Dr. Bana: Takwimu za tume ya Warioba sio za kisayansi

siku huyu anaeitwa bana akisema chochote kinyume na CCM ntatembea kwa mguu hapa hadi zanzbar
 
Hata hivyo amechelewa sana kuunga mkono hotuba ya Jk kiasi nilianza kufikiri labda ametemwa na ccm. Na sikutegemea kitu tofauti na hicho alichokiongea.!

Alitaka wachaguliwe watu maalumu wa kuzungumzia muungano? That was a random selection ya watanzania ambao kati yao kuna walozungumzia muungano. Hivi huyu anafundisha research gani wanachuo hapo udsm?? Naona ccm wanahaha kutaka upuuzi wao uwaingie watu vichwani kwa lazima lakini kila wanayemchagua anachefua zaidi.
 
umemwona bana? muulize redet na takwimu zake za kisayansi REDET inarudi lini?
pia mbona matokeo ya redet yalikuwa hayaakisi ushindi wa ccm?


Inawezekana hawajapata mfadhili wa kuwalipa ili waingie kwenye makabrasha yao watoke na utafiti wenye utata.
 
Dr Bana asipojipendekeza kwa chama tawala anahofia atakosa kuongezewa muda atakapostaafu hafu atanyimwa mlo maana pesa za tafiti zake inawezekana zinatokea huko.
Usiamini wasomi haswa hao dr na prof wa vyuo vikuu kwani wengi wao ni waoga kutoa mawazo yao bainafsi zaidi wanataka kutoa mawazo yasiyokinzana na watawala.


Cc kapalamsenga njoo huku huyu kijana ni saizi yako mweleweshe watoa povu mimi siwezani nao heshima kamanda
 
Takwimu sio za kisayansi!??
Huyu Benson Bana alitaka watumie Bunsen burner?

Samahani sana, lakini nikwambie kuwa wasomi wote wanaounga mkono serikali mbili au tatu wana uhakika kuwa takwimu za Tume ya Warioba si za kitaalamu na hazitakiwi kutumiwa kuhitimisha sehemu yoyote ya mjadala. Yeyote aliyeingia darasa la takwimu au research methododology anajua hivyo. Sababu ni mbili za wazi. Moja imesemwa sana, kuwa takwimu zao wenyewe haziungi mkono majumuisho yao. Nyingine ambayo ndiyo muhimu zaidi ni kuwa maoni hayakusanywi kwa watu kujileta, kwa kuwa watajileta waliohamasika tu, na kutakuwa na uwezekano wa maoni kuwa ya makundi ya mtazamo mmoja. Kwa vyovyote vile maoni hayo yatakuwa na unacceptable margins of error. Serikali tatu zinaweza kutetewa bila takwimu za mashaka hizi.
 
Dr Bana naye ni janga la taifa kama TBC na Mchembe.

Unfortunately hao ndio wasomi wetu Tanzania; njaa ina nguvu sana. Utashangaa serikali ya CCM inampa u-VC wa chuo chochote cha serikali: UDSM, MU au UDOM. Mukandala alianza hivyo hivyo na sote tunajua alichopata!
 
Samahani sana, lakini nikwambie kuwa wasomi wote wanaounga mkono serikali mbili au tatu wana uhakika kuwa takwimu za Tume ya Warioba si za kitaalamu na hazitakiwi kutumiwa kuhitimisha sehemu yoyote ya mjadala. Yeyote aliyeingia darasa la takwimu au research methododology anajua hivyo. Sababu ni mbili za wazi. Moja imesemwa sana, kuwa takwimu zao wenyewe haziungi mkono majumuisho yao. Nyingine ambayo ndiyo muhimu zaidi ni kuwa maoni hayakusanywi kwa watu kujileta, kwa kuwa watajileta waliohamasika tu, na kutakuwa na uwezekano wa maoni kuwa ya makundi ya mtazamo mmoja. Kwa vyovyote vile maoni hayo yatakuwa na unacceptable margins of error. Serikali tatu zinaweza kutetewa bila takwimu za mashaka hizi.

umenena mkuu,na ukifatilia mchango wangu uliopita katika uzi huu utagundua tupo pamoja,wacha wasiojua nini maana ya takwimu waendelee kutokwa na povu,ila sisi tunaoelewa nadhani tunaongea lugha moja,the data are not supposed to be used to draw conclusion(generalization),since they are not scientific data' period!!!!
 
Dr Bana akiwa anahojiwa kwenye kipindi cha Hot Mix EATV amesema twakimu za tume ya jaji warioba sio za kisayansi na zisitumike kuafanya majumhisho ni kama za kipima joto cha ITV pia ameendelea kusema kuwa hata waliokuwa wakiziandika watakuwa walikosea kwa sababu hawakuchukuwa sampuli.

Ingawaje siyo vizuri kuwajibu madaktari, lakini mara nyingine huwa wanazidhalilisha elimu zao. Kwanza sayansi ni nini mpaka aseme kuwa takwimu za Warioba siyo za kisayansi? Kitu cha pili nadhani wanaomchallenge Warioba kwa kutumia kanuni za utafiti wanatumia mtazamo mmoja tu (yaani quantitative approach). Sasa quantitative approach inafaa kama unataka kufikia hitimisho kwa watu wote (inference about population yaani statistical generalization). Je Warioba alikuwa na kazi hiyo? Jibu ni hapana. Warioba alikuwa na kazi ya kutoa rasimu ya katiba. Kwa hiyo approach ya Warioba ilikuwa ni qualitative approach.

