Dr. Reginald Mengi's Presentation on Local participation in the OIL & GAS industry in Tanzania

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
LOCAL PARTICIPATION IN THE OIL & GAS INDUSTRY IN TANZANIA BY DR. REGINALD A. MENGI, CHAIRMAN
TANZANIA PRIVATE SECTOR FOUNDATION
24TH OCTOBER, 2013 DAR ES SALAM


1.0 INTRODUCTION


We all agree on the necessity for local participation in the emerging oil and gas industry in Tanzania. The critical question we need to ask ourselves is what will pave the way for such participation? In the view of Tanzania Private Sector Foundation, it must be a deliberately designed policy that ensures guaranteed levels of local participation in the industry.

If there is much that has been said recently about local participation in the Oil and Gas industry it is because of TPSF's fear that history may repeat itself; in that, a century after gold and diamond reserves were discovered in Tanzania, to this date, the majority of Tanzanians are only playing a marginal role – as artisan miners; low and mid-level employees or suppliers of minor goods and services to international mining companies. Accordingly, concrete steps by the Government and Private Sector are necessary to demonstrate that this phenomenon shall never repeat itself.

TPSF is not in doubt that the Government recognizes the necessity for the empowerment of Tanzanians. This is clearly contained in the policy the Government articulated in its National Economic Empowerment Act of 2004 that: "Natural resources, trade, agriculture industry and other economic opportunities must generate wealth, boost the small and medium enterprise sector, in order to bring about a sustainable affirmative action and facilitate genuine and positive economic empowerment to the population of Tanzanians". It further states that: "Economic empowerment is a central means for bringing about economic growth and social.

Justice among our people that is necessary for the promotion of peace, tranquility and social stability that has characterized our society". Unfortunately, the National Economic Empowerment Act was not implemented in a manner that would have empowered Tanzanians in the mining sector. In consequence, Tanzania should not now shy away from this golden opportunity which will wipe our years of agony caused by the mining sector in this country. We have been blessed with a second chance and let us fully utilize it to create sustainable local participation that will benefit future generations.


2.0 ECONOMIC EMPOWERMENT OF TANZANIANS IN OIL AND GAS INDUSTRY

The overall empowerment of Tanzanians to participate in the oil and gas industry is therefore crucial and in line with the National Economic Empowerment Policy, 2004 and the National Economic Empowerment Act, 2004. The objective is to ensure that we adopt inclusiveness approach to enable Tanzanians and Tanzanian firms to partner with foreign firms at all levels of the value chain – upstream, midstream and downstream.

Tanzania Private Sector Foundation therefore advocates for the enforcement of the National Economic Empowerment Act 2004 which calls for affirmative action to enable Tanzanians to participate effectively and productively in the oil and gas sector rather than remaining spectators. TPSF notes that the Government has developed a natural gas policy which focuses on regulating the mid and downstream activities but it has no link to the National Economic Empowerment Policy.

This is a serious weakness that should be addressed quickly by all of us. It is important to note that the country has no policy to regulate UPSTREAM development in the gas industry, in particular, the allocation of blocks, which would take into account the provisions of the National Economic Empowerment Policy, 2004.

3.0 THE EXPERIENCE OF OTHER COUNTRIES

Many countries, including Mozambique, Uganda, Angola, Libya, Algeria, Ghana and Saudi Arabia are now seeking to create more in value through local content. The most successful countries that have achieved a national content level of 40%-80% include Brazil, Malaysia, the United Kingdom, and Norway. Many others which are struggling to reach 25%-30% include Nigeria, Angola, Trinidad and Tobago, Saudi Arabia, and Libya.

3.1 THE CASE OF NIGERIA

In 2010 the Nigerian National Assembly enacted a law titled "Nigeria Oil and Gas Content Development Act" whose main objective is to ensure Nigerians participate effectively in the oil and gas industry. Section 3 (1) of the Act states that Nigerian Independent operators shall be given first consideration in the award of oil blocks, oil field licenses, oil lifting licenses and in all projects for which contract is to be awarded in the oil and gas industry subject to fulfillment of such conditions as may be determined by the Minister.

As a result of the affirmative action, to-date Nigeria has allocated 52% of the 173 awarded blocks to Nigerians and 48% have been given to foreign companies. Nigeria has discovered a total 388 oil blocks. As a result of this move Nigeria has created wealth owned by Nigerians which can be confirmed by the recently published list of 30 billionaires of which the top three are all in the oil and gas business but the list has 14 billionaires investing in oil and gas industry.

3.2 THE CASE OF BRAZIL

Brazil has a law which: aims to grow the local labour market, technology, and its competitiveness; requires oil and gas
companies to contract with Brazilian suppliers; and has a minimum local content requirement for exploration projects of 55%. Ultimately, the local content policy framework in Brazil, due to the Government's strategic push and leadership, has seen policies converted into actionable and measurable impact and the local supplier force has grown extensively over the last three years.

3.3 THE CASE OF ANGOLA

In its effort to ensure local participation by Angolan suppliers in the oil and gas supply chain, Angola has identified a number of products and services which Angolan suppliers have competence in and this group has been categorized as opportunities for Angolan suppliers ONLY.

Because foreign companies have many advantages over local companies, what Angola has done is to stipulate that when a local company can meet the time, quality and quantity requirements but is higher on price, they will be given preference if they are 10% within the required price. 10% may be too low but at least Angola has been specific in its stipulation.

4.0 PARTICIPATION OF TANZANIAN LOCAL FIRMS – A PROPOSED CONTRACTUAL STRATEGY FRAMEWORK


- To maximize Tanzanian Content in the development of gas projects, a list of broad contract categories have been identified. Local content must aim at increasing local participation and develop local capacity towards international competitiveness. Thus, local content development on the back of contracts has been identified as the best model to drive capacity building and local participation. This gives an overview of a strategic case and proposed contractual framework which will guarantee that local suppliers in Tanzania participate in this new market.

- Invitations to Tender need to create an environment promoting local participation. The following activities that will potentially take part in Tanzania need to be considered for local participation:

o For survey service-based contracts (Environmental Impact Assessment, Geotechnical/Geophysical Surveys and Metocean Data).

o The Government should identify individual areas of expertise that are required as part of FEED and assess in which of these Tanzanian firms have competence (i.e. risers, flow lines, PLEMs, umbilicals, manifolds and foundations, subsea control system and Xmas trees). All FEED work carried out shall include the use of all available materials, facilities and installation equipment locally available in Tanzania. This will be a crucial evaluation criterion in all FEED contract packages.

o When it comes to Detailed Engineering Design work, the international contractor should go into a joint venture/partnership with competent and capable Tanzanian engineering companies with a capacity to deliver on small elements (work packages) that can be locally executed. These must however be domiciled in the country. These alliances must show clear evidence that they support technical growth and improve their capacity to compete for the contracts.

o Other areas of focus that the Tanzanian Government must mandate 1st tier construction contractors to sub-contract to Tanzanian firms must include roads, mechanical and electrical works, painting, insulation, machine operation and building services.

o The Government must require suppliers of subsea hardware to carry out their Systems Integration Tests in Tanzania.

o Fabrication has been identified in several countries as a major area of focus in Local Content Development. The Government should ensure that piles, decks, anchors, buoys, jackets, pipe racks, bridges, flare booms and storage tanks will be fabricated locally as far as possible. It is said to take at least 5 years to develop a fabrication yard and competence from scratch. With the production date set for 7 to 10 year timeline, this calls for fabrication development initiatives to start YESTERDAY. We are already running behind.

o Like Norway, Tanzania should require for Research & Development Centers be established in Tanzania. This will ensure that technology transfer takes place.

- The emphasis therefore is towards knowledge transfer so that in future these firms can compete independently and even act as mentors to other Tanzanian companies that lack technical capacities to be globally competitive.

