Dkt. Mwigulu Nchemba ateua wadau watakaotoa elimu ya mlipa kodi; wamo Hamisa Mobetto, Edo Kumwembe na Mbwana Samatta

Nyie mnaopinga hapo juu mnajielewa? Wewe uliyesoma upo mbwinde huko na mbwana samatta au edo kumwembe nani ana fan base kubwa na anaweza kusikilizwa akihamasisha kodi?
Swala la kodi linahitaji elimu na uelewa mkubwa tatizo hii nchi inaendeshwa kibongo movie watu hamjui hata kodi zinaatakiwa zikusanyweje halafu unaokota watu ni heri vyuo vinavyotoa elimu ya kodi vifutwe
 
Hao wote walifaa kupewa ubalozi wa kuhamasisha Utalii ila kwenye kodi sijui Mh. Waziri amewaza nini kwa hao wateule!!!
 
Bora huo ubalozi angempa mtu kama Diamond, Majizzo na celebrity wengine ambao wanajihusisha na ulipaji wa kodi mbalimbali kutokana na mishe zao.
 
Kaka hapa tunazungumzia serikali wewe unaleta mambo ya cocakola!!! Em kuwa serious isee. Hivi wajua kuwa mambo ya Taxation particularly tax compliance ni mambo complex hayahitajii midemko???
Wewe ndo hauko serious hujui hata Mambo ya online influencer au wamwonea wivu mabeto kisa hyo nafasi, tax hata Mimi naweza toa maelezo kwa umma kuhusu ulipaji Kodi na Wala haihitaji kuwa mtu wa PhD in tax management, unataka ku reach a certain group lazima utafte mtu wanaoelewana lugha. Na hivi tax compliance Ina kipi kipya mtu akielekezwa na kutoa ujumbe kwa umma?
 
Yeye mwenyewe waziri anatakiwa kwenda kukutana na mtaalamu wa kodi TRA apewe ABC za hesabu za kodi mbali mbali kwanza, allowable expenditure (including fees) zina influence vipi kodi, umuhimu wa kutunza kumbukumbu za matumizi (including fees receipts) kama evidence and so forth.

Halafu aone upuuzi wake ulipo kwenye kufanya hesabu za income (suppose rent is income taxable) na wazo lake kulipia tozo za nyumba kupitia luku wakati risiti wanakaa nazo wapangaji.

Heck ata system yenyewe ya kukusanya hiyo kodi TANESCO bado awajaindaa.

Sasa mtu ambae yeye mwenyewe elimu ya kodi hana, kwanini tushangae anapoteua watu ambao cluesless kwenye maswala ya kodi kama wahamasishaji.

Mambo mengine yanawezekana Tanzania tu.
Napendekeza Rais atumie muda wa kutosha kujifunza misingi iliyotumika kuanzisha TRA kama chombo nje ya mfumo wa kawaida wa uendeshaji na usimamizi wa utumishi wa umma. Baada ya hapo atagundua kuwa serikali kuingilia usimamizi na uendeshaji wa TRA ndiyo chanzo cha malalamiko yake juu ya utendaji wa chombo hicho. Tangu mwanzo KAZI ya Rais ilikuwa kuteua mtendaji mkuu(Commissioner General) na alikuwa HAAPISHWI NA RAIS. Aliwajibika kwa Bodi ya Wakurugenzi na kwa mbaaaali, kwa Waziri wa Fedha. Miaka ya mwanzo Waziri asingeweza hata kuingilia uteuzi wa watumishi. Hata kabla ya Waziri kupendekeza kwa Rais mtu wa kuteua kuwa Kamishna Mkuu alishauriana na na Bodi ya Wakurugenzi.
 
Acha kudharau na kuharibu ugali wa wenzio. Kwa taarifa yako, Misa alifaulu darasa la saba na kusoma sekondari ya serikali. Ana akili kuliko wewe, hawezi shindwa kuamwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa lao.
Kwani wewe huwezi?
 
Napendekeza Rais atumie muda wa kutosha kujifunza misingi iliyotumika kuanzisha TRA kama chombo nje ya mfumo wa kawaida wa uendeshaji na usimamizi wa utumishi wa umma. Baada ya hapo atagundua kuwa serikali kuingilia usimamizi na uendeshaji wa TRA ndiyo chanzo cha malalamiko yake juu ya utendaji wa chombo hicho. Tangu mwanzo KAZI ya Rais ilikuwa kuteua mtendaji mkuu(Commissioner General) na alikuwa HAAPISHWI NA RAIS. Aliwajibika kwa Bodi ya Wakurugenzi na kwa mbaaaali, kwa Waziri wa Fedha. Miaka ya mwanzo Waziri asingeweza hata kuingilia uteuzi wa watumishi. Hata kabla ya Waziri kupendekeza kwa Rais mtu wa kuteua kuwa Kamishna Mkuu alishauriana na na Bodi ya Wakurugenzi.
Hilo ndio jukumu la TRA na taasisi zote za kodi duniani ni quasi-governmental.

Tax ni sheria ambayo aspects zake zinabadilika badilika kila budget; TRA wanatoa mapendekezo kwa tafsiri yao walivyoilewa sheria (or atleast taasisi zingine ndio zinavyofanya duniani how to compute taxation with the new budget kama kuna mabadiliko au tozo mpya).