Sasa kwa wanaojua utafiti, hii mbinu hutumika kama unataka kutengeneza nadharia yaani theoretical generalization. Nadharia inaweza kujaribiwa au isijaribiwe kwa kutumia quantitative approach. Na hii inaweza kutumika kama hatua ya mwanzo ya utafiti. Na hapa siyo lazima kutumia kanunin za kuchukua sampuli kama za kwenye quantitative approach. Unaweza kuchagua watu wanaolijua jambo wakaongelea ukatoa nadharia yako. Kwa hiyo kwa Warioba hicho ndicho wamekifanya. Walitoa nafasi ya watu kutoa maoni. Baada ya hayo maoni wakatoa rasimu ya katiba (hii hapa ni kama nadharia kwenye utafiti).

Hii rasimu (ambayo kwangu naweza kusema ni kama nadharia) inajadiliwa na bunge maalum la katiba (kwa kutumia qualitatitve approach hii stage unaweza kuiita kama confirmatory stage). Hii inajaribu kulinganisha kama kilichoandikwa kinareflect kweli maoni ya watu. Hawa wataiweka vizuri ili kuwa tayari kwa testing. Sasa hatua ya mwisho itatumia quantitative approach ambapo rasimu ya katiba itapigiwa kura ya maoni kuona kama inakubaliwa au vipi. Na hapo kanuni za kuchukua sampli lazima zizingatiwe ikiwemo umri wa mpiga kura, kujiorodhesha kwenye daftari la wapiga kura nk. Kwa hiyo unapokuta Daktari mzima anasema takwimu za Jaji Warioba siyo za kisayansi unajiuliza sayansi ipi hiyo anayoongelea. Hivi kweli huyu Daktari huwa anasoma majuzuu ya utafiti ambayo yana makala ambazo zinatumia qualitatite approach, na kama huwa anasoma wale jamaa walimwambia kuwa majuzuu yao siyo ya kisayansi?
 
If this academic did not talk about the inappropriateness and awkwardness of Kikwete's speech, especially that "over my dead body" swagger, then he is not doing the matter justice and quite possibly biased.
 
Haina haja kuendelea kubishana na Warioba....Muda wake umekwisha tume imevunjwa sasa ni wakati wetu wanaCCM tunaowakilisha sauti kubwa za wananchi tufanye yetu...

Kuendelea kubishana na Warioba wakati tuna uwezo wa kufuta na kuongeza lolote kwenye katiba ni kupoteza mda na kufukuza upepo....

Zama zake zimepita sasa ni wakati wetu...
 
Hahaaaa, umedata mkuu.
Mkuu huyu Dr Benson Bana mara nyingi huwa anatoa mitazamo ya kuunga mkono matakwa au maslahi ya chama cha mapinduzi hata kama yako kinyume na ukweli halisi.
Na huyu tunaweza kumwita kama ambavyo Warioba juzi kamuita Issa Shivji, INTELLECTUALLY DISHONEST.
 
Mkuu huyu Dr Benson Bana mara nyingi huwa anatoa mitazamo ya kuunga mkono matakwa au maslahi ya chama cha mapinduzi hata kama yako kinyume na ukweli halisi.
Na huyu tunaweza kumwita kama ambavyo Warioba juzi kamuita Issa Shivji, INTELLECTUALLY DISHONEST.



Mimi sina matatizo nakujaribu kum criticize mzee wangu Warioba. I can debate the finer details, but that I cannot.

I am sure hata Mzee Warioba, being the consummate "lawyer's lawyer", elder statesman and international jurist that he is, does understand the value of dissenting opinions.

Lakini huyu Dr. Bana, kama hajaongelea Kikwete ku shove down our throats the merits of the two governments system, after blowing a lot of time and other resouces in commissioning a team of stalwarts and scholars, then ananipa sababu ya kukubali kwamba ni kibaraka anatumiwa na watawala tu.

Kwa sababu msomi wa ukweli anatakiwa kuwa balanced, akiona hata upande anaoutetea umezidisha ujuha anaubwaga na kuusema.

Hata Noam Chomsky aliyekuwa anambeba Hugo Chavez miaka kibao kama "The Bolivarian Revolutionary" alikuja kumbwaga baadaye, kwa sababu Chavez alizidisha kuendesha nchi kwa ujanja ujanja.

Kama hajakemea Kikwete's bullying, basi anadhalilisha wasomi wetu.
 
alete za kwake ambazo ni za kisayansi sio kukosoa tu ili kufurahisha mabwana zao.hao ndio ma dr wa tz

Watanzania waliotoa maoni juu ya muungano kwenye tume ya warioba ndio sampuli ya watanzania. Na hio ndio ilikuwa njia pekee ya warioba kujua mfumo upi unapendwa na watanzania wengi. Kama unaona sampuli sio ya kisayansi ngoja tuone wanzania watasema nini kwenye kura ya maoni baada ya kuipitisha rasimu badala ya kupinga kuwa sio mawazo ya wananchi bila kuonyensha takwimu zenu mkitumia sampuli za kisayansi. Vikao vya CCM sio sampuli ya kisayansi ya watanzania na mawazo yao sio mawazo ya watanzania
 
Back
Top Bottom