- Tanzania signs PSA with the operators but it is not the operators who do most of the work. A big chunk of the work is being done by what is being referred to as Tier 1 Suppliers. How then does the Government ensure that these Tier 1 Suppliers do create an environment that accommodates local participation? It is a common practice in countries where is a local content policy that it is the operators who have the responsibility to ensure that Tier 1 Suppliers do create this environment. Operators are made accountable for their Tier 1 Suppliers.


5.0 ISSUE OF CAPITAL AND EXPERTISE

Tanzanians fully recognize that exploration and extraction of minerals be them gold, oil or gas requires "rare skills" and vast amount of capital. This creates considerable reliance on foreign investors. On the other hand, Tanzanians have their vast mineral resources, which the foreign investors do not have and at this time Tanzania offers an attractive climate for their investment. Thus, Tanzanians (not only through their Government but also through their Private Sector) would be bringing their mineral resources (gold, oil, gas etc.) to the table and, likewise, the foreign investors bring their "rare skills" and vast amount of capital (which is what they have) to the table in agreed proportions. This is what partnership is all about! So, this notion of Tanzanians being weak and lacking capital is imaginary and should be discarded. The minerals are a huge part of the capital.

The issue is how the Tanzania Private Sector can be facilitated to access the mineral resources of their country. Partnership between Tanzanians and foreign investors can and should be facilitated by the Government through its declared policy of empowerment and affirmative action (National Economic Empowerment Act no. 16 of 2004) and our oil and gas sector presents historic opportunities. The most important factor is for Tanzanians to have the capacity to effectively negotiate with foreign partners to ensure balanced partnership agreements.


6.0 THE ISSUE OF TPDC SHARES FOR TANZANIANS

There was an announcement at the Oil and Gas conference by the Honourable Minister of Energy and Minerals that Tanzanians shall participate through the purchase of TPDC shares when such shares shall be offered to the public. The major shortcoming of this arrangement is that it will have denied Tanzanians opportunities to develop the capacity that will enable them to participate in all aspects of the developments of the sector and internalize such capacity in the domestic private sector for present and future generations.

7.0 WHOM TO EMPOWER

A question raised most – both within and outside the Government – is how the Government will choose who, among Tanzanians, it shall empower. There may well be some merit in this question. Yet, this question arises more when it comes to allocation of upstream oil and gas operations to Tanzanians. Less pronounced, however, is that in addition to Public Procurement Policy (which includes some preferential arrangement to local suppliers), the Government has already stated its commitment to ensure that the "midstream and downstream" gas development shall be dominated by Tanzanian Private Sector.

In consequence, there is no reason why the criteria applicable to choose the Tanzanians for empowerment in "midstream and upstream" oil and gas operations, should also not apply to choosing them for allocation of oil and gas blocks. It may be fair to add that Tanzanians aspiring especially for oil and gas blocks should have entities based on an inclusive (rather than an individual) shareholding structure with demonstrated capacity for partnership with foreign investors. It is important to emphasize two things: countries benefit more in terms of technology and transfer of skills if foreign investment involves joint ventures with local companies and secondly, foreign investors are more attracted to a country where local investors have a reasonable stake in their economy.

8.0 CONCLUSION

What makes gas a curse is the policies not the product itself. Taking loans on future earnings is one of the traps. Tanzania should not fall into this trap of being offered huge loans that it can use its future earnings from this industry as collateral. We want the earnings of this industry to be used to develop and build Tanzania into becoming a Middle Income Country and most importantly benefit the future generation.

TPSF is known for its particular interest in seeing local participation in exploration activities and owning blocks. It is through the local content policy that this can be achieved. An example of how it can be done is through local companies forming Joint Ventures with a Tier 1 Supplier. This will automatically reduce the risk factors and give local participants a stake in this crucial resource.

There are no two countries or situations which are exactly alike; but if history and experience is of any guide, one thing is abundantly clear: countries that have succeeded in creating prosperity for their people through their mineral resources (Botswana, Norway, Malaysia to mention a few) are those that not only ensured maximum local content in the process, but also empowered their people to effectively participate in the upstream, midstream and downstream of the resource development.

Additionally, these countries observed a high level of transparency in the development and management of their mineral resources and accountability to their people of their actions pertaining to their mineral sector. The choices for Tanzania are clear! Tanzania should emulate the winners to ensure prosperity for its people.


THANK YOU FOR YOUR ATTENTION

========================

Swahili version:
MAFUTA NA GESI ASILIA... USHIRIKISHWAJI WA WAZAWA


1. UTANGULIZI
Sote tunakubaliana juu ya umuhimu wa ushiriki wa Watanzania katika sekta ya mafuta na gesi asilia nchini Tanzania. Swali muhimu la kujiuliza hapa ni hatua gani zichukuliwe ili kufanikisha ushiriki huu wa Wazawa? Kwa mtazamo wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), ni lazima kuwepo na sera ya makusudi kabisa ya kuhakikisha kunakuwepo upendeleo maalum kwa ushiriki wa Wazawa katika sekta hiyo.

Kama kuna mengi ambayo yamesemwa hivi karibuni kuhusu ushiriki wa Watanzania katika sekta ya mafuta na gesi asilia ni kwa sababu tu ya hofu ya TPSF kwamba historia inaweza kujirudia; kwa kuwa karne moja baada ya dhahabu na almasi kugunduliwa nchini Tanzania, hadi leo hii, Watanzania wengi wamekuwa wamejikuta wako katika nafasi za pembezoni – katika sekta ya madini kama vile wachimbaji wadogo, wafanyakazi wa ngazi za chini na kati au wauzaji wa bidhaa na huduma ndogondogo kwa makampuni ya madini. Kwa hali hii, hatua madhubuti zinatakiwa kuchukuliwa haraka na Serikali pamoja na Sekta Binafsi ili kuhakikisha kwamba jambo hili kamwe halitajirudia.

TPSF haina shaka kwamba Serikali inatambua umuhimu wa kuwawezesha Wazawa. Haya yapo wazi katika sera ambayo Serikali ilifafanua katika Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004 kwamba: "Maliasili, biashara, sekta ya kilimo na fursa nyingine za kiuchumi lazima zizalishe mali, zikuze biashara ya sekta ndogo na za kati, ili kuleta usawa endelevu na kuwezesha uwezeshaji halisi na chanya kiuchumi kwa Watanzania." Sheria ikaendelea kusema: "Uwezeshaji wa kiuchumi ni njia kuu kwa kuleta ukuaji wa kiuchumi na haki ya kijamii kwa watu wetu na ni muhimu kwa ajili ya kuleta amani, utulivu na uimara wa kijamii ambayo imekuwa ndio sifa ya jamii yetu."

Kwa bahati mbaya, Sheria ya Uwezeshaji haikutekelezwa kwa namna ambayo ingewapa uwezo Wazawa katika sekta ya madini. Kutokana na haya, Tanzania, lazima sasa ivalie njuga fursa hii adimu ambayo itafuta machungu ya miaka mingi yanayosababishwa na sekta ya madini katika nchi hii. Tumebahatika kupata nafasi ya pili, basi hebu tuitumie kikamilifu kwa kujenga ushiriki endelevu utakaofaidisha vizazi vya sasa na vijavyo.

2. UWEZESHAJI WA WAZAWA KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA
Uwezeshaji wa jumla wa Wazawa kushiriki katika sekta ya mafuta na gesi asilia ni muhimu kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004 na Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004. Lengo ni kuhakikisha kwamba inatumika njia shirikishi kuwawezesha Wazawa na makampuni ya Tanzania kushirikiana na makampuni ya kigeni katika ngazi zote za mnyororo wa thamani - zinazotumia upstream, midstream na downstream.

