Ilikuwa majira ya saa 10:30 mchana alitua na Helkopta kama kawaida. Alizungumzia mambo ya msingi yatakayofanyika siku Chadema itakapoingia madarakani:
1. Kushusha bei ya vifaa vya ujenzi ili wananchi wajenge nyumba za maana.
2. Elimu: Tunapofungua milango yetu kuhusu ajira na huku Watanzania tukiwa nyuma kielimu ipo siku tutashangaa afisa mtendaji wa kata atatokea Uganda.
3. Kupunguza gharama ya uendeshaji wa Serikali: Yeye kama rais atapunguza bajeti ya nyumba ya rais, atatembelea Landcruiser la thamani ya milioni 100 badala ya shangingi la milioni 200 ili aokoe milioni 100. Alisema kuwa ni muda wa serikali kukaza mkanda na wananchi kulegeza mikanda.
Kwa kifupi watua walijaa uwanjani huku Dr. Slaa akitumia dakika kama 30 na hatimaye akaelekea Endabsh hadi Karatu na kabla ya hapo alikuwa akitokea Dongobesh