! Hii lugha mbona ni ya Kiswahili?
 
Kuna thread zingine hata zingekuwa na malengo mazuri kiasi gani timing yake inakuwa suspect. Tayari Mwanakijiji kwa kuanzisha hii mada anapanda mbegu kwenye mioyo ya wadandiaji fulani fulani kuwa kuna mgongano katika uongozi wa Chadema, kati ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu au kati ya mgombea Uraisi na mgombea Ubunge - hogwash !

Sikusikia hii wakati Mwinyi anafanya Kampeni Mwenyekiti wake akiwa Mwalimu Nyerere, sikusikia hii Mkapa akifanya kampeni huku Mwenyekiti wake akiwa Mwinyi na sikusikia mgongano wakati Kikwete anapiga kampeni Mwenyekiti wa CCM akiwa Mkapa. Hizi controversies zinazoanzishwa kuhusu Chadema at this time zina malengo gani kama si kuidhoofisha Chadema wakati uhai wa chama chochote cha siasa kwa wakati huu unategemea mshikamano na si vyeo ?
 
Mwanakijiji,
Mimi ni mwanafunzi wa historia. Naamini kabisa kuwa Dr. Slaa atakapokuwa rais atakuwa ndiye "main spokesman" wa CHADEMA. Tuachane for a minute na culture ya CCM ambapo Mwenyekiti wa chama alikuwa/ndiye rais wa nchi. Tunaweza kutumia altenative ya Marekani ambapo flag bearer katika uchaguzi anakuwa automatic party leader. Licha ya ushabiki wangu kwa Zitto au Mbowe, sasa hivi our flag bearer ni Dr. Slaa. Nitaendelea kuwaheshimu Mbowe/Zitto kama viongozi wetu lakini tunajua anayebeba bendera yetu ni Dr. Slaa. Na ikitokea hivyo CHADEMA will be writing a new page in our history kwamba siyo lazima uwe mwenyekiti wa chama kuwa flag bearer. Ni dalili njema.
 
Tatizo hapa ni kufikiri campaign team + manager= Mwenyekiti
You are right mawazo ya wengi yamejikita kwenye kampeni team yanasahau majukumu ya mwenyekiti ambaye ni kiongozi mkuu wa chama wherther kuna uchaguzi au hakuna, mwenyekiti wa chama anabaki na madaraka yake hanyang'anywi na mgombea yayote, hiyo ndiyo misingi ya chama.

Unaweza ukawa mwalimu mkuu lakini usijue kufundisha hesabu au PE na vile vile unaweza ukawa mwenyekiti lakini ukipewa ukatibu unakushinda and vice versa ila ukawa na sifa za kugombea urais, hatuwezi kuacha kukuteua ugombea urais kwa vile tu huna sifa za kuwa katibu.

Kipindi kama hiki ikiwezekana mgombea urais asiwe msemaji wa chama awe free yeye awe anakuwa directed na campeign team au manager, kama kampeni manager ni mwenyekiti wa chama sawa, huo ndio unaitwa utawala wa sheria siyo wa kubahatisha, kwa mfano leo Mutamwega Mugahywa – TLP anagombea urais basi Mrema amwachie uenyekiti nafikiri huo si utaratibu mzuri.
 
Kuna thread zingine hata zingekuwa na malengo mazuri kiasi gani timing yake inakuwa suspect. Tayari Mwanakijiji kwa kuanzisha hii mada anapanda mbegu kwenye mioyo ya wadandiaji fulani fulani kuwa kuna mgongano katika uongozi wa Chadema, kati ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu au kati ya mgombea Uraisi na mgombea Ubunge - hogwash !

Sikusikia hii wakati Mwinyi anafanya Kampeni Mwenyekiti wake akiwa Mwalimu Nyerere, sikusikia hii Mkapa akifanya kampeni huku Mwenyekiti wake akiwa Mwinyi na sikusikia mgongano wakati Kikwete anapiga kampeni Mwenyekiti wa CCM akiwa Mkapa. Hizi controversies zinazoanzishwa kuhusu Chadema at this time zina malengo gani kama si kuidhoofisha Chadema wakati uhai wa chama chochote cha siasa kwa wakati huu unategemea mshikamano na si vyeo ?

Nami nilikuwa na maelezo kama hayo ya kwako (in blue).

Nchi hii hakika CCM itatawala kwa miongo mingi ijayo, kama wasomi wenyewe ndio wana mawazo haya.
 
Mimi sikubaliani na hili na si kweli kwamba maraisi wote ni wenyeviti. Obama ni kiongozi wa Democratic lakini si mwenyekiti wa chama!!. Chadema kinaendeshwa vizuri sana sasa na nisingependa Mbowe atolewe kwenye nafasi hiyo. Mbowe siyo mwanasiasa mzuri au mahiri lakini ni manager mzuri na nafasi ya mwenyekiti inahitaji manager na siyo mwanasiasa. Kwasasa Dr Slaa anaweza kuwa kiongozi wa chama bila kuwa mwenyekiti kama ilivyo Marekani. Watu wengi wanasema Mbowe atolewa lakini Chadema ni imara kwasababu Mbowe ni manager mzuri sana.
 