Hivyo, Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania inatetea utekelezaji wa Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004 ambayo inatoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti na za upendeleo kuwawezesha Wazawa kiuchumi badala ya kubaki kama watazamaji. TPSF inatambua kwamba Serikali imeandaa Sera ya Gesi Asilia ambayo inalenga katika kusimamia shughuli za midstream na downstream lakini sera hiyo haizingatii misingi ya Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya 2004. Huu ni udhaifu mkubwa ambao ni lazima ushughulikiwe haraka na sisi sote. Ni muhimu kutambua kwamba nchi haina sera ya kusimamia maendeleo ya upstream katika sekta ya gesi asilia, hasa, ugawaji wa vitalu, ambayo itazingatia Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004.

3. UZOEFU WA NCHI NYINGINE
Nchi nyingi, zikiwamo Msumbiji, Uganda, Angola, Libya, Algeria, Ghana na Saudi Arabia sasa zinajikita zaidi kujenga kuongeza thamani kwa kushirikisha zaidi Wazawa. Nchi zenye mafanikio zaidi katika ngazi ya ushiriki wa Wazawa kitaifa kwa kiwango cha asilimia 40% - 80% ni pamoja na Brazil, Malaysia, Uingereza na Norway.

3.1 UZOEFU WA NIGERIA
Mwaka 2010, Bunge la Nigeria lilipitisha sheria ijulikanayo kama "Sheria ya Uendelezwaji na Ushiriki katika Mafuta na Gesi asilia Nigeria" ambayo lengo kuu ni kuhakikisha Wanigeria wanashiriki kikamilifu katika sekta ya mafuta na gesi asilia. Kifungu cha 3 (1) cha Sheria hii kinatamka kwamba waendeshaji binafsi wa Nigeria watapewa kipaumbele cha kwanza katika fursa ya vitalu vya mafuta; leseni za uchimbaji mafuta; leseni za kuondoa mafuta; na, katika miradi yote ambayo itatolewa kwa zabuni au fursa mbalilmbali katika miradi ya sekta ya mafuta na gesi asilia ili mradi Mnigeria huyo atimize masharti kama itakavyoamuliwa na Waziri husika.

Kutokana na sera hiyo, mpaka sasa Nigeria imetenga asilimia 52% ya vitalu 173 kwa ajili ya Wanigeria na asilimia 48% yamepewa makampuni ya kigeni. Kufuatia sera hiyo Nigeria imezalisha mali inayomilikiwa na Wanigeria kama ambavyo inaweza kuthibitishwa na orodha iliyochapishwa hivi karibuni ya mabilionea 30 ambapo mabilionea 14 kati yao wamewekeza katika sekta ya mafuta na gesi asilia.

3.2 UZOEFU WA BRAZIL
Brazil ina sheria ambayo inalenga kukuza soko la ajira kwa wazawa, teknolojia, na ushindani wake; sheria hiyo inahitaji makampuni ya kigeni ya mafuta na gesi asilia kuingia mikataba na Wabrazil, na ina kiwango cha chini cha asilimia 55% cha ushirikishwaji katika miradi ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia.

Hatimaye, mfumo wa sera ya ushirikishwaji nchini Brazil umeweza kuifanya sera hiyo kutekelezeka na kupimika na hatimaye nguvu ya washiriki wazalendo imeongezeka kwa kasi mnamo miaka mitatu iliyopita. Hii yote ni kutokana na Serikali kujipanga kimkakati na kiuongozi.

3.3 UZOEFU WA ANGOLA
Katika jitihada zake za kuhakikisha ushiriki wa wazawa wa Angola katika sekta ya mafuta na gesi asilia, Angola imebainisha bidhaa na huduma kadhaa ambazo wauzaji wazalendo wa Angola wana umahiri nazo na bidhaa na huduma hizo zimetengwa maalum kama fursa kwa wa watu WaAngola TU.

Kwa kuzingatia kwamba makampuni ya kigeni yana uwezo zaidi ukilinganisha na makampuni ya wazawa, Angola imeweka wazi kwamba pale ambapo kampuni za wazawa zitakidhi vigezo vya muda, mahitaji ya ubora na wingi, hata kama bei yao itakuwa juu, watapewa upendeleo maalum endapo bei hizo hazitazidi asilimia 10% ya bei iliyopangwa. Asilimia 10% inaweza kuwa ni chini sana lakini angalau Angola imekuwa wazi katika sera zake.

4. USHIRIKI WA MAKAMPUNI YA KITANZANIA - MAPENDEKEZO KIMKATABA, KIMKAKATI NA KIMFUMO
• Kuhakikisha ushiriki wa Watanzania wazawa katika maendeleo ya miradi ya gesi asilia, orodha ya makundi ya mikataba mikubwa imeainishwa. Mkakati huu Ushiriki hauna budi kulenga kuongeza ushiriki wa wazawa na kuwajengea uwezo wazawa kuelekea ushindani wa kimataifa. Hivyo, imethibitishwa kwamba mikataba inayoshirikisha zaidi wazawa kama njia bora ya kujenga uwezo na ushiriki wa wananchi. Hii inatoa mtazamo wa jumla wa mfumo wa kimkakati na ambao utahakikisha kwamba Watanzania wanashiriki ipasavyo katika soko hili jipya.
• Ipo haja ya utangazwaji wa Zabuni kujenga mazingira ya kukuza ushiriki wa ndani. Shughuli zifuatazo ambazo kuna uwezekano mkubwa zikafanyika ndani ya Tanzania zifikiriwe kwa ajili ya ushiriki wa wazawa:

o kufanya utafiti wa mikataba ya huduma - msingi (Tathmini ya athari za Mazingira, Tafiti za Geotechnical / Geophysical na Data Metocean).
o Serikali inapaswa kuanisha maeneo ya kiutaalamu yanayohitajika kwenye FEED na kutathmini ni makampuni yapi ya kitanzania yaliyo na umahiri katika maeneo hayo (k.m. risers, flow lines, PLEMs, umbilicals, manifolds na foundations, subsea control system and Xmas trees). Kazi zote zinazohusu FEED zifanyike kwa kutumia nyenzo zilizopo ikiwa ni pamoja na matumizi ya vifaa vyote vinavyopatikana na ufungaji unaopatikana ndani ya nchi.
o Pale ambapo utahitajika ubunifu wa kina wa kihandisi, basi kandarasi wa kimataifa atapaswa kuingia ubia/kumshirikisha kampuni ya kitanzania ambayo ina uwezo wa kiushindani wa kufanya baadhi ya kazi zitakazoweza kufanywa na kampuni za ndani. Kampuni hizi ni lazima ziwe za hapa nchini. Ubia huu ni lazima kuonesha ushahidi wa wazi kwamba unasaidia ukuaji wa kiufundi na kuboresha uwezo wao wa kushindana kwa mikataba.
o Maeneo mengine ya kuzingatia ambayo Serikali ya Tanzania lazima iwaamrishe wakandarasi wa ujenzi wa daraja la kwanza kutoa mikataba ya ukandarasi kwa makampuni ya Tanzania kwenye kazi zifuatazo: barabara, kazi na mitambo ya umeme, uchoraji, insulation, operesheni za mashine na huduma za majengo.
o Serikali lazima iwatake wauzaji wa vifaa vya chini ya bahari kuu (subsea) kufanya uchunguzi wa mifumo yao (System Integration Tests) hapa Tanzania.

