Dk Kimei (CRDB) kuwania tuzo ya kinara benki Afrika

Crdb-means community rural development bank-ilianza kama saccos miaka ya sabini na baadae transformnation mpaka crdb
 
Unahaki ya kukataa asipewe hiyo tuzo, lakini huwezi kupinga mafanikio yake. Hata mwenyewe inawezekana ulisha ficha maovu mkeo asiyajue. Tofauti ni aina ya uovu
 
Kama kuna benki mbovu na ya hovyo zaidi nchini basi ni CRDB. Nilianza kuidharau kipindi kile cha EPA ambapo mwanzoni Kenya Commercial Bank (KCB) waliona mtiririko usio wa kawaida wa ufunguaji akaunti na uwekaji hela wakakataa na kuitaarifu BoT.

Mafisadi yalivyoona hivyo wakaamua kupitishia pesa haramu CRDB (eti benki ya wazawa!) wakifungua akaunti hadi siku za mapumziko; labda baada ya kuona hivyo na ili waweze kuendelea na ufisadi wao ndio maana wameamua baadhi ya matawi ya-operate hadi sikukuu ili wapate utetezi mbele ya sheria huko tuendako; kuna siri zaidi ya tunavyodhani ni kumjali mteja.

Kama mchango wangu kwa taifa, nilichoweza kufanya ni kufunga mara moja akaunti yangu niliyokuwa nayo CRDB mara baada ya ile kashfa ya EPA japo haikuwa na hela ya maana. Lakini angalau nilionesha hisia zangu hata kama ni kilio cha samaki.

Hata hivyo, nikiri kwamba, pamoja na kufunga akaunti yangu, lakini kwa namna moja ama nyingine "inanilazimu" kutumia huduma za CRDB hasa kama kulipa ada za watoto, n.k. Huduma zao bado ni bomu mno. Inaweza kukuchukua hata saa nzima kumfikia teller hata kama kwenye queue ni mtu wa tatu. Jibu rahisi ni MTANDAO UNASUMBUA.
M
Eti benki ya aina hii, BENKI ISIYO NA JINA, ndio inawania nafasi ya benki bora Africa! Pathetic! Anayefahamu kirefu cha CRDB atufahamishe.

NISeme kweli toka Moyoni kwa maoni haya sasa Watanzania wanajionesha wazi wazi kwamba wanajielewa. HIVYO, hatuwezi kumshabikia mtu aliyefanya mambo ya Hovyo ati sababu tu ni Mtanzania wa kwanza Kuingia kwenye tuzo hizo. Mtu kama hafai hata kama ni Babako au mfadhili Wako. Huyo Dr. amesaidia sana kufanikisha UFISADI kwa KUTUMIA elimu yake badala ya Kujenga heshima yake na ya watanzania. Vile vile anaonekana anapenda sana kujipendekeza ili apate cheo au tuzo, bahati nzuri sana umeutafuta sana UGAVANA wa BOT bila mafanikio
 
Kama kuna benki mbovu na ya hovyo zaidi nchini basi ni CRDB. Nilianza kuidharau kipindi kile cha EPA ambapo mwanzoni Kenya Commercial Bank (KCB) waliona mtiririko usio wa kawaida wa ufunguaji akaunti na uwekaji hela wakakataa na kuitaarifu BoT.

Mafisadi yalivyoona hivyo wakaamua kupitishia pesa haramu CRDB (eti benki ya wazawa!) wakifungua akaunti hadi siku za mapumziko; labda baada ya kuona hivyo na ili waweze kuendelea na ufisadi wao ndio maana wameamua baadhi ya matawi ya-operate hadi sikukuu ili wapate utetezi mbele ya sheria huko tuendako; kuna siri zaidi ya tunavyodhani ni kumjali mteja.

Kama mchango wangu kwa taifa, nilichoweza kufanya ni kufunga mara moja akaunti yangu niliyokuwa nayo CRDB mara baada ya ile kashfa ya EPA japo haikuwa na hela ya maana. Lakini angalau nilionesha hisia zangu hata kama ni kilio cha samaki.

Hata hivyo, nikiri kwamba, pamoja na kufunga akaunti yangu, lakini kwa namna moja ama nyingine "inanilazimu" kutumia huduma za CRDB hasa kama kulipa ada za watoto, n.k. Huduma zao bado ni bomu mno. Inaweza kukuchukua hata saa nzima kumfikia teller hata kama kwenye queue ni mtu wa tatu. Jibu rahisi ni MTANDAO UNASUMBUA.

