Nemesis
JF-Expert Member
- Feb 13, 2008
- 5,462
- 4,364
Mkuu Nziku,
Unapotosha kabisa dhana ya mbunge kuleta maendeleo au kusukuma maendeleo kwenye jimbo lake.
Haina maana yeye ndiye anaamua nini cha kufanya au yeye ndio anatoa resources za kufanya hayo maendeleo yatokee.
Mbunge ndio kiongozi aliyechaguliwa na wananchi ili awasaidie kutatua matatizo yao. Sasa kama kuna shule mbovu, ni wajibu wa mbunge kuwakutanisha wadau wote na kuangalia namna ya kuongeza ubora.
Kama kuna mabomba yamejengwa na wafadhili, wameondoka na maji nayo yamehama nao, ni wajibu wa mbunge kuangalia kutafuta solution kwa kushirikiana na viongozi wengine wa wilaya pamoja wananchi. Kwanini wafadhili wakiondoka na maji yakauke?
Kama kilimo cha kawaha au mpunga kinaanguka, ni wajibu wa mbunge kupata majibu ya kitaalamu kupitia vyanzo mbalimbali na ikiwezekana ku mobilize resources iliyopo ili kusaidia kutatua tatizo.
Kwa mimi ningetaka mbunge wangu awe a troubleshooter na sio mropokaji tu. Awe na uwezo wa kuwakutanisha watu pamoja kwenye mambo ya maendeleo na sio mtu wa kuwagawa watu.
Aweze kuibana serikali kuu, aweze kuibana halmashauri ya wilaya kwa niaba ya wananchi wake ili watekeleze ahadi walizoahidi, ili miradi wanayoendesha iwe value for money nk.
Nimeshangaa kuona idadi kubwa ya wana JF wanafikiri kazi ya mbunge wa Tanzania ni kwenda kupiga kelele kule Dodoma. Eti kukusanya matatizo ya wananchi na kwenda kuyawakilisha bungeni, nonsense, wala hata huhitaji kusubiri bunge kuwakilisha matatizo yalipo. Kama umeona tatizo, ni hapo hapo kuanza kutafuta solution, kama haiwezekani wilayani, basi huko mkoani, huko wizarani, huko bungeni nk.
Wasanii wetu wengi hawafanyi kitu, anapiga kelele siku moja bungeni, kisha anarudi kwa wananchi na kuwaambia mmenisikia bungeni?
sijamaanisha Mbunge asifanye hayo unayosema, nasema kipaumbele cha kuwajibishwa kiwe kwa watendaji siyo Mbunge. Serikali ndiyo inayowajibika moja kwa moja kwa kuwa ndiyo iliyopewa resources na ndiyo yenye wataalam/watendaji.
Tatizo la huu mfumo mnaoutaka wa kumweka mbele mwanasiasa eti kwa kuwa amechaguliwa ndiyo utakaoendelea kutuletea matatizo. Nasema tunajenga Taifa la wanasiasa ni kwasababu tumeamua kustawisha hii dhana mbovu.
Mbunge atapenda short term plans, ili apate kitu cha kuwaonyesha au kuombea kura. Mbunge anapobeba maendeleo ya Halmashauri ina maana mahali popote atakuwa ndiye mwenyekauli kwani ndiye atakayeulizwa na wananchi au ndiye atakaye wajibika.
Ndiyo maana maamuzi mengi siku hizi yanashinikizwa kisiasa, yaani makatibu wakuu wa Wizara, Wakurugenzi wa Wilaya au Halmashauri wamekosa maamuzi na kuwasikiliza wanasiasa au wanatekeleza kwa kufuata interest za wanasiasa mojawapo Wabunge.
Ndiyo maana watalaam wanaacha kazi zao na kujiunga kwenye siasa. Tena mtendaji fulani akionekana anafanikiwa kazini anatafutiwa zengwe ili kumharibia kwa hofu tu kwamba atakuja kugombea ubunge.Tunajimaliza wenyewe, acha tuwape hiyo nafasi, miaka ijayo ndo tutajua.