Dkt. Mpango: ATCL ishughulikie tatizo la kuahirishwa au kusogeza mbele muda wa kuanza safari za Ndege zake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akipokea ndege ya Abiria, Boeing 737-Max 9, leo Oktoba 3, 2023.


Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amesema bado kuna malalamiko ya wateja wa ATCL kuhusu huduma za usafiri ikiwemo kuahirisha safari au kusogeza mbele muda wa kuanza safari hasa kiwanja cha ndege cha Mwanza na vinginevyo.

Baada ya kupokea ndege hii mpya, matarajio ya watanzania ni kuona ATCL sasa inamaliza kabisa kero hiyo ya kuahirisha au kufuta safari.

Aidha, ameitaka Wizara ya Uchukuzi ifuatilie kwa ukaribu ubora wa huduma unaotolewa na ATCL.
 
Namuona Mganilwa hapa 'analia lia' kuhusu ndege za twin engine. Ningeshauri wapewe ile ndege ya Fokker 70 waitumie kwa mazoezi kama bado inafanya kazi.
images (1).jpeg
 
Una maanisha usukuma (ushamba)Bado umetamalaki???Nchi hii?? Kama ndo unamaanisha hivyo jibu ni yes Kwa sababu hizi steps Ndio zinaakisi ujinga wetu
 
Haya mambo hufanywa na nchi za kusadikika tuu.Wangejua vijijini Hali ya kilimo na mifugo ilivyo wasingefanya haya
Juzi tu kwenye ziara ya Bibie huko kusini watu walikuwa wakimlilia kuwa hakuna maji.
 
Vipaombele kwa Africa ni zero kabisa, zilizoko biashara inasuasua wanaleta nyingine,

Wangeendeleza hata barabara ya mbezi chalize mpaka watakapofika,

Kuna mengi ya kufanya
Hii mikataba walishaingia , hivyo lazima itekelezwe.
Ifike wakati watanzania tuwe waelewa sana. Hizi ndege lazima zije huwezi vunja mikataba hata kama unaona ni hasara kwa biashara hiyo.
 
Yani hapa uswahilini Kila kitu hadi kiwe na uzinduzi na kiongozi mkubwa wa nchi lazima awepo, bila kufanya hivyo inatokea nini labda 🤔🤔 nikimaliza kuezeka nyumba yangu ya tope Kijijini nitawaalika waje kufanya uzinduzi kwa sababu ndio kazi wanayo weza
 
Back
Top Bottom