• Moja ya eneo muhimu linalotambuliwa kuwa na mchango mkubwa kwenye kuhakikisha Watanzania wanashiriki ni uwepo wa viwanda (fabrication). Serikali inapaswa kuhakikisha kwamba piles decks, nanga, maboya, jackets, racks za mabomba, madaraja, flare booms na matangi ya kuhifadhia yanatengenezwa hapa hapa nchini kwa njia yoyote ile inavyowezekana. Inasemekana kwamba huchukua angalau miaka 5 ya kutengeneza yadi ya viwanda hivi ikiwa ni pamoja na kuwa na umahiri/ujuzi unaotakiwa. Kwa sasa tayari tupo nyuma ya wakati kwa kuwa uzalishaji unatarajiwa kuanza kati ya mwaka wa 7 na mwaka wa 10 kutoka sasa.
• Kama ilivyo kwa nchi ya Norway, Tanzania lazima ihakikishe inaanzisha vituo vya Utafiti na Maendeleo hapa nchini. Hii itahakikisha kwamba uhamishaji wa teknolojia unafanyika kama inavyotakiwa.
• Ni lazima msisitizo uwekwe katika uhamisho wa maarifa na ujuzi ili katika siku zijazo haya makampuni yaweze kushindana kwa kujitegemea na hata kuwa washauri wa makampuni mengine ya Tanzania ambayo yanakosa uwezo wa kiufundi kwenye ushindani wa kimataifa.
• Tanzania inaingia katika mikataba (PSA) na waendeshaji lakini si waendeshaji ambao hufanya nyingi ya kazi hizi. Sehemu kubwa sana ya kazi hizi hufanywa na Tier 1 Suppliers. Ni kwa jinsi gani serikali itaweza kuhakikisha kwamba hawa Tier 1 Suppliers wanaweka mazingira yanayoweza kujumuisha ushiriki wa wenyeji? Hii ipo wazi kabisa katika nchi zilizo na sera ya ushirikishwaji wa wazawa kwamba waendeshaji wana wajibu wa kuhakikisha Tier 1 suppliers wanaweka mazingira hayo. Kwa mantiki hii, waendeshaji wanawajibika juu ya Tier 1 Suppliers wao.

5. SUALA LA MTAJI NA UTAALAMU
Watanzania wanatambua kikamilifu kwamba utafutaji na uchimbaji wa madini iwe dhahabu, mafuta au gesi asilia unahitaji "ujuzi adimu" na kiasi kikubwa cha mtaji. Hii peke yake inajenga utegemezi mkubwa kwa wawekezaji wa kigeni. Kwa upande mwingine, Watanzania wana rasilimali yao kubwa ya madini, gesi asilia nk ambayo wawekezaji wa kigeni hawana na kwa wakati huu Tanzania inavutia sana wawekezaji hao kwa kuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji. Hivyo, basi, Watanzania (si tu kupitia Serikali yao bali pia kwa kupitia Sekta Binafsi) wanaleta rasilimali zao (dhahabu, mafuta, gesi asilia nk) mezani na vivyo hivyo, wawekezaji wa nje wanaleta "ujuzi wao adimu" na kiasi chao kikubwa cha mtaji (ambayo ndicho walicho nacho) ili yawemo majadiliano na uwiano utakaokubalika. Huu ndio ubia wa kweli! Kwa hiyo, hii dhana ya Wazawa kuwa dhaifu na kukosa mtaji ni ya kufikiria upya na lazima iondolewe. Kwa mfano gesi asilia ni sehemu kubwa sana sana ya mtaji. Suala hapa ni jinsi gani Sekta Binafsi ya Tanzania inaweza kuwezeshwa kupitia rasilimali ya nchi yao, kwa sasa gesi asilia. Ushirikiano/Ubia kati ya Watanzania na wawekezaji wa kigeni ni lazima uwezeshwe na Serikali kupitia sera yake ya Uwezeshaji wa Kiuchumi, sheria namba 16 ya mwaka 2004; na sekta ya mafuta na gesi asilia inatoa fursa za kihistoria. Jambo la msingi zaidi ni kwa Wazawa kuwa na uwezo wa kujadiliana na wawekezaji wa kigeni kuhakikisha mikataba ya ushirikiano inakuwa na uwiano unaokubalika.

6. SUALA LA HISA ZA TPDC KWA WATANZANIA
Kulikuwa na tamko katika mkutano wa mafuta na gesi asilia toka kwa Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini kwamba Wazawa watashiriki kwa njia ya ununuzi wa hisa za TPDC wakati hisa hizo zitatangazwa kwa umma. Kasoro kubwa ya utaratibu huu ni kwamba itakuwa imewanyima fursa Wazawa kujenga uwezo ambao utawawezesha kushiriki katika masuala yote ya maendeleo ya sekta hii na jamii kuendeleza ujuzi huu katika sekta binafsi ya ndani kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.

7. NANI WA KUWEZESHWA?
Swali limekuwa likiulizwa mara nyingi - ndani na nje ya Serikali - ni vipi Serikali itachagua nani miongoni mwa Watanzania, ambaye atawezeshwa. Inawezekana kwamba suala hili lina uhalali. Hata hivyo, swali hili linajitokeza zaidi inapokuja kwenye mgao wa vitalu vya mafuta na gesi asilia kwa Wazawa. Jambo ambalo halitajwi sana, hata hivyo, ni pamoja na Sera ya Manunuzi ya Umma (ambayo ndani yake kuna mpango wa upendeleo kwa wauzaji wa ndani ), pili, Serikali tayari imetamka ahadi yake ya kuhakikisha kwamba maendeleo ya gesi asilia "midstream na downstream" itaongozwa na Sekta Binafsi ya Tanzania . Kwa hali hii, hakuna sababu kwa nini vigezo vya kuchagua Wazawa kwa uwezeshaji katika huduma na shughuli ya mafuta na gesi asilia "midstream na downstream", visitumike kuwachagua kwa ajili ya ugawaji wa vitalu vya mafuta na gesi asilia. Lakini ni muhimu kuongezea kuwa Wazawa wanaotaka kuwania vitalu vya mafuta na gesi asilia lazima wawe ni taasisi au makundi (na sio mtu binafsi) katika hisa na muundo wa kampuni hizo na pia wawe na uwezo na dhamira ya kushirikiana na wawekezaji wa kigeni. Ni muhimu kusisitiza mambo mawili: nchi zinafaidika zaidi katika suala la teknolojia na uhamisho wa ujuzi ni pale ambapo uwekezaji wa kigeni unaingia ubia na makampuni ya ndani; na, pili, wawekezaji wa kigeni huvutiwa zaidi na nchi ambapo wawekezaji wa ndani wanakuwa na vitegauchumi na uwekezaji wa kuridhisha katika uchumi wao.

8. HITIMISHO
Kinachofanya gesi asilia kuwa laana ni sera na sio bidhaa yenyewe.Kwa mfano, Taifa kuchukua mikopo juu ya mapato ya baadaye ni moja ya mitego inayokuwepo. Tanzania, isiingie katika mtego huu wa kuchukua mikopo mikubwa kwa matumaini kwamba inaweza kutumia mapato yake ya baadaye kutoka sekta hii kama dhamana. Tunataka mapato ya sekta hii yatumike kuendeleza na kujenga Tanzania katika kuwa nchi ya uchumi wa kati na muhimu zaidi ifaidishe vizazi vijavyo.

TPSF inajulikana kwa utashi wake hasa wa kutaka kuona ushiriki wa wazawa katika shughuli za utafutaji na umiliki wa vitalu. Ni kupitia sera itayohakikisha ushiriki wa wazawa ndipo hali hii inaweza kupatikana. Mfano wa jinsi gani hili linaweza kufanyika ni kwa makampuni ya ndani kuunda ubia na Supplier wa Ngazi ya kwanza yani Tier 1 Suppliers.

