Dr. Mwakyembe ni 'mtendaji mwenye weledi'

MALIGANYA MALIMBE

JF-Expert Member
Jun 14, 2015
280
206
Nianze kwa kusema kuwa Dr Harrison George Mwakyembe ni mtu ambaye kwa kiwango chake cha elimu,umri wake na wadhifa wake hastahili hata kidogo kutenda mambo kwa namna anavyotenda katika nchi hii ya tanzania.Kama dr mwakyembe angelikuwa ni raia wa nchi za ulaya na akatenda kama anavyotenda tanzania,Basi angelikwisha fungwa jela au kupigwa marufuku kushughulika na baadhi mambo.Naomba tujikumbushe baadhi ya mambo ambayo dr mwakyembe hakulitendea taifa letu pamoja na wananchi wake kwa kile anachokijua yeye.

1. Dr. mwakyembe alikuwa ni mwenyekiti wa bodi ya benki ya NBC wakati benki hiyo inauzwa na serikali ya mkapa mwaka 1999.Ni huyu huyu mwakyembe aliyekataa katakata uuzwaji wa benki hii,Kiasi kwmba aliitisha maandamano ya wanafunzi wa chuo kikuu dsm ili kupinga uuzwaji wa benki hii ya NBC.Pamoja na maandamano hayo alijiuzulu wadhifa wake wa uwenyekiti wa bodi ya benki hii.Lakini ,tarehe 22/02/2002 alipokuwa kwenye mdahalo kuhusiana na uwekezaji kwenye kipindi kinachorushwa na channel 10,Dr mwakyembe aliunga mkono uuzwaji wa benki hii.Kumbukumbu zinaonyesha kuwa mwendesha kipindi hicho jenerali ulimwengualimuuliza dr mwakyembe kuwa...nukuu"Dr.ilikuwaje ukapinga kubinafsishwa benki hii hapo mwanzo lkn sasa umekubali kuwa uuzwaji wake ulikuwa sahihi?"...dr mwakyembe alijifanya hakusikia swali ,lkn liliporudiwa dr. alijibu "mwanzoni sikuelewa faida za ubinafsishaji wa benki hiyo lkn sasa nimeelewa na ubinafsishaji huo utakuwa na faida".Leo hii tunapoongea,Ni kweli ubinafsishaji wa benki hiyo ina faida kwetu kama taifa?...HUYO NDIYE DR MWAKYEMBE.

2. Dr mwakyembe ni msomi wa kiwango cha juu katika taaluma yake ya sheria.Machapisho yake yanasomwa dunia nzima na hata kufanyiwa rejea pale inapobidi.Moja ya vitabu alivyoviandika wakati anachukua phd yake ujerumani ilihusu muungano wa tanzania ,kuundwa kwake,uhalali wake kisheria na ridhia ya muungano huo kwa wananchi wa pande mbili zilizoungana.Dr mwakyembe katika kitabu hicho alihitimisha kwa kusema kuwa "muungano wa serikali tatu ndiyo muungano unaotakiwa na kuwafaa wananchi wa tanzania na siyo muungano wa serikali mbili.Lakini huyuhuyu mwakyembe ndiye aliyekana maandishi yake hayo wakati wa bunge la katiba..kwa lugha za kejeli kwa jussa na tundu lisi....Hakujibu hoja zilizotolewa na vijana hao katika bunge la katiba.HUYO NDIYE MWAKYEMBE.

