Dk. Ali Mohamed Shein amesema yeye bado ni Rais wa Zanzibar

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,790
1.jpg

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema yeye bado ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na kutoa changamoto kwa wasioiamini Katiba hiyo kupeleka shauri hilo Mahakama Kuu ya Zanzibar ambayo ndiyo pekee yenye uwezo wa kutafsiri Katiba.
 
Last edited by a moderator:
Swala sio kwamba yeye sio Rais
Hoja ni kwamba atoke aliyeshinda atangazwe naye aingie !!

Vinginevyo mlifuta ili muendelee kwa mujibu wa katiba hiyo Hiyo
 
1.jpg

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema yeye bado ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na kutoa changamoto kwa wasioiamini Katiba hiyo kupeleka shauri hilo Mahakama Kuu ya Zanzibar ambayo ndiyo pekee yenye uwezo wa kutafsiri Katiba.

Sheria iliompa mamlaka ndio hiyo hiyo inayomuwekea ukomo kwa kutokuchaguliwa asije kuwa
BAGBO mwingine
 
Kwa hakika naendelea kujiridhisha pasina shaka kwamba madaraka/utawala ni MVINYO MKALI kweli kweli hasa kwa watawala (viongozi?) wa Kiafrika.
 
Sheria iliompa mamlaka ndio hiyo hiyo inayomuwekea ukomo kwa kutokuchaguliwa asije kuwa
BAGBO mwingine
Huyu ni Bagbo tayari. Jamaa na udaktari wote halina hata haya limeng'ang'ania madarakani wakati limeshindwa. Aibu!
 
ikitokea bahati mbaya wananchi wazanzibar wakianza kuuwana tutakuja kutumia nguvu kubwa sana huko tuendako kwa kutafuta muafaka wa kupatana
nashauri mshindi atangazwe haraka ili kuepusha maafa
 
1.jpg

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema yeye bado ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na kutoa changamoto kwa wasioiamini Katiba hiyo kupeleka shauri hilo Mahakama Kuu ya Zanzibar ambayo ndiyo pekee yenye uwezo wa kutafsiri Katiba.

Anamwambia nani?
 
Xx kuna tofauti gan kati yake na Nkurunzinza. Unafiki tu wa watz kuingilia masuala ya Burundi wakati Nkurunzinza mwngne yupo huku.
 
Tokea alipoapishwa baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka 28/10/215 kwa muda wa takriban miaka mitano, aliwahi kusema kuwa, mimi ndiye raisi wa Zanzibar? Mbona anajitia wasi wasi mwenyewe? Aendelee tu kukaa wenzake walifia kwenye mitaro ya maji machafu na walikuwa wanatenda kila aina ya jema kwa wananchi wao na bara zima la Afrika. Yana mwisho hayo!

Damu ya binadamu ina thamani zaidi ya matakwa yake ya uongozi
 
Huyu ni Bagbo tayari. Jamaa na udaktari wote halina hata haya limeng'ang'ania madarakani wakati limeshindwa. Aibu!

Ndugu yangu shida ya hawa jamaa ni CCM na UNAFKI wa kiswahili. Kudhani wanafikiri zaidi ya wananchi wenye kutoa MADARAKA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom