Dowans what we have so Far..... (Evidences Kuhusu Dowans)

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,194
1,355
Baada ya kuona evidence za hii issue inayotugusa wote zimetapakaa jamvini kote naona bora nianzishe hii topic ili evidence zote tuziweke humu, kuanzia zile za kina Mwanakijiji, Rutaba..... na wengine wengi please..... Together we Shall overcome....
 
mpaka sasa tunajuwa kuwa hawa ndio baadhi ya wakurugenzi...
Andrew James Tice; cv yake Andrew James Tice - LinkedIn lakini hakuna connection na Dowans

Guy Arthur Picard ambaye connection yake ameji-register alibaba (platform ya kuuza vitu) kama Dowans Tanzania Dowans Tanzania Ltd - Energy, na contacts zake mpaka simu ipo hapo kampuni anasema ipo morogoro rd Dar

Hon Sung Woo kuna kampuni ya Portek Middle East FZCO...PORTEK MIDDLE EAST FZCO Oilfield & Natural Gas Equipment & Spare Parts Trading 17815 DUBAI United Arab Emirates 0097104 8860071 0097104 8860073 nelson.woo@portek.com

Je connection ya Dowans ni Kampuni ya Portek International au ni hii kampuni ya kwenye briefcase Portek Middle East FZCO....

Tafadhali naomba na kina Mwanakijiji na wengine wamwage evidences zao so far tuone tupo wapi..... pia hata kama Sitta anapita pita huku hata kwa ID ambayo sio yake na yeye atumwagie anachokijua
 
Nimejaribu kuulizia kwa marafiki wanipatie namba ya simu ya huyo A J Tice, lakini sijafanikiwa ila bado juhudi zinaendelea. Watanzania tumetapakaa katika kona nyingi za dunia tuna nyenzo za kila aina katika kuhakikisha tunalinda maslahi ya nchi yetu popote pale tulipo. Hili la Dowans lazima tulifuatile mpaka ukweli ujulikane. Nimeshangaa sana huyo Tice hakuweka ukurugenzi wake wa Dowans katika CV yake huu ni ushahidi mwingine wa kuonyesha kwamba kampuni hii ni ya kifisadi. Hii kampuni haijawahi kufanya mradi wowote ule duniani, Tanzania mradi wake wa kwanza ndiyo huo wa kifisadi ambao wanakaribia kuvuna au wameshavuna $69m. Mpaka kieleweleke!
 
Wengine tunatumia simu, mkiweka links siyo simu zote zinaweza kufungua kila link au attachments. Please paste hapa hara kama ni ndefu

in addition, katika hii kadhia, napenda mapema kabisa kutanguliza shukrani zangu za dhati kabisa kwa VoR na MM kwa kazi kubwa ambayo wameshafanya so far. I am so enlighted but frustrated over why could our own leaders betray us in this proportion.

I am ready for anything
 
Ukisoma nini kilichofichuliwa ktk thread ya MMK juu ya nini kilifichwa kuhusu Dowans, mwenye akiri timamu hata agepewa kiasi gani cha pesa asingekubali kuihalalisha Dowans. Ni uvundo unaonuka ambao ni kero kwa kila mwenye pua.
 
Swali ni kwamba je kuna connection kati ya Portek International na Portek Middle East ?
Nadhani connection hakuna ila hawa watu kuficha tracks zao nadhani watasema connection na Portek sio Portek International bali Portek Middle East .PORTEK MIDDLE EAST FZCO Oilfield & Natural Gas Equipment & Spare Parts Trading 17815 DUBAI United Arab Emirates 0097104 8860071 0097104 8860073 nelson.woo@portek.com

Kwa wanao kaa Dar hivi Morogoro Road Kuna Hii Kampuni ya Dowans Tanzania.... Sababu Contacts za huyu Guy Arthur Picard ndio anasema yupo hapo.... simu zake ni 255-756-606042
 
