Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,293
- 9,723
Ndugu zangu Watanzania,
Kwa namna dkt Tulia anavyokubalika,kupendwa, kuaminika na kuungwa mkono na wana Mbeya. kwa hakika uchaguzi ujao Dr Tulia atakuwa mbunge wa kwanza kushinda na kutangazwa mshindi mapema sana na kuacha wananchi wakifunga barabara na jiji zima kwa shangwe, nderemo na vifijo kushangilia ushindi wake.
Maana kila mtu anasubiri kwa hamu na kwa kiu kubwa sana siku na wakati ufike ili ampigie kura ya ndio Dr Tulia. kila mtu anataka kujiwekea historia ya kumpigia kura Rais wa IPU. kila mtu anataka kuitangazia Dunia kuwa hawakukosea kumchagua kuwa Rais wao wa IPU ,kwa kuwa hata wao wana Mbeya bado wanaendelea kumpenda na kumhitaji kuendelea kuwa mbunge wao.
Kwa sasa kila mwana Mbeya anataka kuja kupiga kura kama sehemu ya kutoa shukurani na asante kwa Dr Tulia kwa kazi kubwa aliyoifanya na kugusa maisha ya wana Mbeya wengi. Dr Tulia kwa sasa hahitaji kutumia nguvu katika kampeni maana wana Mbeya wanaendelea kumpigia kampeni kila siku, wanaendelea kuonyesha na kutaja mambo aliyoyafanya katika uongozi wake ambayo yalikuwa hayajawahi kufanywa na mbunge aliyemtangulia.
Kikubwa tuendelee kumuombea afya njema na nguvu za kuendelea kuwatumikia wana Mbeya .tumuombe Mungu aendelee kumpigania, kumtetea na kumlinda wakati wote. Mungu aendelee kuwa upande wake na kumuongoza katika kila hatua apigayo .lakini pia Dr Tulia naye aendelee kumtumainia na kumtegemea Mungu katika kila jambo kama ambavyo amekuwa akifanya siku zote .
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.