Dkt. Tulia Ackson kurithi Urais wa Tanzania, kutoka kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, baada ya Kuhitimisha ngwe zake Kikatiba

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
8,189
11,618
Kuchaguliwa kwa Dkt. Tulia Ackson kua Rais wa IPU kumebadili kabisa equation ya nani ndani ya chama Tawala kumrithi Dkt. Samia atakapohitimisha Ngwee zake za Utawala kikatiba nchini.

Ushindi wa Dkt. Tulia Ackson IPU umepandisha joto la kisiasa ndani ya chama Tawala na kuwalazimu wanaokusudia au kuonyesha nia ya kumrithi Rais alieoko Madarakani, warudi tena kwenye drawing table kujipanga upya kivingine. Ushindi wa kishindo wa speaker wa Tanzania, IPU ni dhihirisho la uwezo na kukubalika kwake kitaifa na kimataifa.

Endorsement ya Rais Samia kwa Dkt. Tulia Ackson kugombea Urais IPU, iliaambatana na surport kabambe mno ya hali na mali, na hiyo ndiyo ikawa ni dhihirisho la Rais Samia Suluhu Hassan kumuamini sana Dkt. Tulia, na kwakweli akavutiwa mno na uwezo wake mkubwa wa kuongoza na siasa zake tulivu, kitaifa na kimataifa.

Kwa ufupi Dkt. Tulia Ackson ndiye mwenye kupewa nafasi kubwa zaidi kumrithi Rais Dr Samia, atakapomaliza muda wake.

Elimu, Uzoefu wa kazi za kitaifa na kimataifa, Jinsia, Uadulifu, bidii, utumishi uliotukuka, weledi na umahiri wake katika kupanga na kusimamia hoja na masuala mbalimbali kitafa na kimataifa ni sifa za kipekee zitakazombeba Dr Tulia, ndani ya Chama Tawala lakini pia dhidi ya Upinzani nchini.

Jambo la Mwisho,
Rais, wa sasa kama atashindwa kuacha legecy kwenye maeneo mengine, basi bilashaka atapendelea kuacha legecy muhimu katika historia ya Tanzania. Nayo ni kuiacha nchi katika mikono salama ya Mwanamke jasiri, naye ni Speaker wa sasa wa Bunge la Tanzania Dr Tulia.

IPU-Inter Parliamentary Union.

Haya ni maoni na mtazamo wangu....
 
Ni nchi maskini kabisa duniani ndo zilizoshindanishwa Malawi, Somalia, tunaweza kusema wazungu waliamua tu kuipa Tanzania, hata bumunda angetuwakilisha angepewa.

Msituchoshe,[Ila tu anawaharibia soko wadada kwa wazungu.
 
Jambo la Mwisho,
Rais, atapendelea kuacha legecy muhimu katika historia ya Tanzania. Nayo ni kuiacha nchi katika mikono salama ya Mwanamke jasiri, naye ni Speaker wa sasa wa Bunge la Tanzania Dr Tulia.

IPU-Inter Parliamentary Union.

Haya ni maoni na mtazamo wangu....
Mkuu Tlaatlaah , kwanza naunga mkono hoja ila sio lazima mpaka Rais Samia akamilishe ngwe zake zote mbili.

Jambo kama hili, limesemwa jana humu Hongera Dkt. Tulia. Sasa unatosha kuchukua kijiti 2030 mimi nilichangia hivi
Ujumbe wangu kwa Rais Samia- Naona umemuona Tulia. Kusema kweli mwanamke mwenzako anaweza. Mjenge vizuri, mpe exposure, mjenge aendeleze haya mazuri yote unayoyafanya sana hasa katika kujenga uchumi imara kupitia sekta binafsi pale utakapomaliza uongozi wako. Mpe exposure apate kujifunza vizuri geopolitics. Na mwisho ikikupendeza chama chako kimpe kijiti akapeperushe bendera ya chama 2030.

Asanteni
Lord Denning
Kigali
Mkuu Lord denning , kwanza naunga mkono hoja Dr. Tulia awe mgombea wa urais wa CCM mwaka 2030.