Hii itakuwa njia moja kubwa ya kuwapa nafasi wazalendo washiriki ubia katika rasilimali hii muhimu. Hakuna nchi mbili au hali ambazo zinafanana moja kwa moja; lakini kama historia na uzoefu utasaidia kutoa mwongozo wowote, jambo moja ni wazi sana: nchi ambazo zimefanikiwa kuleta mafanikio kwa wananchi wao kupitia rasilimali zao za madini (k.m. Botswana, Norway, Malaysia kutaja chache tu) ni zile ambazo sio tu zimehakikisha uengezaji thamani wa hali ya juu katika uendelezaji huo, lakini pia ziliwezesha watu wao kushiriki kikamilifu kwenye maendeleo ya rasilimali hizo downstream, midstream na upstream. Zaidi ya hayo, nchi hizi zimekuwa na kiwango cha juu cha uwazi katika maendeleo na usimamizi wa rasilimali zao za madini na uwajibikaji kwa watu wao katika utendaji wa masuala yanayohusu sekta hiyo ya madini.

Itakachochagua Tanzania kipo wazi! Tanzania inapaswa kuiga washindi ili kuhakikisha ustawi wa uchumi wake na maendeleo ya watu wake.
 
Mzee Mengi awe mpole tu.Mimi pia nilikuwa mbishi lakini baada ya kuambiwa hata makampuni yote ya BIMA Tanzania (Insurance Companies) kwa ujumla wao (we have at least 27 Insurance Companies in Tanzania) wataweza kuchukua risk za 1% tu kwenye Oil and Gas! 99% ya risk zitabebwa na Foreign companies!

Hii miradi ni very expensive!!
 
This man has become a super greedy on this Tz soil,kama ni mzalendo na si capitalist kwanini haanzi na wafanyakazi wake kwenye media zake? why is he paying them that extremely hand-mouth wages? by the way,yeye si amewekwa kama msimamizi wa mabepari alafu anazuga eti he owns? si anafanya on behalf ya makabaila pia?

Tafadhari Muhongo kick this arrogant,sturbon&selfish man miles away,
 
This man has become a super greedy on this Tz soil,kama ni mzalendo na si capitalist kwanini haanzi na wafanyakazi wake kwenye media zake? why is he paying them that extremely hand-mouth wages? by the way,yeye si amewekwa kama msimamizi wa mabepari alafu anazuga eti he owns? si anafanya on behalf ya makabaila pia?

Tafadhari Muhongo kick this arrogant,sturbon&selfish man miles away,
Ni mentality kama hii inayotengeneza slaves.
Better kuajiriwa na muzungu kuliko kujiajiri.

Mister you will end up a retired slave.
 
Ni mentality kama hii inayotengeneza slaves.
Better kuajiriwa na muzungu kuliko kujiajiri.

Mister you will end up a retired slave.

He deserve attention.Jamaa yangu ana kila kigezo cha kufungua light industry including 50% equity lakini mhindi a competitor katoa fungu eti jamaa asipwe loan. Crazy
 
Hii presentation nitakuja kuisoma yote baadae, nimeihia njiani baada ya kugundua kwamba kuna facts manipulation kabla sijafika mwisho! Nimeishia kwenye case studies za Nigeria na Brazil. Facts zimekuwa manipulated! Kwa mfano, ukichukua NIgeria Case, Mzee Mengi ameangalia Act 3 (1) ambayo inasema:

Act 3(1) Nigerian independent operators shall be given first consideration in the award of oil blocks, oil field licences, oil lifting licenses and in all projects for which contract is to be awarded in the Nigerian oil and gas industry subject to the fulfillment of such conditions as may be specified by the Minister.

Hata hivyo, hawakujiangaisha kutafuta tafsiri ya operators ni nani hasa. Acording to the act, operator' is defined to include any Nigerian, foreign or international oil and gas company operating in the Nigerian oil and gas industry under "any petroleum arrangement.
Nadhani hiyo definition imejitosheleza! Lakini pamoja na yote hayo, sidhani kama local investors wa hapa wamekatazwa, lakini ni kama ilivyo kwa kwa hiyo sheria mpya ya Nigeria hapo kwenye RED!

But on top of that, Bado the largest operator kwa Nigeria ni serikali under Nigeria National Petroleum Corporation(NNPC); ambayo inamiliki Hisa 55% na 45% inamilikiwa na private companies, one of them being Shell Nigeria! Hiyo NNPC ndiyo TPDC ya huko.

Ukirudi kwenye hiyo Brazil Case nako TPDC ya Brazil ndiyo ina-play major role. TPDC ya Brazil inayoitwa PETROBRAS ndo kampuni inayohodhi biashara kubwa ya mafuta kule kwao huku wakimiliki 64% of shares! Hili nalo bado linashawishi umuhimu wa ushiriki wa TPDC kama ilivyokuwa huko Brazil.

Baada ya kuona hivyo, nikalazimika kutafuta sehemu ambayo amezungumzia sources of fund for local investor! Good enough, kama ambavyo nimepata kuzungumza kwenye posts kadhaa huko nyuma, ndicho alichokisema Mzee Mengi. Kwamba, wapate vitalu kisha watafute mbia kutoka nje kisha wao wamilikishwe less than 10%!!!! Lakini cha ajabu, alipozungumzia suala la TPDC anaonekana wazi kwamba haungi mkono suala la TPDC kushiriki wakati Case Studies alizotoa kote Mashirika ya Serikali ni major players! Lakini pamoja na yote hayo, bado kuna kila dalili ya ubinafsi wa kutisha katika hili!

Lakini mwisho nikumbushe tu kwamba, Utajiri wa Mnigeria anayeongoza kwa Utajiri kule kwao ni kama mara arobaini ya utajiri wa Tajiri namba moja wa Tanzania! Utajiri wa Mnigeria huyu ni zaidi ya mara themanini ya utajiri wa Mzee Mengi! Kule Nigeria, wafanyabishara wengi wamejikita kwenye zile sub sectors na services associated in the energy industry lakini bado wanapiga pesa chafu! Hawa wa kwetu wanang'ang'ania kumiliki vitalu ili wamilikishwe parcent ndogo kutoka kwa foreigners! Kwahiyo, kwao ni heri hivi kuliko TPDC! Ubinafsi wa hali ya juu dhidi ya mtu anayejigamba kwamba ni mzalendo.
 
Huyu jamaa ni mbinafsi.anatoa mfano wa Nigeria kuwa imezakisha mabilioni 5 tayari !! Yaani katika watu 150 million raia wa Nigeria only 5?

Haoni kasoro hapo? Haoni hayo ndio yaliosababisha maoinduzi katika nchi ? Haoni NIgeria ni nchi ya 5 kwa uzalishaji mafuta duniani lakini watu wake ni masikini wa kutupwa
Suluhisho pekee ni kwa serikali kuingia ubia na kuwa na share katika sekta hii
Ubinafsi haufai .hivi sasa anazo vijisenti na haachi kuleta longolongo mara nataka kuuliwa mara unga mara hivi na kutia fitina hizi na zile
Mengi aache tuchimbe nchi ifaidike
 
Mzee Mengi awe mpole tu.Mimi pia nilikuwa mbishi lakini baada ya kuambiwa hata makampuni yote ya BIMA Tanzania (Insurance Companies) kwa ujumla wao (we have at least 27 Insurance Companies in Tanzania) wataweza kuchukua risk za 1% tu kwenye Oil and Gas! 99% ya risk zitabebwa na Foreign companies!