Eti benki ya aina hii, BENKI ISIYO NA JINA, ndio inawania nafasi ya benki bora Africa! Pathetic! Anayefahamu kirefu cha CRDB atufahamishe.

commercial rural development bank
 
Tatizo watu tunachanganya tuhuma na kushtakiwa .......ni kweli EPA zilipigwa ila Benki na serikali na hao mafisadi wote wameziweka chini ya carpet kwa hiyo imebaki kuwa tuhuma tuu , tukirudi kwenye mambo ya kibenki CRDB ndio ina Amana kubwa kuliko benki zote ....Jamaa amekuwa MD wa benki kwa zaidi ya 15 years .......benki inafanya vizuri ...tumeona madudu ya wabongo wakipewa nafasi za kuongoza mabenki afadhali jamaa amekomaa miaka yote hii.......Mimi nampongeza.......kila la kheri
 
Yaani wabongo huwa tunaangalia mabaya tu ! mazuri hatuangalii, Kimei anastahili kabisa kupata Tunzo hata hizo account za epa sio kazi yake kufungua, benk ni nyingi sana yeye kama mtendaji atawezaje kuangalia hii accout ni ya nani na hii ni ya nini hata kama ni robot litachoka tu. mwacheni mtu wa watu afanye mambo yake akingali hai. :angry:
 
Duh! Hii kali. Kwa hiyo CRDB ni neno la kiwapi hilo Mkuu? Ni kichina, kisukuma, kireno, au? Kama ni la Kiswahili, kwa mara ya kwanza Kiswahili kimepata neno linaloundwa na "makonsonanti" matupu; kama ni Kiingereza basi kimepata neno la kwanza linaloundwa na consonants tupu zaidi ya tatu! Huu ni ubabaishaji ulikubuhu kwa viwango vyote. Linapaswa kuingizwa kwenye kamusi ya lugha husika kama neno jipya!

Kumbe ndio maana wanaiita CDRB Bank? I thought ile "B" ilimaanisha "Bank" kumbe ni sehemu ya neno lenyewe na ndio maana inafahamika kama CRDB Bank; ha ha ha!

Mkuu habari ndio hiyo.
 
Yaani wabongo huwa tunaangalia mabaya tu ! mazuri hatuangalii, Kimei anastahili kabisa kupata Tunzo hata hizo account za epa sio kazi yake kufungua, benk ni nyingi sana yeye kama mtendaji atawezaje kuangalia hii accout ni ya nani na hii ni ya nini hata kama ni robot litachoka tu. mwacheni mtu wa watu afanye mambo yake akingali hai. :angry:

Kenya Commercial Bank (KCB) waliwezaje? Nani alitakiwa kuwa mzalendo zaidi kwa Tanzania kati ya CRDB na KCB?
 
crdb unaweza fungua akaunti hata siku ya mapumziko, wanachojali ni hela hata kama ni haramu
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei amechaguliwa kwenye mchakato wa kumtafuta Kinara wa Benki Afrika kwa mwaka 2013.

Mchakato huo unaendeshwa na African Banker Awards chini ya African Development Bank Group.

Kinara wa benki wa mwaka, ni tuzo inayotolewa kwa viongozi (CEO`s) wa sekta ya benki na fedha barani Afrika, ambao wamepata mafanikio makubwa kwenye mashirika yao hivyo kuleta maendeleo kwenye sekta fedha na uchumi kwa nchi zao.

African Banker Awards imechagua vinara watano wa sekta ya fedha Afrika kuingia katika mchakato huo, mmoja wao ndiye atakayejitwalia tuzo hiyo.

Zaidi ya Dk Kimei, wengine waliongia kwenye mchakato huo na nchi wanazotoka kwenye mabano ni Segun Agbaje wa GTB Bank (Nigeria), Aigboje Aig wa Imoukhede-Access Bank (Nigeria), Andrew Allly wa Africa Finance Corporation (Nigeria) na Jao Figuerdo wa Unico Bank.

Dk Kimei ni Mtanzania wa kwanza kuingizwa kwenye mchakato huu tangu kuanzishwa kwa tuzo hiyo zaidi ya miaka kumi iliyopita, npia ni pekee kwenye kinyang’anyiro hicho ambacho kimekuwa kikitawaliwa na benki kutoka Nigeria na Afrika ya Kusini.

Dk Kimei ambaye ni mchumi mwenye Stashahada ya Uzamivu, amefanya kazi sekta ya fedha kwa zaidi ya miaka 30 akitokea Benki Kuu ya Tanzania (BoT), alikokuwa Mkurugenzi wa Sera na Utafiti kabla ya kujiunga CRDB mwaka 1998 kama Mkurugenzi Mkuu.

