Dr. Shein amteua Joel Thomas kuwa mjumbe wa baraza la wawakilishi

Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
4,896
1,862

Wadau, kuonyesha wazanzibar ni wamoja na hawana matatizo ya kidin, shein amemteua "Mkristo" kuingia barazani. hii itaondoa propaganda zinazoenezwa na wasioitakia mema znz

Na Juma Mohammed,
MAELEZO Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein,amemteua Marina Joel Thomas kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee,kwa vyombo vya habari imesema uteuzi huo umeanza Juni 17 mwaka huu.
Rais amefanya uteuzi huo chini ya kifungu 66 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Katiba ya Zanzibar inampa uwezo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuteuwa watu kumi kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Walioteuliwa kupitia nafasi hizo na nyadhifa zao za sasa kwenye mabano ni Balozi Seif Ali Idd(Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar), Mohammed Aboud Mohammed(Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais) Omar Yussuf Mzee(Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo).
Wengine ni Zainab Omar( Waziri wa Ustawi wa Jamii,Maendeleo Vijana Wanawake na Watoto), Ali Mzee Ali, Sira Mwamboya (Naibu Waziri wa Afya) Juma Duni Haji (Waziri wa Afya), Fatma Abdulhabib Ferej(Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais) Ramadhan Abdallah Shabaan( Waziri wa Ardhi, Maji na Maendeleo ya Makaazi) na Marina Joel Thomas.

sosi: Rais wa Zanzibar Dk. Shein amteuwa Marina Joel Thomas | Mzalendo.net
 
mkristo mmoja zanzibar...wazenji wako wangapi kwenye tanganyika yetu...anyway mmoja is better than nothing
 
Kwanini Sasa, angefanya 2010 baada ya Uchaguzi hapo ingekuwa swafi sana sio sasa hivi labda

kapigiwa simu na wafadhili, ICC imekodolea Macho, labda kaisha ambiwa ukijitenga ulivyo sasa

hatukutambui hata kidogo.

Mabadiliko kwa Presha sio Mabadiliko hata kidogo
 
Naona anataka kuwapoza Wakristo kwa kuchomewa makanisa - a drop of water in the ocean!
 
Ni hatua nzuri lakini kwa nini hakufanya hivyo tangu awali? Miaka miwili na nusu yuko ofisini hakuona ulazima? Na kama makanisa yasingechomwa angefanya huu uteuzi? Haya ni maswali ambayo nadhani watu wengi watakuwa wanajiuliza.
 
Kwanini Sasa, angefanya 2010 baada ya Uchaguzi hapo ingekuwa swafi sana sio sasa hivi labda

kapigiwa simu na wafadhili, ICC imekodolea Macho, labda kaisha ambiwa ukijitenga ulivyo sasa

hatukutambui hata kidogo.

Mabadiliko kwa Presha sio Mabadiliko hata kidogo

Hivi Watanzania sijui huwafanyie nini aisee!
 
Hakuna lolote. Changa la macho tu. wasubiri uchaguzi Tz bara 2015 ndiyo mbivu na mbichi ya udini itajulikana!! Miaka hii kumi Tanzania bara tumejifunza mengi ya udini na ukabila!!!! Kanda ya kaskazini haitakiwi kabisa katika post za juu serikalini!! Sorry to say this but ndiyo ukweli mpaka maongezi informal yapo!!!!!!!!!!
 
Ni hatua nzuri lakini kwa nini hakufanya hivyo tangu awali? Miaka miwili na nusu yuko ofisini hakuona ulazima? Na kama makanisa yasingechomwa angefanya huu uteuzi? Haya ni maswali ambayo nadhani watu wengi watakuwa wanajiuliza.

FJM,
Tatizo lako wewe unakubali mambo ya Slaa, tu...Dr Shein kathubutu nani Zanzibar kaishafanya hivyo? Tuache ushabiki.
 
Hakuna lolote. Changa la macho tu. wasubiri uchaguzi Tz bara 2015 ndiyo mbivu na mbichi ya udini itajulikana!! Miaka hii kumi Tanzania bara tumejifunza mengi ya udini na ukabila!!!! Kanda ya kaskazini haitakiwi kabisa katika post za juu serikalini!! Sorry to say this but ndiyo ukweli mpaka maongezi informal yapo!!!!!!!!!!

Hahahahahaa!!!
Watawaweza hao wanaoitwa wa kaskazini!!??
Wamuondoe Utoh tuone!!!
 
Hongera zake ila nataka kujua anatoka ccm ipi ktk mbili zinazo tawala zanzibar?
Ccm A au ccm B?
 
mkristo mmoja zanzibar...wazenji wako wangapi kwenye tanganyika yetu...anyway mmoja is better than nothing

Shein ana nafasi 10,

Ikiwa population ya zanzibar waislam ni zaidi ya 95%, basi kuchagua mkristo mmoja kutoka nafasi 10 ina maana 10% ya nafasi zake katumia kwa WAGALA sio mbaya jamani, tumuunge mkono.
 
FJM,
Tatizo lako wewe unakubali mambo ya Slaa, tu...Dr Shein kathubutu nani Zanzibar kaishafanya hivyo? Tuache ushabiki.

Ni wapi nimemtaja Slaa? Na kwa nini you are equating Dr Shein na Dr Slaa?
 
Back
Top Bottom