Hii miradi ni very expensive!!
Afadhali useme wewe mkuu wangu, tukisema wengine tunaambiwa tunaongea lugha ya Kikwete na Muhongo kumbe kabla hatujasema huwa kwanza tunafanya utafiti! Chukua matajiri watano wakubwa kuliko wote wa Tanzania kisha wauze assets zao zote ili wawekeze kwenye gas industry; wanaweza kushindwa kukamilisha even a single project! It's crazy business na ndio maana nchi nyingi kwa kuanzia ni lazima watumie government corporation. Hata huo mfano wa Brazil alioutoa Mzee Mengi, biashara kubwa ya pale imehodhiwa na kampuni iitwayo Petrobras....hii ni kama TPDC kwa hapa! Hawa Petrobras wapo Tanzania na mwaka jana walikula bonge la shoti wakati wanafanya exploration kwenye kitalu kimojawapo! Short waliyokula, kama ndo Mzee Mengi, anafunga biashara zake zote!

Huyu Bwana kwavile biashara anaifahamu vizuri, badala ya kupoteza muda huku; hivi sasa angeanza kujipanga ku-deal na sub sectors or services associated in the gas industry! Sekta ya Gas/Mafuta ni kama Real Estate! You can be building contractor, electrical, surveyor, mkodisha vifaa vya ujenzi na mambo mengine kibao! Haya ndiyo mambo ambayo tungetakiwa ku-focus na kuilazimisha serikali kutoa exclusive right kwa local investors kwa zile sub sectors! Matokeo yake tutaendelea kulia lia; utashangaa si ajabu wajanja kutoka Kenya washaanza ku-work out na issues kama hizo!
 
Kaka Nasdaz .. Sioni shida ya Mengi ipo wapi? Kwanza tukumbuke Andiko hilo si la Mengi mwenyewe ni la Tspf...

Pili Mengi / tspf ameainisha Aina mbalimbali ambazo Watanazania wanaweza kushirikisha rejea heading no 4.

Naona personal hatrage dhidi ya Mengi zisizokuwa na Msingi... Kwa Vyovyote vile Tamko la Tspsf lilikuwa kuikumbusha serikali umuhimu wa kulinda na ushirikishaji wa wazawa katika utajili wa gesi?

Kinachotakiwa kufanyika ni kuweka malengo, mikakati na mbinu zitakazohakikisha wazawa wanashirikishwa na sio kuwabeza..
 
Nasdaz....Ubinafsi wa hali ya juu dhidi ya mtu anayejigamba kwamba ni mzalendo.[/FONT][/COLOR]

Kaka Nasdaz .. Sioni shida ya Mengi ipo wapi? Kwanza tukumbuke Andiko hilo si la Mengi mwenyewe ni la Tspf...

Pili Mengi / tspf ameainisha Aina mbalimbali ambazo Watanazania wanaweza kushirikisha rejea heading no 4.

Naona personal hatrage dhidi ya Mengi zisizokuwa na Msingi... Kwa Vyovyote vile Tamko la Tspsf lilikuwa kuikumbusha serikali umuhimu wa kulinda na ushirikishaji wa wazawa katika utajili wa gesi?

Kinachotakiwa kufanyika ni kuweka malengo, mikakati na mbinu zitakazohakikisha wazawa wanashirikishwa na sio kuwabeza..[/QUOTE]

Hivi Mzawa kufaidika maana yake nini? Mengi kuwezeshwa na Serikali kumiliki kitalu, au TPDC kusimamia Mapato kwa faida ya Watanzania wote?
 
Hivi Mzawa kufaidika maana yake nini? Mengi kuwezeshwa na Serikali kumiliki kitalu, au TPDC kusimamia Mapato kwa faida ya Watanzania wote?

Pamoja na serikali kukusanya mapato ... kama sector binafsi haitashirikishwa bado kutakuwa na mapungufu... mgawanyo mzuri wa matunda ya uchumi ni ule unaoshirikisha sector binafsj kuwa washifiriki wa namna moja au nyingine na sio wao kuwa wasindikizaji...

Kuna haja gani ya Tender za kusapply vitu migodini zote zifanywe na wageni... hipo migodi mpaka chakula na maji ya kunywa yanatoka kwao....

Tspf / Mengi wameainisha namna mbalimbali za ushirikiswaji kwenye heading no 4 ... tafadhali rudia kusoma speech yake.
 
Kaka Nasdaz .. Sioni shida ya Mengi ipo wapi? Kwanza tukumbuke Andiko hilo si la Mengi mwenyewe ni la Tspf...

Pili Mengi / tspf ameainisha Aina mbalimbali ambazo Watanazania wanaweza kushirikisha rejea heading no 4.

Naona personal hatrage dhidi ya Mengi zisizokuwa na Msingi... Kwa Vyovyote vile Tamko la Tspsf lilikuwa kuikumbusha serikali umuhimu wa kulinda na ushirikishaji wa wazawa katika utajili wa gesi?

Kinachotakiwa kufanyika ni kuweka malengo, mikakati na mbinu zitakazohakikisha wazawa wanashirikishwa na sio kuwabeza..
Ndugu yangu mimi sina tatizo na na Mengi au mfanyabiashara yeyote mzawa kufanya hii biashara tatizo nililo nalo dhidi ya Mengi ni moja; ni kama hajaridhika suala la TPDC to act on behalf of majority! Kwa mfano angalia hata kipengele alichoizungumzia TPDC, kaizungumzia katika hali ya kutoipa umuhimu wowote! Kwa mtu anayejiita Mzalendo kama Mengi; pamoja na kuelezea suala la Private Sector angeeleza vilevile ni namna gani hiyo TPDC ishiriki for the interest of Tanzanians. Kwa mfano, mie nimeweka thread humu kuhusu hilo; na nikashauri kwamba TPDC ifanye reforms kisha umiliko itakaokuwa nao, iuze hisa...sehemu ya hisa iuze kwa wafanyabishara wa Tanzania na sehemu nyingine ziuzwe kwa wananchi mmoja mmoja! Hivyo ndivyo ambavyo sehemu kubwa ya Watanzania watakavyoweza kushiriki lakini sio huu mtindo anaoung'ang'ania Mengi. Kwa hiki anachotaka yeye, ni wafanyabiashara wakubwa tu ndio watakaoshiriki!

Lakini kubwa kuliko yote, hata hawa wafanyabishara (local) wakipewa hivyo vitalu; hawana uwezo wa kuviendesha wenyewe bali watakachofanya ni kuingia ubia na foreign investors!! Na kutokana na huge investment inayohitajika, hakuna atakayekuwa na jeuri ya kuweza kumiliki hata 20% ya total company shares; kiasi kikubwa kitamilikiwa na foreign partners. Lakini kwacase ya TPDC, kwamba ni government, kwahiyo uwezo wa ku-outsource finance kwao ni mkubwa! Si tu kwamba Government inaweza ikaipatia pesa bali pia wanaweza ku-issue hisa Stock exchange na kukusanya mtaji! Hawa private investors wamesha-prove failure katika hili kwani taabani iliyopo NICOL ni kutokana na management ya hawa hawa local investors! Na kama sio huruma ya serikali ya kutoa upendeleo kwa NICOL kununua hisa za NMB,hivi sasa wangekuwa ICU!

So, kama local investors wana uwezo wala hawakukatazwa kushiriki lakini suala la kutaka vitalu kisha wakatafute partners nje kisha wamiliki(shwe) asilimia chache; huko ni kutozingatia maslahi ya wengi! Halafu kumbukumbu zangu, zinanionesha kwamba Mzee Mengi zaidi ya miaka kumi iliyopita aligombana na watu wa wizarani kufuatia ununuzi wa Kilimanjaro Hotel. Akataka apewe priority. Hata hivyo, the highest bidder hakuwa yeye (ingawaje akalalamika kwamba kwanini hakuambiwa ili aongze bidding amount; sijui aliwahi kusikia wapi hii kitu!). Lakini cha kuzingatia hapa kitu kimoja. Nisaidie wewe mkuu wangu. Tangu Mzee Mengi anyimwe Kilimanjaro Hotel ni karibu miaka kumi sasa imepita! Je, katika kipindi hiki kuna Hotel yoyote ya Kitalii ambayo amejenga? NISAIDIE, mimi siifahamu na kwavile siifahamu nita-conclude kwamba hajajenga! Sasa kama kweli alikuwa na nia ya kuwekeza kwenye Hospitality Industry, ina maana anashindwa nini sasa? Yaani kutopewa Kilimanjaro Hotel iwe ndo basi tena aone sekta mzima haifai? Hivi kweli alitaka kuwekeza kwenye sekta ya mahoteli au alitaka tu lile jengo kwavile lipo kwenye prime area ambalo anafahamu angeweza kuliuza kwa pesa ndefu hapo baadae? Hivi kweli Mzee Mengi anaweza kushindwa kupata kiwanja?

