Niko Handeni, Tanga na ADC wana mkutano wao hapa. Doyo anasema baada ya kuondoka cuf hakujiunga na cdm au nccr kwasababu vyama vyote hivyo vina tabia zinazofanana na cuf. Anasema cuf iliwatimua wao, nccr ikawatimua akina Kafulila na Cdm ikawatimua madiwani 5 Arusha. Anasema kwa tabia yake yakutovumilia ubabe ndani ya vyama basi hata huko watamtimua. Anasema ametimuliwa cuf baada ya kuhoji matumizi ya chama wakati wa kampeni huko igunga. Anasema igunga alikabidhiwa kata mbili kuongoza kampeni na kutumia jumla ya sh l milion 6 tu. Kwa kata zote za igunga walitumia tshs milion 80, lkn taarifa za vikaoni zikaonyesha matumizi ya tshs mil mia tatu! Alipohoji ikawa sababu ya kutimuliwa