Pili kwa vile Rais Samia alishauri 2025, twende na mgombea Mwanamke, japo wengi wanadhani Mwanamke huyo wa 2025 ni lazima awe Mama Samia, kwasababu ndio awamu yake ya pili, mimi pia Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!, hii maana yake 2025 Rais Samia is most likely but not necessarily ni lazima, yeye!, sio lazima, Mwanamke huyo, anaweza kuwa mwanamke mwingine yeyote, ila ukimuondoa Rais Samia as the No. 1 top lady in Tanzania, Dr. Tulia is the second!, hivyo 2025 anaweza kuwa ni Dr. Tulia!.

Kisha tembelea uzi huu, Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke angalia nilichosema kumhusu Dr. Tulia na uchaguzi wa 2030
Na kipindi hicho cha 2025- 2030 ndipo sasa sasa tufanye grooming ya Mwanamke atakaye kuja kugombea urais wa JMT kwa 2030, na kwa maoni yangu, Mwanamke huyu sii mwingine yeyote zaidi ya Dr. Tulia Akson Mwansasu, Spika wa sasa wa Bunge la JMT.
Hivyo kwa hoja yako hii ya Dr. Tulia kuwa mgombea urais wa JMT kwa tiketi ya CCM mwaka 2030, tunafanana!.
P
 
Mkuu Tlaatlaah , kwanza naunga mkono hoja ila sio lazima mpaka Rais Samia akamilishe ngwe zake zote mbili.

Jambo kama hili, limesemwa jana humu Hongera Dkt. Tulia. Sasa unatosha kuchukua kijiti 2030 mimi nilichangia hivi

Mkuu Lord denning , kwanza naunga mkono hoja Dr. Tulia awe mgombea wa urais wa CCM mwaka 2030.

Pili kwa vile Rais Samia alishauri 2025, twende na mgombea Mwanamke, japo wengi wanadhani Mwanamke huyo wa 2025 ni lazima awe Mama Samia, kwasababu ndio awamu yake ya pili, mimi pia Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!, hii maana yake 2025 Rais Samia is most likely but not necessarily ni lazima, yeye!, sio lazima, Mwanamke huyo, anaweza kuwa mwanamke mwingine yeyote, ila ukimuondoa Rais Samia as the No. 1 top lady in Tanzania, Dr. Tulia is the second!, hivyo 2025 anaweza kuwa ni Dr. Tulia!.

Kisha tembelea uzi huu, Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke angalia nilichosema kumhusu Dr. Tulia na uchaguzi wa 2030

Hivyo kwa hoja yako hii ya Dr. Tulia kuwa mgombea urais wa JMT kwa tiketi ya CCM mwaka 2030, tunafanana!.
P

very interesting.....
Shukran sana Pascal Mayalla na Lord denning kwa maoni mujarabu sana dhidi ya uelekeo wa siasa za Tz kwa siku za usoni, hususani ndani ya Chama Tawala, naona rythym zina uelekeo unaoshabihiana dhidi ya anaefikiriwa kumrithi Dr Samia wakati ujao..

Asanti kwa Link za kuchota maarifa pia
 
Mnatumia nini kufikiria?
Mnaona watanzania wapumbavu sana eeeh???
calm down mambo bado,

tumia hicho unachotumia wewe kufikiri vizuri, kufanya uamuzi na uchaguzi sahihi ili kuepuka ghadhabu dhidi ya machaguo au mapendekezo ya wengine baadae...
 
Napita wima mazuzu kwanini wasimpe Nchi, hata kikiwekwa kigoda kinagombea uongozi CCM kinachukua ushindi watu watakipogia kura kigoda
 
Kuchaguliwa kwa Dr Tulia Ackson kua Rais wa IPU kumebadili kabisa equation ya nani ndani ya chama Tawala kumrithi Dr Samia atakapohitimisha Ngwee zake za Utawala kikatiba nchini.

IPU-Inter Parliamentary Union.

Haya ni maoni na mtazamo wangu....
Hahahaaa! AshaRose aliishia wapi? Yeye hafai kuwa rais baada ya ya JK?
 
Back
Top Bottom