Dkt. Wilbroad Slaa ndio chanzo cha migawanyiko CHADEMA

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,904
4,050
DR SLAA NA UTENDAJI KAZI
KATIBU MKUU wa chadema DK WILBROD SLAA ndio chanzo cha migawanyiko chadema moja alichangia sana kuondoka kwa makamanda shonza na mwampamba,pili katika ofisi yake barua za siri zimekua zikivuja mfano ni barua ya zito ambayo tuliisoma hp mtandaoni,tatu kumshinikiza prof baregu ajitoe katika tume ya katiba bila kutoa 7bu za kueleweka na kusababisha mjadala mkubwa ndani na nje ya chama,tano kukurupuka na kusema chadema hawatashiriki ujio wa obama kisha tunamwona mwenyekiti wake akiwa ikulu jambo hili limeleta mkanganyiko na migawanyiko source akiwa dr SLAA.NAFIKIRI IMEFIKA WAKATI CHADEMA WAKATAFUTA MTENDAJI MKUU HUYU AKAWA MSTAAFU KWA SASA KWANI MGEMA AKISIFIWA TEMBO HULITIA MAJI

=========MAJIBU KUTOKA KWA DR. SLAA==========​
Chilisosi,

Upotoshwaji ikiachwa kuendelea kwa muda mrefu hatimaye kuna watu wataamini ni ukweli. Naomba kujibu Mimi mwenyewe hoja zote zilizotolewa na mleta thread.

1) Ni dhahiri lengo la mleta thread ni kupotosha umma, na kujaribu kuchanganisha viongozi. Kuondolewa kwa Shonza, Mwampamba na kundi Lao ni matokeo ya tabia ya mbovu, utovu wa nidhamu, siyo tu ndani ya Chama, Bali hata ndani ya Chombo chao BAVICHA. Kamati ya kuwachunguza iliundwa Morogoro Katibu Mkuu hakuwepo. Hivyo ni wazi mleta mad a hajui au kwa makusudi tu ameamua kupotosha. Kwa Katiba ya CHADEMA namabaraza yake kuchukuliwa mtu hatua ya kinidhamu ni mchakato mrefu na unapitia vikao mbalimbali. Maswala ya nidhamu yanasimamiwa na Katiba ya Chama Toleo la 2006 Ibara za 5.4(1-4); Kukoma kwa uongozi ( Ibara 6.3.4(b na c na e). Mamlaka za Nidhamu zinatajwa Ibara ya 6.3.6 pamoja na Kanuni Mbalimbali za Chama nazo ziko ndani ya Kitabu cha Katiba. Mto mada au hajasoma, au ni mbumbumbu tu mwenye kutumika au mpotoshaji tu. Kama anavyosema mleta mada ni kweli, Dr Slaa anaweza kuamua tu, basi Dr Slaa ni sawa na Mungu. CHADEMA ni Kati ya vyama vichache vinavyofanya vikao vya kikatiba, siyo tu kwa mujibu wa Katiba na Mara nyingi kwa kutumia mamlaka ya vikao vya dharura. Kauli ya mleta mada ni matusi kwa wanachadema wote na hasa Kamati Kuu na Baraza Kuu, ambazo indigo vyombo vya maamuzi.

2)Barua ya Siri kuvuja. Hiki ni kichekesho. Ebu to a hadharani barua iliyovuja. Kwanza barua hiyo ikiwasilishwa kwa Katibu Mkuu kwa Dispatch ya Tarehe ngapi na nani kwa mujibu wa dispatch kaipokea. Hiyo itaonyesha Kama kweli barua hiyo ya siri ikiwasilishwa under tight confidential system. Pili, weka barua hiyo hadharani ili WanaJF waone Kama in a mhuri wa siri. na Kama imewekwa muhuri kwa siri imeandikwa kwa Katibu Mkuu peke yake au imenskiliwa kwa wengine. Iwapo imenakiliwa kwa watu wengine, kwanini hoja iwe imefuja toka kwa Dr Slaa. Barua iliyoko kwa Ofisi ya Katibu Mkuu imenakiliwa kwa watu au vyombo vinginevyo pia. Huhitaji kuwa na elimu ya darasa la kwanza kujua kuwa jambo lililopelekwa kwa watu wengi, huwezi kusema tu fulani ndiye kavujisha, labda uwe tu na sababu zako binafsi kusema hilo.

3) Hoja ya Profesa Baregu kutakiwa kujitoa kwenye Tume.Kama Source ya Gazeti basi nafikiri unasababu zote kumwuliza Prof. Baregu, nini hasa tulizungumza, na kama kuna wakati wowote alitakiwa ajitoe. Aidha, mwulize Profe. baregu Kama hayo tuliyozungumza ni ya Dr Slaa au ni utekelezaji wa maamuzi ya vikao vya maamuzi. No research no right to speak. Rafiki yangu kana unaandika kwa dhamira njema chunguza kwanza nafsi yako, na uwe na hofu ya Mungu. Kuwapotosha Watanzania kutakuwa na gharama kubwa kwa vile kuna siku uzalendo utatushinda Kama ilivyo Leo, na nitatetea chama na procedures za chama. CHADEMA inaongozwa kwa Katiba, Kanuni na Taratibu, ni wazi Dr Slaa asingeweza kwa utashi wake kutoa amri yeyote kwa mtu yeyote yule.

4) Ujio wa Obama na kauli mbalimbali zilizotoka nimejibu Leo asubuhi. Sijakagua, labda Mods awe ameondoa majibu yangu. Vinginevyo siwezi kujibu hoja hiyo hiyo, tena ya kipuuzi tu na au ya ki propaganda.