Akiwa CRDB ameiongoza kutoka benki iliyokuwa ikijiendesha kwa hasara hadi inayoongoza nchini.
Benki hiyo imefanya marekebisho mbalimbali, ambayo yameiletea mafanikio na kuwa miongoni mwa benki zinazoongoza nchini.

Chanzo: Mwananchi

Akiwa CRDB ameiongoza kutoka benki iliyokuwa ikijiendesha kwa hasara hadi inayoongoza nchini. (mwongo sana wewe mwandishi)Benki ilikuwa ikitengeneza Faida hata kabla ya CRDB, Kabla ya Kimei CEO alikuwa Mr Mann ambaye aliongoza vizuri tu, kwa vile mann hakuwa karibu na wanasiasa akapigwa chini, ndo Kimei kuletwa na hao wanasiasa toka BOT.
Ndo maana EPA, KAGODA NA FRAUD nyingi zipita sana CRDB kwa sababu ya wanasiasa wanaitumia sana. SASA hivi Kimei anakaribia kustaafu amempachika cheo ndugu yake toka uko Kasikazini kama Deputy MD hili apate experience na si vinginevyo. Branch managers wengi ni kutoka uko Kasikazini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei amechaguliwa kwenye mchakato wa kumtafuta Kinara wa Benki Afrika kwa mwaka 2013.

Mchakato huo unaendeshwa na African Banker Awards chini ya African Development Bank Group.

Kinara wa benki wa mwaka, ni tuzo inayotolewa kwa viongozi (CEO`s) wa sekta ya benki na fedha barani Afrika, ambao wamepata mafanikio makubwa kwenye mashirika yao hivyo kuleta maendeleo kwenye sekta fedha na uchumi kwa nchi zao.

African Banker Awards imechagua vinara watano wa sekta ya fedha Afrika kuingia katika mchakato huo, mmoja wao ndiye atakayejitwalia tuzo hiyo.

Zaidi ya Dk Kimei, wengine waliongia kwenye mchakato huo na nchi wanazotoka kwenye mabano ni Segun Agbaje wa GTB Bank (Nigeria), Aigboje Aig wa Imoukhede-Access Bank (Nigeria), Andrew Allly wa Africa Finance Corporation (Nigeria) na Jao Figuerdo wa Unico Bank.

Dk Kimei ni Mtanzania wa kwanza kuingizwa kwenye mchakato huu tangu kuanzishwa kwa tuzo hiyo zaidi ya miaka kumi iliyopita, npia ni pekee kwenye kinyang’anyiro hicho ambacho kimekuwa kikitawaliwa na benki kutoka Nigeria na Afrika ya Kusini.

Dk Kimei ambaye ni mchumi mwenye Stashahada ya Uzamivu, amefanya kazi sekta ya fedha kwa zaidi ya miaka 30 akitokea Benki Kuu ya Tanzania (BoT), alikokuwa Mkurugenzi wa Sera na Utafiti kabla ya kujiunga CRDB mwaka 1998 kama Mkurugenzi Mkuu.

Akiwa CRDB ameiongoza kutoka benki iliyokuwa ikijiendesha kwa hasara hadi inayoongoza nchini.

Benki hiyo imefanya marekebisho mbalimbali, ambayo yameiletea mafanikio na kuwa miongoni mwa benki zinazoongoza nchini.

Chanzo: Mwananchi

My Take;
CRDB chini ya Dr Kimei ni benki ambayo imetumika kisiasa yaani imekuwa ikishirikiana na mafisadi ndani ya utawala wa CCM. Katika tukio la EPA benki hiyo inayoelezwa kuwa ni ya wazawa ilihifadhi fedha zailizochotwa (zilioibiwa) kutoka BoT na wale wezi naye akakaa kimya.

Katika ule mchoto wa Kagoda mabilioni yaliwekwa katika akaunti sita za matawi ya benki hiyo na baadaye kuchotwa na watu eti hadi leo hawajulikani hadi leo!!! Hii inawezekana kwa benki kubwa kama hiyo kutojua ilimlipa nani mabilioni hayo na zile akaunti alizifungua nani?

Pili CRDB chini ya Kimei iliisaidia sana kampuni feki ya Richmond kuwapatia guarantee ya letter of credit kuisadidia ufisadi wao.

Kwa hali hii Dr Kimei hafai kupata tuzo hiyo.

Nawasilisha.

waislamu tunazidi kuonewa, kwa nini asipewe sheikh ponda?
 
Back
Top Bottom