The good side of Mr. Mengi ni kwamba he's very good in playing how innocent he's! Anajua kucheza na people's psychology. Na vile mungu kamjalia uongeaji na sura ya upole, ndo basi tena! And count on me, within a week lazima kutakuwa na Kipindi Maalumu ITV kuzungumzia sekta ya gesi; kipindi kitakacholenga ku-manipulate watu ili ionekane ni namna wafanyabishara kama yeye wasivyothaminiwa!!

So, kama nilivyosema hapo awali; kama Mengi na wenzako wana-access na project financing, then well and good; wapewe nafasi lakini kama wanachotaka ni vitalu kisha wanaenda tena kutafuta foreign investors wa kuingia nao ubia kisha wanamilikishwa 10%, I DON'T AGREE WITH IT AT ALL! Hivi jaribu kutafakari; kwa mfano project inahitaji USD 8billion, Mzee Mengi atakuwa na uwezo wa ku-contribute kiasi gan hapo? Kama kweli Mzee Mengi Mzalendo na sio Mbinafsi anayeota kuwa among the Greatest Africans Billionaires; basi aishauri serikali ni namna gani TPDC ishiriki ili hapo baadae hiyo TPDC ndipo iuze Hisa kwa Wafanyabishara na watanzania!
 
Huyu jamaa ni mbinafsi.anatoa mfano wa Nigeria kuwa imezakisha mabilioni 5 tayari !! Yaani katika watu 150 million raia wa Nigeria only 5?

Haoni kasoro hapo? Haoni hayo ndio yaliosababisha maoinduzi katika nchi ? Haoni NIgeria ni nchi ya 5 kwa uzalishaji mafuta duniani lakini watu wake ni masikini wa kutupwa
Suluhisho pekee ni kwa serikali kuingia ubia na kuwa na share katika sekta hii
Ubinafsi haufai .hivi sasa anazo vijisenti na haachi kuleta longolongo mara nataka kuuliwa mara unga mara hivi na kutia fitina hizi na zile
Mengi aache tuchimbe nchi ifaidike
Huyu jamaa ni mbinafsi na selfish wa kutupwa; kwa bahati mzuri ameweza kucheza vizuri na akili za Watanzania wanaodanganyika kirahisi kiasi cha kumuona ni bonge la mzalendo! Watu wanazuzuka na misaada anayopenda kutoa mbele ya kamera. Tujikumbushe machache yanayotoa viashiria vya ubinafsi wa Mzee Mengi!

  • Mwaka 1994 kuelekea World Cup aliingia kwenye bifu na mmiliki wa DTV. Chanzo ni bifu hilo ni hatua ya Mengi kutaka kuonesha michuano ya World Cup peke yake; yaani waoneshe ITV na DTV wasiwe na haki hiyo!! Lakini cha ajabu zaidi, hata wakati anagombana na mmiliki wa DTV, hiyo ITV yenyewe ilikuwa wala haipatikani sauti; ni hadi uweke sijui vidudu gani sijui! Muhindi yule (kama sikosei ni Dewj) akakomaa na wote wakaonesha. Lakini baada ya kuona ameshindwa battle, akautangazia umma kwamba eti anataka kumuua hadi kufikia hatua ya Bwana Mengi kulindwa na Polisi hata pale nyumbani kwake! GOOD enough, inakaribia miaka ishirini sasa; ITV hainoshi hata ligi ya mtaa au ya daraja ya saba, lakini DTV pamoja na udogo wao, bado wanaonesha soka ya Ulaya!


  • Wakati wa ubinafsishaji Kilimanjaro Hotel, alilia dunia mzima! Alitaka apewe priority. Abdallah Kigoda wakati anajibu tuhuma za Mengi; akasema wazi kwamba Mzee Mengi alikuwa ni one of the lowest bidder! Hata hivyo, Mengi nae akaibuka na kudai, kama bidding yake ilikuwa ni ndogo; sasa kwanini hakuambiwa ili aongeze wakati anafahamu kabisa kwamba bids zinakuwa sealed! Lakini yote tisa, kumi ni kwamba it's almost Ten Years tangu aikose Kilimanjaro Hotel! Sasa sijui ni mimi ndiye nipo less informed au vipi; kwani hadi sasa bado sijasikia kwamba Hotel ile ni ya Mengi! Hebu nisaidieni mwenye kufahamu! Sasa kama hadi leo hana cha Hotel wala nini; mtu anaweza kujiuliza alikuwa anaitaka Kilimanjaro ili aiendeleze au alikuwa anaitaka ili baadae nae aipige bei?!


  • Mimi ni Yanga Damu; niliposikia kwamba Manji anataka kugombea Uenyekiti Yanga, sikuamini! Sikutaka kuamini kama yupo tayari kushiriki moja kwa moja kwenye fitina za soka la Bongo! Basi bwana, my favorite Sports Show ni Sport Leo ya Radio One! NIka-tune Radio one kwenye kipindi cha michezo ili nisikie habari za Manji; siku ya kwanza, HOLAAA!! Siku ya pili, HOLAAA! Siku ya tatu, ya nne , ya tano and so on; HOLAAA! Lakini taarifa za wagombea wengine zilikuwa zinatangazwa! Baada kabisa, ndipo nikakumbuka bifu la Mengi na Manji! Hapo ndo nikang'amua, kwamba alah, kumbe! Kumbe STOP ORDER NEWS ROOM za IPP Media kutoandika habari za Manji! Sasa kama si ubinafsi kuwa nini?!!


  • LIkaja hili la miezi michache iliyopita, hili la DIJITALI! TCRA waliposema wangezima mitambo ya Dijitali; jamaa akadhani Mkoma anatania! Alipokuja kuzima; jamaa akatoka mbele, akalalamika weeeeeee! Hadi wanaodanganyika kirahisi wakazikubali hoja zake! Kama ambavyo hivi sasa anaitumia TSPF, wakati ule alikuwa anaituia nafasi yake kwenye media council! Akaongea lugha tamu tamu za kudaka public sympathy, kwamba wananchi wengi hawana uwezo wa kununua ving'amuzi, wanakosa haki yao ya kupata habari hivyo TCRA wasifunge kwanza! Wenye akili zetu tukajua hana lolote; ni kwavile bado ving'amuzi vyake vya DIGTEK havijafika! Anaogopa, mitambo ikishazimwa, watu hawatakuwa na option bali watalazimika kununua ving'amuzi vya Startimes! Na kweli, watu wakawa wanavigombania kama njugu! Hii ikamuuma zaidi; na zaidi! Alipoleta ving'amuzi vyake; KIMYAAAAAA! Zile kelele za kwamba wananchi maskini wanakosa haki ya kupata habari ZILIKOKWENDA! Cha ajabu zaidi, ving'amuzi vyake ndo ving'amuzi ghari zaidi kuliko vingine hata kama havina monthly charge!