WanaJF na wote wenye mapenzi mema. Narudia tena hoja za aina hii zany lengo la ki propaganda zisitupotezee muda, na ndiyo maana Mara nyingi sizijibu. Mkiona nimepuuza hoja mjue kuwa nimepuuza kwa kuwa ni ya ovyo. Wapuuzeni wahusika hao Kama ambavyo tupuuze hoja zao.
 
vijana wapewe zaidi nafasi wazee wabaki tu km washauri kwani wameshazeeka na haifai kung'ang'ania madaraka mwishoe unaharibu
 
DR SLAA NA UTENDAJI KAZI
KATIBU MKUU wa chadema DK WILBROD SLAA ndio chanzo cha migawanyiko chadema moja alichangia sana kuondoka kwa makamanda shonza na mwampamba,pili katika ofisi yake barua za siri zimekua zikivuja mfano ni barua ya zito ambayo tuliisoma hp mtandaoni,tatu kumshinikiza prof baregu ajitoe katika tume ya katiba bila kutoa 7bu za kueleweka na kusababisha mjadala mkubwa ndani na nje ya chama,tano kukurupuka na kusema chadema hawatashiriki ujio wa obama kisha tunamwona mwenyekiti wake akiwa ikulu jambo hili limeleta mkanganyiko na migawanyiko source akiwa dr SLAA.NAFIKIRI IMEFIKA WAKATI CHADEMA WAKATAFUTA MTENDAJI MKUU HUYU AKAWA MSTAAFU KWA SASA KWANI MGEMA AKISIFIWA TEMBO HULITIA MAJI

Wewe una nafasi gani CHADEMA? Au unaandika kuhalalisha buku saba yako leo? Shonza nae ni mwanasiasa au ni kama ule mpira unaotumiwa mara moja?
 
Tatizo la babu ni woga, anawaogopa sana vijana wanaokuja kasi na anajua kuwa hana tena sifa za kugombea Urais
 
Mwacheni babu wa watu

"To know the enemy is half the victory"
 
DR SLAA NA UTENDAJI KAZI
KATIBU MKUU wa chadema DK WILBROD SLAA ndio chanzo cha migawanyiko chadema moja alichangia sana kuondoka kwa makamanda shonza na mwampamba,pili katika ofisi yake barua za siri zimekua zikivuja mfano ni barua ya zito ambayo tuliisoma hp mtandaoni,tatu kumshinikiza prof baregu ajitoe katika tume ya katiba bila kutoa 7bu za kueleweka na kusababisha mjadala mkubwa ndani na nje ya chama,tano kukurupuka na kusema chadema hawatashiriki ujio wa obama kisha tunamwona mwenyekiti wake akiwa ikulu jambo hili limeleta mkanganyiko na migawanyiko source akiwa dr SLAA.NAFIKIRI IMEFIKA WAKATI CHADEMA WAKATAFUTA MTENDAJI MKUU HUYU AKAWA MSTAAFU KWA SASA KWANI MGEMA AKISIFIWA TEMBO HULITIA MAJI

Unamaanisha propaganda za Mabomu , Tindikali na Ugaidi zimefeli kiasi cha kuleta hii nyepesi kabisa. Ivi kweli kuwatimua kina Shonza ni kubomoa chama au kujenga, hao ''makamanda'' wako unashuudia wanovoiboa CCM?! Barua ya Zitto ilivuja kabla ya kusainiwa, mjinga unaamini kuwa barua ilifika ofisini kwa katibu kabla ya kusainiwa
 
DR SLAA NA UTENDAJI KAZI
KATIBU MKUU wa chadema DK WILBROD SLAA ndio chanzo cha migawanyiko chadema moja alichangia sana kuondoka kwa makamanda shonza na mwampamba,pili katika ofisi yake barua za siri zimekua zikivuja mfano ni barua ya zito ambayo tuliisoma hp mtandaoni,tatu kumshinikiza prof baregu ajitoe katika tume ya katiba bila kutoa 7bu za kueleweka na kusababisha mjadala mkubwa ndani na nje ya chama,tano kukurupuka na kusema chadema hawatashiriki ujio wa obama kisha tunamwona mwenyekiti wake akiwa ikulu jambo hili limeleta mkanganyiko na migawanyiko source akiwa dr SLAA.NAFIKIRI IMEFIKA WAKATI CHADEMA WAKATAFUTA MTENDAJI MKUU HUYU AKAWA MSTAAFU KWA SASA KWANI MGEMA AKISIFIWA TEMBO HULITIA MAJI

vijana wapewe zaidi nafasi wazee wabaki tu km washauri kwani wameshazeeka na haifai kung'ang'ania madaraka mwishoe unaharibu

mkuu babu amechoka kinachomsaidia na kwa sababu ya roho ngumu na uroho wa madaraka lakini anapaswa kumwachia zito au mnyika.
Guys, why are you so much concerned with CHADEMA issues? Kama babu anaiharibu chadema nyie kinawauma nini, ilihali mnajulikana wazi ni wanaCCM? Kuharibika kwa CHADEMA si ndiyo faraja yenu ili nyie mfanikiwe? Sasa mnaumia nini? Au hata pilipili za shamba nyie huwa zinawawasha? Mind your business bwana, ya CHADEMA tuachieni CHADEMA wenyewe. Chama chenu kinaporomoka mchana kutwa, lakini hamuhangaikii kukinusuru, kucha kuchwa mnaiongelea CHADEMA.
 
Back
Top Bottom