3.Dr mwakyembe ni mwanasheria kitaaluma na vilevile ni mwandishi wa habari.Katika ethics za wanasheria na waandishi wa habari,moja wa vitu wanavyotakiwa kufanya ni kuweka wazi facts na evidance wakati wanafanya kazi zao au wanapotekeleza majukumu yao.Hii ni kinyume kabisa kwa dr mwakyembe....kwa nini?.Dr mwakyembe ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge iliyochunguza sakata la richmond.Ni yeye mwenyewe kwa kinywa kuwa kuna mambo ambayo aliyaficha ili serikali yote isianguke.MWAKYEMBE anajua kuwa hilo ni kosa kwa mujibu wa taaluma yake na sheria.Vilevile bunge halikumtuma kuficha baadhi ya mambo kama anvyodai alizificha.MWAKYEMBE Kama mwanasheria aliyebobea,Anafahamu fika kuwa serikali yetu inaundwa na rais na siyo waziri mkuu.Rais ndiye mwenye serikali...na ndiyo maana rais wetu hutamka ...serikali yangu....spika..bunge langu..jaji mahakama yangu...waziri...wizara yangu nk.Kwa maneno ya mwakyembe kuwa alificha baadhi ya mambo ili serikali yote isianguke,Alikuwa na maana ya rais kikwete ambaye ndiye mwenye serikali na siyo waziri mkuu.Kwa nini mwakyembe asienende katika taaluma yake?..HUYO NDIYE MWAKYEMBE.

4.Wakati mwakyembe akiwa ni waziri wa uchukuzi aliingia kwa mbwembwe nyingi sana wizarani hapo na kutangaza kiama kwa mafisadi na wazembe.Aidha ktk kipindi hicho,dr mwakyembe alikuwa akionekana angalau kila wiki kwenye viombo vya habari akielezea alivyo mchapa kazi hodari na mpambanaji wa ufisadi.Lakini ni yeye aliyefanya kinyume na matarajio ya watanzania wengi.Aliagiza mabehewa feki,aliipa zabuni kampuni ya VIP ENG Ya james rwegamalila ya kujenga reli kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma,Aliipa CCM eneo la bandari ili wajenge yard ya kuhifadhi makontena,Ni yeye aliyeondoa baadhi ya tozo zilizokuwa zikitozwa kwa kampuni ya TICS Ya KARAMAGI...yule wa richmond.HUYU NDIYE MWAKYEMBE.

Mara nyingi Dr Mwakyembe anapokuwa amebanwa katika mambo machafu na ya kifisadi anayoyatenda,Amekuwa akitumia lugha za dharau na kejeli ili akwepe kujibu tuhuma zinazomkabili.Ninamuomba dr mwakyembe anijibu neno moja tu...SIHUSIKI NA MAMBO HAYO...Baada ya hapo nitaweka na ushahidi usio na shaka.Lakini nitaweka wazi jinsi alivyopata fedha za miradi yake ambayo anamiliki kupitia ndugu zake huku akidhani watanzania ni mbumbumbu.
 
Khaa!! Sijui watajificha wapi?? Kama huku yupo JPM na kule kwenye uPM yupo Mwakyembe! Mbona itakuwa balaa! Mafisadi na wazembe itakuwa mperampera hadi watakimbia ofisi
 
Mjinga kuwa mjinga ni jambo la kawaida na linahitaji wakati na kuelimishwa.
Lakini msomi kuwa mjinga ni hasara kwani ana nafasi ya kuongeza idadi ya wajinga kuwa wengi kwani atawapotosha wengi.
Mwakyembe ni msomi mjinga hivyo ni hasara kubwa kwa taifa. Anapaswa aepukwe.
 
tumekubaliana naye,tuna ombi kwa ndugu yetu mwakyembe,atusaidie tu kujua je,LOWASA alilipwa mlungulu kiasi gani kwenye hii issue ya RICHMOND???
asante kwa hilo
 
Katika serikali nzima hata mkulu mwenyewe hamuamini huyo, soon tutakuja kusikia sababu zilizomtoa katika wizara ya uchukuzi, anajifanya anaboresha kumbe ndie muhujumu mkubwa wa reli
 
Khaa!! Sijui watajificha wapi?? Kama huku yupo JPM na kule kwenye uPM yupo Mwakyembe! Mbona itakuwa balaa! Mafisadi na wazembe itakuwa mperampera hadi watakimbia ofisi

Uliza wafanyakazi wa wizara aliyoondolewa utaupata ukweli
 
Yote haya uliyo yaeleza sijui nbc na mbwembwe nyngne haziondoi ukweli kwamba lowasa alihusika kupiga dili la richmond ,kwa hiyo mwache mwakyembe aendelee kutueleza ukweli.namtulie kimya mnyolewe bila maji
 
