DR.Slaa amgomea KIKWETE

The Magnificent

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
2,694
1,247
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameeleza kushtushwa na kauli ya Rais Jakaya Kikwete inayolenga kuzuia wananchi kujadili kuhusu Muungano wakati wa mchakato wa marekebisho ya Katiba.

Dk. Slaa aliye katika ziara ya kichama kukagua uhai wa chama hicho ikiwa ni pamoja na kukijenga, alitoa dukuduku lake hilo jana wakati akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shycom, mjini Shinyanga.
Katibu mkuu huyo wa CHADEMA alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tu tangu Rais Kikwete alipowaapisha wajumbe 30 wa Tume ya kukusanya maoni ya Katiba mpya inayoongozwa na mwanasheria na mwanasiasa anayeheshimika, Jaji Joseph Warioba.
Wakati akizindua tume hiyo juzi, pamoja na mambo mengine, Rais Kikwete alisema tume hiyo katika kazi yake haitahusika katika kuhoji kuhusu kuwapo ama kutokuwapo kwa muungano.
Kwa upande wake Dk. Slaa aliwataka Watanzania kuachana na maneno ya watawala na kutobweteka baada ya kuundwa kwa tume hiyo ya Jaji Warioba.
“Jamani Watanzania wenzangu wa Shinyanga, naomba tuzungumze kidogo hili la Katiba mpya, kwanza nawaomba msibweteke eti kwa sababu tume imeundwa, kuundwa tume hakuleti katiba mpya na bora. Pia tunataka Kikwete ajue kuwa Watanzania hawatengenezi katiba ya Kikwete wala ya CCM. Wanataka Katiba mpya na bora ya kwao.
“Nami namuomba ni bora akajitahidi kujiepusha na matamko ya ajabu, maana anaendelea kutupatia ajenda. Anasema suala la muungano lisijadiliwe wakati wa mchakato wa utoaji maoni. Hapa anataka kutuma ujumbe gani…” alisema Dk. Slaa na kushangiliwa.
Akiuchambua muungano, Dk. Slaa alisema ni haki ya Watanzania kwa maana ya wale wa Zanzibar na wa Bara kujadili muungano wanaoutaka kwani kufanya hivyo hakuna nia ya kuuvunja.
“Sisi CHADEMA tunasimamia nini? Tunataka Watanzania wajadili wanataka muungano wa aina gani, tunataka Zanzibar ipate haki zake kama ilivyokuwa mwaka 1964.
“Hapa hoja si muungano uwepo ama usiwepo, hoja ni aina gani ya muungano wa kisiasa Watanzania wanautaka. Tunaamini kuwa hakuna mwanasiasa mwenye akili timamu anaweza kuhubiri kuvunja muungano.
“Mwanasiasa anayezungumzia kuvunja muungano huyo ni mwendawazimu, maana muungano wa kweli wa Watanzania uko kwenye damu zao. Lakini katika suala la kiutawala wananchi waachwe waamue wanataka aina gani, hii ndiyo hoja hapa,” alisema Dk. Slaa.
Akifafanua, Dk. Slaa alisema wanazo taarifa kwamba tayari CCM kupitia katika Halmashauri Kuu yao ya Taifa wameshafikia hatua ya kuwatumia makada wao, wakiwamo viongozi wa kiserikali kama wakuu wa mikoa na wilaya katika kuhakikisha yale ambayo chama hicho tawala kinayataka, yanaingizwa katika Katiba mpya.
“Napenda kumwambia haya huku akijua kuwa, mkononi kwangu au ofisini kwetu tayari tunao uamuzi wa Halmashauri Kuu ya chama chao, ambayo imewaagiza viongozi ambao ni makada wao, kuhakikisha masuala ambayo chama hicho kinataka yanaingia katika Katiba mpya, hii ni hatari,” alisema Dk. Slaa.
Akifafanua, alisema chama hicho kitaendelea kuwa mstari wa mbele kuwaongoza Watanzania waandike Katiba mpya inayozingatia haki za msingi kama vile masuala ya ardhi, huku pia akisisitiza kuwa suala la mamlaka ya rais linapaswa kuangaliwa upya na kurekebisha.
Aliongeza kuwa, moja ya mwarobaini wa kuachana na wateule wengi wa rais ni kuwa na serikali za majimbo ambako viongozi wake sharti wachaguliwe na watu badala ya sasa wananchi kutawaliwa na mkuu wa mkoa au wilaya wasiyemjua.

Source:
Tanzania daima.



h.sep3.gif


juu
blank.gif
 
Bila kujadili muundo wa muungano ni sawa na serikali ya CCM kutaka kubaka maoni ya wananchi Tanganyika na Zanzibar siyo za wanaccm bali ni za watu wote yaani watanzania .Tutaujadili huo muungano hakuna wakutunyima haki yetu kama watanzania.
 
hivi inakuwaje binadamu wa kawaida anajipa madaraka ya Mungu ya kuamua kipi kijadiliwe na wananchi na kipi kisijadiliwe? daah nachoka nikipatazama hapo tu...
 
Kwanini jk anapanga mambo ya kujadili na yasiyoyakujadili kwenye mchakato wa katiba? Wananchi wataamua na sio yeye
 
haya wakuu wa wilaya na mikoa wapo busy na kutekeleza mkakati wa ku manipulate process ya kupata Katiba. Nayo hii inaonyesha CCM wameshazima machine ya kutimiza ahadi za mr.JK ambaye yupo tayari ahaidi loote. Sasa CDM wakianza press accellerator CCM wataparalyse kabisa hadi uchaguzi ,Halafu CDM waje na kila hadi,huku wakiwaumbua wale wapenda ahadi (km za mademu na ndoa wakati wanazalishwa before ndoa na hakuna kuolewa). Na kupiga bao rahisi by that time atakuwa na wasikilizaji wa Chekechea wakiwa na juice za bure na pipi, huku wengine wakiita CCM yanga.
 
Back
Top Bottom