Dodoma: Makamu wa Rais Dkt Mpango avunja mkataba wa kampuni ya kuzoa takataka ya Green Waste

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,140
Kumekucha.

Makamu wa Rais Dkt Phillip Mpango leo amefanya ziara ya kushtukiza kukagua shughuli za usafi jijini Dodoma.

Katika ziara hiyo iliyohusisha ukaguzi wa usafi kwenye masoko, Dr Mpango ameagiza kuvunjwa kwa mkataba wa kampuni ya Green Waste inayosuasua kuzoa takataka.
===
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 15 Januari 2022 ametembelea katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dodoma pamoja na Soko la Majengo kukagua utunzaji wa Mazingira katika maeneo hayo.

Akiwa katika mitaa hiyo Makamu wa Rais ameshuhudia uwepo wa takataka katika maeneo mbalimbali ambazo wananchi wamezikusanya lakini huchukua muda mrefu pasipo kuondolewa.

Wananchi hao wamemueleza Makamu wa Rais adha wanayoipata ya kuishi na takataka hizo jirani na maeneo yao kwa kipindi cha wiki mbili pasipo kuondolewa hali inayohatarisha usalama wa afya zao. Aidha wamesema licha ya kutoa fedha kwa mamlaka zinazokusanya takataka hizo lakini bado takataka hizo husalia katika maeneo yao ambayo pia hutumika kwa biashara za vyakula.

Amewataka viongozi wa Jiji la Dodoma kuchukua hatua za haraka katika kuhakikisha jiji hilo linakuwa safi pamoja na maeneo ya masoko na barabara zote.

Source: Star tv!
 
Aaaah kumbe ni mambo ya usafi mtaani ambayo hata Meya au Mwenyekiti wa halmashauri angetosha?! Nilidhani amevunja mkataba wa kampuni inayojenga stigliers gorge! Bwawa halikamiliki na mgao hausemeki mtaani. Au ile inayojenga SGR manake hiyo kitu hakuna timeline ya kukamilika
 
Loh!!!!hii kazi c bora wangekupa hata bwashee!!!!kweli hii nafasi haina lolote
Kumekucha.

Makamu wa Rais Dr Phillip Mpango leo amefanya ziara ya kushtukiza kukagua shughuli za usafi jijini Dodoma.

Katika ziara hiyo iliyohusisha ukaguzi wa usafi kwenye masoko, Dr Mpango ameagiza kuvunjwa kwa mkataba wa kampuni ya Green Waste inayosuasua kuzoa takataka.

Source: Star tv!
 
Kumekucha.

Makamu wa Rais Dr Phillip Mpango leo amefanya ziara ya kushtukiza kukagua shughuli za usafi jijini Dodoma.

Katika ziara hiyo iliyohusisha ukaguzi wa usafi kwenye masoko, Dr Mpango ameagiza kuvunjwa kwa mkataba wa kampuni ya Green Waste inayosuasua kuzoa takataka.

Source: Star tv!

Makamu wa Rais hana mamlaka hayo, yeye siyo rais.
 
Back
Top Bottom