  • Leo hii limekuja suala la GESI! Lakini katika hali ya ajabu kabisa, ni kama haungi mkono suala la TPDC ku-act kwa niaba ya Watanzania! Kwenye hilo andiko lake; ametumia "Tanzanians, Tanzanians. Tanzanians.......!" This's a big lie! It's deception! It's manipulation! Watanzani wadanganyike kirahisi tuone anatusema Watanzania kumbe in reality anawasemea Wafanyabishara wakubwa wa Tanzania! Mzalendo Mengi badala ya kueleza ni namna gani TPDC ifanye mambo yake kwa ajili ya maslahi ya Tanzania na Watanzania; ni kama anaikejeli na kuona njia muafaka ni wao kupewa nafasi hiyo! Ametolea mfano wa Nigeria na Brazil wakati hata huko alikotolea mfano nako mashirika ya serikali yana-participate fully in the oil/gas industry! Huu ni ubinafsi wa wazi ingawaje wapo wafuata upepo ambao mtu akisema hivi atakuambia "chuki binafsi!" Upumbavu mtupu! In addition, I bet, within the next few days kutakuwa na KIPINDI MAALUMU pale ITV kuzungumzia Wazawa na Gesi! Hatatumia Kiingereza kama ulivyo huo waraka, lazima atafute watu wa kumuhurumia Mzalendo Mzee Mengi! Atatumia kiswahili coz' wengi wasiofahamu Kiingereza ni rahisi kuwa manipulated!
 
Mzee Mengi awe mpole tu.Mimi pia nilikuwa mbishi lakini baada ya kuambiwa hata makampuni yote ya BIMA Tanzania (Insurance Companies) kwa ujumla wao (we have at least 27 Insurance Companies in Tanzania) wataweza kuchukua risk za 1% tu kwenye Oil and Gas! 99% ya risk zitabebwa na Foreign companies!

Hii miradi ni very expensive!!
na zaidi ya hapo kama yeye ana uchungu saana na sisi Tz mbona kuna maeneo ambayo fedha au faida nyingi inakwenda kama Insurance? maana ni eneo jingine lenye super profit ambayo inakwenda nje, na pili ni kwenye Bank, tatu hunting blocks, nne hotel za kitali, tano usafiri wa anga, sita usafiri wa reli na meli kwenye maziwa yetu iwe victoria au Tanganyika , then tunge mpigia chepuo kwenye madini , gas na oil.
 
Duh....hata mie mwanzo hii ishu ilinikoroga kichwa na kuona mzee wangu Mengi anachinjiwa baharini.....lakini kwa mafafanuzi ninayokutana nayo hapa akili inafunguka.

...........BIG UP GREAT THINKERS..............

Ila angalizo langu....Muhongo asiachiwe aongee kwa mtindo wa "free style"...wawe awanampa muda aonane na wataalamu wa mawasiliano ya jamii ndio aongee na vyombo vya habari.....other wise, he is a hard working man na ni mzalendo.
 
Kwanza kabisa ukisoma presentation hiyo ya Mzee mengi, hakuna mahali amepinga Ushirikishwaji wa TPDC on behalf of tanzanians!!!. Tusimzushie mzee wa watu.

Yeye anachopigania ni kuwepo ushirikishwaji wa Private sector katika Circle nzima ya mchakato wa Gas kitu ambacho ni kizuri pia. haya mawazo ya kwamba Watanzania hawana uwezo, eti kwamba makampuni ya Kitanzania hayana mtaji ni mawazo ya kipuuzi, WHAT IF 20 YEARS LATER YAKAWA NA UWEZO, YAKAWA NA MITAJI, tutakuwa tumeuza vitalu vyote kwa Wageni?!!!.

Na wala mzee Mengi hamaanishi kwamba yeye binafsi anataka na kwa hiyo atapata. sheria za Tenda ziko wazi, na humo mtu yeyote mwenye vigezo vya kisheria anaweza kupata, inaweza ikawa wewe, yeye, mjukuu wako hapo baadae, n.k

Nilichomuelewa ni kwamba sera ya gesi a sasa imejikita zaidi katika harakati za kuitafuta na kuichimba, lakini haina connection yoyote na na sera na sheria ya uwezeshaji ya mwaka 2004 (National economic empowement act).

Utakuwa ni upofu wa mawazo kudhani kwamba Mengi anapigania maslahi yake binafsi, kivipi sasa?, na solution aliyoitoa hapo ameeleza wazi kwamba Watanzania kupitia shareholding structures wanaweza kwa makundi yao uwekeza katiaka gesi, kama ni leo , kesho keshokutwa lakini policy iwepo!.

Na katiak hiyo presentation ameongea point a msingi sana, kwamba kwa utaratibu ambao serikali inataka kuuchukua, umejikita tu katika kupata mapato kutokana na gesi hiyo, lakini utaratibu huu hauna tija katika technology transfer, na kuwajengea uwezo wananchi wenyewe kupata utaalamu wa sector hiyo, kwa sababu siyo direct participants katika mchakato mzima. yaani tutaendelea kungoja mzungu achimbe auze alete hela, baaasi, lakini sisi hatutajua kuchimba!!!
 
Ukisoma comments nyingi zilizotolewa dhidi ya hotuba ya ndugu mengi, wachangiaji wanataka kutuaminisha kwamba mengi anaongea kwa niaba yake binafsi na si kwa maslahi mapanna ya watanzania wote. Mimi naomba wanaopinga hoja ya mengi wajiulize maswali yafuatayo:

1. Hivi wewe nyumbani kwako unaweza kuwapambanisha watoto wako wadogo na wageni/majirani kwenye sinia moja ya chakula na kuwaambia wanao kwamba hapa kwangu hakuna sera ya upendeleo na kwamba watoto wa ndani na wagesni wote mna ulinganifu na asiyeshiba atajiju?

2. Hivi hawa wageni ambao wengi wao ni matapeli kama john nolan wana mapenzi mema kweli na watanchi wa tanzania? Hivi sisi tunafaidika vipi na hii capital fclight? Hivi tumelogwa? Hivi si ni bora hata vitalu vyote tumpe mtanzania mmoja na kuwe na sera ya kumshurutiszha awekeze humu nchini mabilioni atakayopata ili hizo fedha zibaki humu nchini ili kuboresha mzunguko wa fedha humu ndani kuliko kuziona fedha na raslimali zetu zikihamishwa kwenda nje na baadae kurudi kama mikopo ya benki ya dunia yenye masharti magumu? Hivi tumewachagua viongozi wetu ili wawatetee wazungu wahamishe raszlimali zetu? Hivi viongozi wetu wanamwakilisha nani katika maamuzi yao? Hivi maraisi wa marekani na uchina wanapotetea maslahi ya nchi zao, na viongozi wa afrika nao wanatetea maszlahi ya wawekezaji (au wezi) wa marekani na uchina, nani hasa atakayetetea maszlahi ya mtanzania? Hivi kazi ya vichwa vyetu watanzania havina kazi nyingine ya muhimu zaidi ya kufuga nywele?hivi tunangojea hao waliowekewa mabilioni uswiss ndxio watetee maslahi yetu kweli? Kwa nini tunakimbizana na kuuza vitalu kabla hata sera ya gesi haijawa finalized? Nk., nk.,... Naomba niishie hapa maana machozi yananitoka, mungu atusaidie ili tujitambue!
 
Mzee Mengi awe mpole tu.Mimi pia nilikuwa mbishi lakini baada ya kuambiwa hata makampuni yote ya BIMA Tanzania (Insurance Companies) kwa ujumla wao (we have at least 27 Insurance Companies in Tanzania) wataweza kuchukua risk za 1% tu kwenye Oil and Gas! 99% ya risk zitabebwa na Foreign companies!

Hii miradi ni very expensive!!

hoja inataiwa ijibiwe kwa hoja sio some deus ex machina!!!
 
Back
Top Bottom