Don Nalimison nimerudisha Kitambulisho Cha Taifa la Tanzania(NIDA) kuanzia sasa sina Kitambulisho cha Uraia wa Tanzania

Habari wadau,

Kiukweli huyu mtu hayuko sawa , watu walio karibu nae au kama kuna mtu anawafahamu ndugu zake awaambie kwamba Deo Kisandu anahitaji kupatiwa matibababu ya afya ya akili.

Tukimuacha huyu mtu anarudi tena jela maana kadri siku zinavyozidi kwenda naona taa inaanza kuwaka...Apelekwe kitengo cha afya ya akili apatiwe matibabu na matatizo yake yatapona.
 
Habari wadau,

Kiukweli huyu mtu hayuko sawa , watu walio karibu nae au kama kuna mtu anawafahamu ndugu zake awaambie kwamba Deo Kisandu anahitaji kupatiwa matibababu ya afya ya akili.

Tukimuacha huyu mtu anarudi tena jela maana kadri siku zinavyozidi kwenda naona taa inaanza kuwaka...Apelekwe kitengo cha afya ya akili apatiwe matibabu na matatizo yake yatapona.
cc. Maxence Melo
 
Don wakomeshe...hama na mtaa na ikibidi uwe unakula hoteli za kitalii na kulala hukohuko
 
Nimekuwa nikiona bandiko mbalimbali za huyu member lakini mpaka leo sijapata mantiki hasa tatizo ni nini? Ningelipenda aandae full package ya yaliyomsibu ili wadau tulililike.

(kwa mtindo wa wasifu wake), changamoto alizokutana nazo, nini akitarajiwacho na sababu gani zinamsukuma kufanya hayo yote.
 
Nimekabidhi Masjala Jiji la Mwanza, na pia nimewarudishia PSSSF Kitambulisho Cha LAPF na Pesa zote wakitaka wale au wazigawane, Mimi haya nihusu.@DON NALIMISON.View attachment 1526849
Mbona hutuambii kilichojiri? Hata hivyo, hongera kwa uamuzi wako na tunakutakia mafanikio kule uendako. Nikujuze tu mikasa ya watu kadhaa walioukana uraia wao.

Mtanzania mmoja alikwenda kuishi Sweeden miaka ya 70. Siku moja Rais Nyerere alikwenda kutembelea huko. Huyu mtu akahamasisha maandamano ya kumpinga Nyerere. Siku tarajiwa alijitokeza peke yake lakini polisi wakamruhusu atowe dukuduku zake katika hayo maandamano ya mtu mmoja.

Nyerere na Olof Palme wakasimama kumsikiliza akiitukana nchi maskini ya Tanzania. Akaukana uraia wa Tanzania na kuichana pasipoti ya Tanzania mbele ya wakuu hao. Ikumbukwe kuwa pasipoti ni mali ya serikali unayoazimishwa tu raia kukuwezesha kwenda nchi za kigeni. Ni sawasawa na noti za nchi. Wewe ukifanya kazi ukalipwa mshahara, hizo noti unazopewa ni kithibitisho tu kwamba umelipwa kiasi fulani lakini noti zenyewe zinabaki kuwa mali ya serikali. Huwezi kusema kwamba kwa kuwa umezifanyia kazi, uende ukazichome moto au kuzitupa chooni. Hilo ni kosa la jinai.

Pamoja na hayo, Mtanzania huyo aliyechana pasipoti ya Tanzania, kwa makubaliano kati ya Olof Palme na Nyerere, hakuchukuliwa hatua yo yote. ingawa alikuwa ametenda kosa la jinai. Hiyo ilikuwa kumuonyesha tu kuthamini uhuru wake wa kusema yaliyomo moyoni mwake.

Zaidi ya kuonyeshwa kwenye runinga siku hiyo, habari yake ndiyo ikawa imekwisha. Haikuwa na impact yo yote. Aliendelea kuishi huko Sweeden kwa kubangaiza na baada ya miaka yapata 15 hivi, maisha yakamshinda akawa anaomba kurudi Tanzania. Juhudi hizo zilimchukua miaka mitatu ndipo akafanikiwa kurudi Tanzania na mpaka leo bado anaishi.

Mwingine alikwenda Marekani akawa akiisema vibaya Tanzania kwenye vyombo vya habari akadiri hata kusema kwamba akifa asirudishwe kwemye nchi maskini hiyo. Baada ya miaka kadhaa maisha yalikuwa magumu sana kwake akafa. Ndugu zake wa hapa Tanzania wakishirikiana na Watanzania waliokuwa wakiishi na marehemu wakaamua kumrudisha tu Tanzania kwa mazishi, kinyume na aliyoyasema.

Mtanzania mwingine alikwenda kuishi Canada. Naye pia akawaakiisema vibaya sana Tanzania. Naye aliishia hivyo hivyo kama aliyefia Marekani.

Mfano mwingine ni Bokassa aliyekuwa akiitawala Central African Republic. Baada ya kuangushwa utawala wake alikwenda kuishi Ufafansa ambako alikuwa na majumba ya kifahari na alikuwa amejilimbikizia hela taslimu nyingi tu. Haikupita miaka mingi akaanza kudai arudi nchini kwake vyo vyote vile serikali ya nchini kwake itakavyoamua kumfanyia. Kweli ikawa hivyo na alifia nchini kwake.

Hayo ndiyo matatizo ya kumkwaza mamba kabla hujavuka mto.
 
Ee Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema, naomba kwa makusudi kabisa umsaidie huyu rafiki yangu Deogratius Kisandu, a.k.a Mtemi, a.k.a Masqo, a.k.a Rais Mtarajiwa wa JMT, a.k.a Don Nalimison, arudi katika hali yake ya kawaida.

Unatambua fika Ee Mwenyezi Mungu, huyu rafiki yangu mpendwa kuna 'fuse' moja kichwani mwake imekaa ndivyo sivyo.

Ninaomba haya yote kupitia kwa Mwanao Yesu Kristu, anayeishi na kutawala nawe, daima na milele. Amen.
 
Back
Top Bottom