Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Alipokuwa kwenye kampeni zake katika kanda ya Ziwa, Dr. Slaa alionyesha kukerwa na mkakati wa Dr. Magufuli - Waziri wa uvuvi na ufugaji - katika kupambana na uvuvi haramu.
Kwa Dr. Magufuli ni kuharibu nyavu za uvuvi haramu ambazo yasadikiwa zinavua samaki wachanga na ambazo husababisha kupungua kwa kasi ya kukua kwa uzao wa samaki. Hivyo, kuwaharibia nyavu wavuvi hao Dr. Magufuli anaamini ya kuwa kwanza anawaongezea gharama za uvuvi haramu wahusika hao na pili analinda uzao wa samaki hao kutovunwa au kubakwa mapema mno kwa vichanga hivyo..
Kwa Dr. Slaa kitendo cha kuchoma nyavu ni uchafuzi wa mazingira. Nyavu zingeliweza kurudishwa kiwandani na kutengenezwa upya badala ya kuchomwa kwa nyavu hizo. Lakini kubwa zaidi mbona hao wakubwa wenye hivyo viwanda au wasafirishaji na wauzaji wa hizo nyavu zinazokamata samaki wachanga hawathibitiwi?
Sasa inakuwaje mvuvi ambaye ana kipato kidogo aumizwe na hatua za serikali wakati yule aliyemsababishia madhara hayo anaachwa aendelee na biashara yake hiyo haramu?
Haya ni maswali ya kimsingi kabisa na ndiyo maana vita dhidi ya uvuvi haramu havina mafanikio kwa sababu vita hivyo havitafuti kumaliza kiini cha tatizo ila kumjenga Mheshimiwa Magufuli ili aonekane machoni pa watanzania kuwa anachapakazi lakini ukweli ni kuwa anatwanga maji kwenye kinu.............