Sasa kwa sababu tax ni sheria na taasisi za kodi ni quasi-governmental tafsiri zao inaweza kinzana na independent firms; ndio maana unaona makampuni kama PwC na wao wanatafsiri sheria hizo hizo zetu na washauri makampuni makubwa namna ya kutumia sheria kupunguza kodi.

Matokeo yake tunabaki tunalalamika tu haya makampuni hayalipi kodi sahihi; kivipi wakati sheria zetu wenyewe. Wenzetu kwenye ku counter measures za kupambana na makampuni makubwa au tax lawyers waliobobea; na wao taasisi zao wanaajiri the best accountants of all sorts kwenye top posts.

Yeye Mwigulu anajitungia sheria hajui how it will work in income tax computation, admin challenges za kuitoa hiyo hela TANESCO kuipeleka ardhi, ikitoka ardhi ndio iende kwao.

Mtu kama huyo ata akimchagua Hamisa na Edo wala usishangae. Samatta knows about income tax kushinda Mwigulu na kasheshe yake anacheza mpira Europe so he has an idea; lakini hata yeye awezi hamasisha kwa sababu sidhani kama anaielewa hadi ajifanyie mwenyewe makadirio.

The whole thing ya mabalozi wa kodi is pathetic. Watu wanahitaji kupewa elimu ya kodi hiyo ndio motisha ya kulipa na wenye uwezo wa kuifanya hiyo kazi ni TRA wenyewe sema nao promotional mix yao inahitaji mtaalamu wa marketing to get their message across.
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amewateua Mbwana Samatta, Hamisa Mobeto na Edo Kumwembe kuwa mabalozi wa kuhamasisha ulipaji kodi. Mbali na hao amewateua wanasiasa wengine kuwa mabalozi wa elimu ya kodi, ili kuhakikisha wananchi wanalipa kodi bila kushurutishwa.
Hivi aliyetuloga hatuwezi kutafuta kaburi lake tukamuombe msamaha jamani?
Tuna safari ndefu sana sana kufika tunapotaka
 
Wewe ndo hauko serious hujui hata Mambo ya online influencer au wamwonea wivu mabeto kisa hyo nafasi, tax hata Mimi naweza toa maelezo kwa umma kuhusu ulipaji Kodi na Wala haihitaji kuwa mtu wa PhD in tax management, unataka ku reach a certain group lazima utafte mtu wanaoelewana lugha. Na hivi tax compliance Ina kipi kipya mtu akielekezwa na kutoa ujumbe kwa umma?
niambie Hamisa anaelewana lugha vip na walipa kodi wakubwa wa hii nchi?😂😂😂😂,
Pili ana miliki nini cha maana mpaka aonewe wivu?😂😂😂😂
 
Mwishoni utakuja kusikia zilitumika shilingi kadhaa kwenye blah blah za uhamasishaji kulipa kodi.hizi blah blah tuwaachie jamii za watu ambao tayari wameshastaarabika na wana elimu pana ya ulipaji kodi na wanajua umuhimu wa kulipa kodi kwasababu matumizi sahihi ya kodi yao yanaonekana kilichobaki ni kukumbushwa tu tofauti na sisi ambao elimu ya mlipa kodi yenyewe hatuijui vizuri na maisha yenyewe hayaeleweki.Kama waziri kawalenga wafanya biashara wakubwa sawa ila kama kalenga kuhamasisha jamii nzima ya walipa kodi hii kwangu naona ni kichaka kama vichaka vingine kwasababu sisi ndo tuko kwenye hatua za awali za kuelimishwa kulipa kodi na kuwekeana mipaka ya matumizi na nidhamu ya pesa za umma.Sasa hivi tulitakiwa kuwaza kuongeza nguvu kwenye kitengo cha elimu ya mlipa kodi kifike kila kona ya nchi na kudhibiti ubadhirifu na matumizi holela na yasiyo na umuhimu vinginevyo tuambiwe hao mabalozi wataifanya hiyo kazi bure na iwe bure kweli kweli.
 
Watangaze tu nafasi za ajira waliosomea hayo Mambo wapate Kazi yenye kuleta impact kwenye nchi
 
niambie Hamisa anaelewana lugha vip na walipa kodi wakubwa wa hii nchi?,
Pili ana miliki nini cha maana mpaka aonewe wivu?
Kwani kutoa elimu au tangazo kuhusu swala la Kodi lazima uingie studio.
Hamisa ni maarufu na anajulikana kuliko wewe unayejiona umesoma huku hujulikani hata na mjumbe.
 
Wewe ndo hauko serious hujui hata Mambo ya online influencer au wamwonea wivu mabeto kisa hyo nafasi, tax hata Mimi naweza toa maelezo kwa umma kuhusu ulipaji Kodi na Wala haihitaji kuwa mtu wa PhD in tax management, unataka ku reach a certain group lazima utafte mtu wanaoelewana lugha. Na hivi tax compliance Ina kipi kipya mtu akielekezwa na kutoa ujumbe kwa umma?
Sinaga wivu wa kijinga to that extent. Mimi nazungumza uhalisia na ukweli. Kama waona tax haina kimya kiasi yeyote anaweza kuhamasisha, bora tuishie hapa..!!
Kumbuka tu serikali sio business entity kiasi ikahitaji meneja masoko wa kuvutia wateja...!!
 
Back
Top Bottom