Jenerali Al Adawi aikana Dowans katika mahojiano na Mwanakijiji

Hata hivyo, bado utata umeighubika Dowans. Anayeitwa mmiliki, Jenerali Al Adawi, awali alikanusha kuwa mmiliki.
Alipobanwa akamtaka Mwanakijiji kusoma katika tovuti ya makampuni yake yenye anwani: http://www.stcgroups.com ili kujiridhisha kwamba Dowans siyo moja ya makampuni anayomiliki.
Al Adawi alisisitiza kuwa makampuni yake hayajishughulishi na mambo ya nishati bali ujenzi na kwamba Dowans siyo kampuni ya ujenzi.
Alisema iwapo kuna kampuni inatajwa kuwa yake wakati hajawekeza humo hata shilingi, basi angefurahi sana kupewa "kwa dezo" kampuni ya namna hiyo.
Hii ilikuwa na maana kuwa Jenerali Al Adawi haifahamu Dowans na wala hajawekeza katika kampuni hiyo.
Lakini kwa mujibu wa nyaraka mbalimbali za kampuni ya Dowans zilizopo kwa Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA), zinaonyesha Bregedia Jenerali Al Adawi kuwa mmoja wa wakurugenzi.
Anuani iliyotumika katika fomu hiyo ni P.O.Box 823, PC 112, Sultanate of Oman. Anuani hiyo ndiyo inayotumiwa na kampuni ya Services and Trade ya Oman ambayo Bregedia Jenerali Al Adawi alianzisha na mshirika wake mwingine mwaka 1977.
Al Adawi alipoulizwa uhusiano wake na mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, au uhusiano wa Rostam na Dowans, alikiri kumfahamu Rostam na kusema kuwa ni "rafiki" yake.
Alipoulizwa juu ya uhusiano wa Rostam na kampuni yake ya Dowans, na iwapo Rostam alimfuata na kumshawishi amsaidie kuanzisha kampuni ya Dowans, aling'aka, "Muulize mwenyewe; mbona unaniuliza maswali kama vile nahojiwa na polisi?"
 
Kaka Bubu Anataka Kusema, ninataka nisome comments / michango yako, lakini nakwazika, hizo font za blue unazozitumia nashindwa kuzisoma!!!
 
Inawezekana anamaanisha morogoro road pale tanesco zilipo power plants zao by the way nimeongea na jamaa yangu yupo pale analifuatilia nitawajuza
 
Sasa hapa patamu.... I hope wanakijiji alirecord hii interview ili jamaa asijekukana baadae watakapomuweka sawa

Kwa jinsi Mwanakijiji alivyo makini katika swala hili la mafisadi nchini mwetu ikiwemo hili la Dowans, bila shaka atakuwa amerekodi mahojiano hayo na huyu Jenerali AL Adawi.
 
Hivi katika hizo evidence zoooote, kuna hata moja inayoonyesha kuwa Dowans hawakuleta Mitambo ya kuzalisha umeme?
 
Hujajibu swali, yaani mnakazana evidence, evidence, evidence, lakini hamjaonesha hata sehemu moja ni wapi Dowans hawajaleta mitambo. Kwa kukusaidia:

...The Citizen yesterday, the turbine was air freighted to Tanzania and installed at the Ubungo site in late October 2006, and was commissioned in January 2007...

Soma zaidi: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/101372-richmond-sued-in-us-over-dar-power-deal.html
Mbona unauliza swali kama jibu unalo? Mafisadi bwana!
 
Kwa jinsi Mwanakijiji alivyo makini katika swala hili la mafisadi nchini mwetu ikiwemo hili la Dowans, bila shaka atakuwa amerekodi mahojiano hayo na huyu Jenerali AL Adawi.

Sababu hii Kampuni waliisajili zamani na wali-underestimate intelligence ya Mtanzania am sure kuna makosa mengi tu yamefanyika....

Kuna haja pia ya kumuangalia huyu Stanley Munai, probably na yeye atakataa involvement, hapo ndio sijui nani atakayelipwa? ila nadhani muda unavyokwenda hawa jamaa ndio wanasahihisha makosa yao.... Time is Running Out.
 
The bucks stops with Rostam Aziz...........katumia migongo ya rafiki zake pamoja na connections zake za ndani ya nchi KUTUIBIA............
 
The bucks stops with Rostam Aziz...........katumia migongo ya rafiki zake pamoja na connections zake za ndani ya nchi KUTUIBIA............

Alichoiba ni nini, mbona sijaona hata mmoja wenu kusema hiki hapa ndicho alichoiba Rostam. Japo cha kukisia tu.
 
Back
Top Bottom