Dkt. Kijaji: Uongozi Mkoa wa Tanga shirikianeni na Taasisi kutatua changamoto za wafanyabiashara

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji(Mb.) ameushauri uongozi wa Mkoa wa Tanga kushirikiana na Taasisi husika kutatua changamoto za wanazopata wafanyabiashara wa Jiji la Tanga.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Agosti, 3 2023 alipokua na wafanyabiashara Jijini Tanga kwa lengo la kusikiliza changamoto zao za kibiashara na kuzitafutia ufumbuzi.

Aidha, amebainisha kuwa Dhamira ya Serikali nikulirudisha jiji la Tanga kuwa jiji la Viwanda nchini kama hapo awali ili liweze kutoa ajira kwa vijana kukuza biashara na uchumi wa Taifa .

Vilevile, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rai wa Jmhuri ya Muungano wa Tnzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeamuaa kukabidhi uchumi katika sekta binafsi ili uchumi uwe imara ndani na nje ya Nchi.

Dkt. Kijaji pia ameishauri TRA isiwabebeshe mzigo wafanyabiashara kwa kulimbikiza kodi bali ameitaka TRA ishirikiane na wafanyabiashara hao na kiwapa elimi kuhusu ulipaji kodi ili kukuza uchumi.

WhatsApp Image 2023-08-04 at 12.17.38.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-04 at 12.17.39.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-04 at 12.17.40.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-04 at 12.17.42.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-04 at 12.17.40(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-08-04 at 12.17.43.jpeg
 
Kumbukumbu yangu ya tanga usije ukaenda dukani kwa mtu ukiwa na haraka, eti nipimie nina haraka, anakurudishia pesa yako akikuambia kanunue paleeeee, kama una haraka
 
Kumbukumbu yangu ya tanga usije ukaenda dukani kwa mtu ukiwa na haraka, eti nipimie nina haraka, anakurudishia pesa yako akikuambia kanunue paleeeee, kama una haraka
Hahahaaa ni kweli mkuu,ikifika saa 11 mtu anafunga mahesabu anaenda kupumzika na wake zake,kesho aamka Saaa mbili....yaaan fresh tu Wala hawana jamuu na kusaka pesaa kivilee......😀😀
 
Bwana mmja Toka balaa alipata kazii huko Tanga,akanunua pikipiki...sikumoja akawapita wazee speed mavumbi yakawafuataa...wachaaaa walichukiaa kinomaaa.Wakajiapiza kijana ajifanya anaharakaa hatafikaa aendakoo🤣🤣Jamaa aliendesha pikipiki mpaka Saaa kumi Toka saa mbili hafiki, tambua hapo ni sehemu ya kwenda lisaa limoja tu....mpaka aliposhtuka akarud omba msamahaa🤣🤣
 
Back
Top Bottom