Chedema hawawezi kuongoza nchi. Wanaubinafsi na uroho wa madaraka. Mwaka huu wataanguka zaidi hata kuliko 2005.

Audax sounds like such a nice and beautiful name, what a shame !
 
wakati mwingine ukiwa unapenda kila kitu kukifikiri sana unaweza kugeuka chizi. Kuongoza chama maana yake nini?kuwa mwenyekiti maana yake nini? hebu mwanakijiji tuelekeze vizuri wewe unawazaje. Yaani ukiwa mgombea uraisi upewe uongozi wa chama lakini usiwe mwenyekiti??@@ hii ikoje mbona siipati, au ndo iko juu sana ya uwezo wangu. fafanua tafadhali. kwani mifano yako kweli kama walivyosema wenzangu hai-apply kwa Obama wala Kikwete alipokuwa anagombea mwaka 2005, na wote walikuwa si wenyeviti wala viongozi wakuu wa vyama

Au ulikuwa unamaanisha awe ndio msemaji mkuu wa sera za chama hasa kwakuwa yeye ndio ana nafasi kubwa na nzuri ya kuzinadi kupitia kampeni....???
 
CHADEMA wasilaumiwe mambo hayawezi kukaa vizuri mara moja;

Ni mchakato wa muda mrefu. Nafikiri CHADEMA ni vema wakazingatia ushauri.
Watu wanataka yawe mazuri over a night Chadema iwe na uongozi mzuri kesho, ifike vijiji vyote kesho, ishinde urais kesho, ibadili uongozi kesho, wasipofanya hivyo hawafai kupewa uongozi. Hawaelewi kuwa hayo yote yanahitaji time, resources na watu, na watu wenyewe ndio sisi hatutegemei waje toka Norway au Zambia.

Wakati tunataka kitu tujaribu kuangalia reality, mfano tunalaumu Chadema haijaweka wagombea kwenye majimbo yote. Hatujiulizi kwa nini, kwani chadema haitaki wabunge, kuna constraints ambazo tunaacha kuzizingatia sijui kwa ni kwa makusudi au.

Angalia wagombea wangapi wa Chadema wamewekewa pingamizi za ajabu ajabu na wasimamizi wa NEC wamezikubali, mfano Mwanza mjini eti si raia, chukulia MO waliwekeana pingamizi yake ikapita angalia uraia wa Bashe na wa Kigwangala. Kama wewe si mshabiki vitu kama hivi ni vya kuangalia lakini tukiwa tunajadili huku tukitawaliwa na ushabiki vitu vya msingi hatuwezi kuviona.

Utakuta mtu anasema Chadema hakifai kupewa nchi au CCM wameshindwa kuongoza bila kusema kwanini wameshindwa, na si uongo wote tunazama humo matokeo yake tunajaza page bila ku gain chochote.
 
Watu wanataka yawe mazuri over a night Chadema iwe na uongozi mzuri kesho, ifike vijiji vyote kesho, ishinde urais kesho, ibadili uongozi kesho, wasipofanya hivyo hawafai kupewa uongozi. Hawalewi kuwa hayo yote yanahitaji time, resources na watu, na watu wenyewe ndio sisi hatutegemei waje toka Norway au Zambia.

Wakati tunataka kitu tujaribu kuangalia reality, mfano tunalaumu Chadema haijaweka wagombea kwenye majimbo yote. Hatujiulizi kwa nini, kwani chadema haitaki wabunge, kuna constraints ambazo tunaacha kuzizingatia sijui kwa ni kwa makusudi au.

Angalia wagombea wangapi wa Chadema wamewekewa pingamizi za ajabu ajabu na wasimamizi wa NEC wamezikubali, mfano Mwanza mjini eti si raia, chukulia MO waliwekeana pingamizi yake ikapita angalia uraia wa Bashe na wa Kigwanagala. Kama wewe si mshabiki vitu kama hivi ni vya kuangalia lakini tukiwa tunajadili huku tukitawaliwa na ushabiki vitu vya msingi hatuwezi kuviona.

Utakuta mtu anasema Chadema hakifai kupewa nchi au CCM wameshindwa kuongoza, na si uongo wote tunazama humo matokeo yake tunajaza page bila ku gain chochote.
Mkuu Luteni
ndio maana nimegombana sana na mmoja wao kwenye thredi nyingine kwani anafikiria hizi siasa za kwenye internet ni sawa na za huko majimboni!!!
 