Mwakyembe ni mnafiki suprimo,alianza kudai serikali inataka kumuua kwa kumtumia afande Kimaro -saba sita-na kundi la mapolisi,akadai ugonjwa wake ni sumu kalishwa,kali akadai kuna mchawi Songea kapewa kandarasi ya kumroa.Leo ni mtetezi wa serikali hiyo hiyo,baada kukwaa mradi wa umeme Singida na ndio unafiki aka upumbavu
 
Shukran mleta mada kwa kuleta picha nyingine kuhusu ufisadi na unafiki unaoendelea nchini. Twende mbele zaidi. Sidhani kama kuna atakayebisha kwamba Lowasa hakuhusika kabisa na ufisadi wa Richmond. Lakini kudai kwamba ni yeye pekee ndiye mhusika au mhusika mkuu wa ufisadi ule ni kutaka kutufanya hatuna shule kichwani.

Tatizo ni watu kama akina Magufuli na Mwakyembe ambao wanatumika kufunika uozo wa mfumo wa ufisadi kwa kutaka kutuzuga wananchi kwamba chama ni kisafi ila ni tatizo la mtu fulani pekee: Lowasa. Ni kama vile wameapizwa na wenye mfumo huo kujitoa mhanga kuendesha ghilba ili Watanzania tuendelee kuubeba na kuuvumilia mfumo huo - tusithubutu kabisa hata kufikiria kuung'oa. Leo hii Mwakyembe na Magufuli wanaweza kweli kuthubutu kung'oa mizizi ya kifisadi iliyosimikwa kwenye biashara kubwa za vigogo wa CCM wakiwemo Mkapa, JK, Chenge, n.k.

Nafikiri hicho chama kinaua kabisa integrity ya wasomi. Mwakyembe wamempiga nyuklia (polonium) lakini bado yuko nao tu anawabebea mafurushi yao. Mama Tibaijuka tuliyemheshimu sana kwa usomi na uongozi wa kimataifa naye wamemgeuza kama muimba taarabu za mipasho! Haoni wala hasikii tena mantiki mbele ya wenye chama.
 
Kwan mwakyembe yumo humu jf?
Ingekuwa vzr tumfuate kwake tukamuulize
 
Umenena vema.
 
hahahahaha ila mama tibaijuka ndoo kiboko kwenye mipasho...vijihela vya mboga......huuuuiiiiiii:wink:
 
Lowasa akisikia jina la Myakyembe anaweza kujificha hata chooni anamuongopa balaa anajua kuwa siri yake yote anayo.
 
Watanzania tumekuwa sana washabiki kwa mahaba tu ya kumpenda mtu tunafahamu kuwa ht waswahili walisema ukipenda ht "chongo utaita kengeza"endeleeni kuwa hivyo kwsbb wengi wenu fikra zenu zinaishia mwisho wa pua zenu,naamini ipo sk mtu ukawa unamuona ng'ombe lkn ukasema c ng'ombe bali ni punda,yoooote haya ni MAHABA ila poleni sana na akili zenu za nyumbu
 
Khaa!! Sijui watajificha wapi?? Kama huku yupo JPM na kule kwenye uPM yupo Mwakyembe! Mbona itakuwa balaa! Mafisadi na wazembe itakuwa mperampera hadi watakimbia ofisi/QUOTE]

jasiri kutoka mbeya aliyewafundisha monduli siasa, tumefika hapa kutokana na makandokando ya mamvii hakika magufuli ndiye chaguop letu
 
Mjinga kuwa mjinga ni jambo la kawaida na linahitaji wakati na kuelimishwa.
Lakini msomi kuwa mjinga ni hasara kwani ana nafasi ya kuongeza idadi ya wajinga kuwa wengi kwani atawapotosha wengi.
Mwakyembe ni msomi mjinga hivyo ni hasara kubwa kwa taifa. Anapaswa aepukwe.

Nadhani wewe unastahili neno alilotoa mzee Mkapa majuzi: Mpumbavu!
 
Back
Top Bottom