On Obama's campaign I read the following:-

The Democratic National Committee provides national leadership for the Democratic Party of the United States. It is responsible for promoting the Democratic political platform, as well as coordinating fundraising and election strategy. Shortly after his inauguration, Barack Obama transferred his Obama For America organization to the DNC


Ref. (http://en.wikipedia.org/wiki/Democratic_National_Committee)
 
Mimi nadhani kinachotakiwa ni utaratibu unaweza kuleta Ushindi tu. Kuna nguvu mbili hapa.. ile ya chama kwa wagombea wote na ile ya rais mtarajiwa ambaye pia huwa na team yake maalum aliyoipendekeza yeye..Yaani mgombea urais huanza kuunza nguvu ya kuongoza toka wakati wa kampeni za kuingia Ikulu na mara nyingi chama hupanga jinsi ya kuwashirikisha wote wawili ktk jukwaa moja kuuza sera na Ilani za chama..

Kama sikosei Obama alifanya hivyo toka akishindana na Clinton na hadi kitaifa na McCain wakati wote alikuwa na kampeni team yake na sio ya chama. Kwa hiyo kama Dr. Slaa alimchagua Mbowe au Zitto kuwa mwenyekiti wa kampeni zake sioni sababu ya kumwondoa Mbowe/Zitto hali Dr.Slaa na team yake wanaridhika. Tunachoweza kuhofia tu ni kama chama hakikumpa nafasi Dr. Slaa kuchagua team yake ya kampeni na pengine jinsi Dr. Slaa anavyotaka kujitangaza. Lakini wakati huo huo ktk kampeni za wabunge wengine woote chama kina sauti kubwa zaidi ya kupanga nani atakuwa wapi na wapi ktk kushiriki kuwauza hawa wabunge kama wanavyofanya CCM wakimtumia zaidi Malecela.

Chama kitampa mwongozo wake na watasimama nyuma yake na siio chama kusimama mbele ya Dr. Slaa ktk maswala ya uchaguzi na hata kuunda serikali. Ifahamike tu huu ndio mwanzo wa kutafuta Urais, madaraka ya chama yanpokwenda nje ya chama ndio mwanzo wa chama kumchagulia/teulia rais watu ktk nafasi za Uongozi wa nchi.. Rais mtarajiwa ndiye anayetakiwa kuchagua watakao ongoza kampeni yake na sio lazima yeye awe Mwenyekiti wa Kampeni ya Uchaguzi na sio kabisa awe mwenyekiti wa chama kwa sababu hiyo hiyo, ila kama atapenda kuwa mwenyekiti wa kampeni YAKE, basi chama hakina sababu ya kukataa.
 
Mwanakijiji,
Mimi ni mwanafunzi wa historia. Naamini kabisa kuwa Dr. Slaa atakapokuwa rais atakuwa ndiye "main spokesman" wa CHADEMA. Tuachane for a minute na culture ya CCM ambapo Mwenyekiti wa chama alikuwa/ndiye rais wa nchi.

Duh jamani ndio maana kwa makusudi nimekwepa kusema Dr. Slaa awe "Mwenyekiti" wa Chadema.

Tunaweza kutumia altenative ya Marekani ambapo flag bearer katika uchaguzi anakuwa automatic party leader.

Thats what I A M SAYING.

Licha ya ushabiki wangu kwa Zitto au Mbowe, sasa hivi our flag bearer ni Dr. Slaa. Nitaendelea kuwaheshimu Mbowe/Zitto kama viongozi wetu lakini tunajua anayebeba bendera yetu ni Dr. Slaa. Na ikitokea hivyo CHADEMA will be writing a new page in our history kwamba siyo lazima uwe mwenyekiti wa chama kuwa flag bearer. Ni dalili njema.

ndicho ninachoitisha; je Mbowe, Zitto na viongozi wengine wa Chadema wako tayari kusimama nyuma ya flag bearer? Au wanaweza kumoverule wakati wa kampeni.
 
Chama kitampa mwongozo wake na watasimama nyuma yake na siio chama kusimama mbele ya Dr. Slaa ktk maswala ya uchaguzi na hata kuunda serikali. Ifahamike tu huu ndio mwanzo wa kutafuta Urais, madaraka makubwa ya chama yanpokwenda nje ya chama ndio mwanzo wa chama kumchagulia rais watu ktk nafasi za Uongozi wa nchi.. Rais mtarajiwa ndiye anayetakiwa kuchagua watakao ongoza kampeni yake na sio lazima yeye awe Mwenyekiti wa Kampeni ya Uchaguzi na sio kabisa awe mwenyekiti wa chama, ila kama atapenda kuwa mwenyekiti wa kampeni ya uchaguzi basi chama hakina sababu ya kukataa.

kwa mfano, Dr. Slaa anataka x na timu yake aliyoiunda inataka x lakini Uongozi mwigine wa chama unasema unataka "y" na Mwenyekiti anataka "y" Dr. Slaa afanye kile wanachotaka viongozi wa juu wa chama au kile ambacho anajua ni bora kwa kampeni ya Urais na kinachofaa kuelekea kupata ushindi? Kama akisema "nitafanya "x" je uongozi wa chama uko tayari kusupport maamuzi yake au utagawanyika kwa sababu Mwenyekiti alikuwa anataka "y" na watu wake nao walikuwa wanataka "y"?
 
Back
Top Bottom