Diwani wa Monduli na M/kiti wa UVCCM Monduli ndani ya CHADEMA!

Diwani wa Monduli na M/kiti wa Uvccm Monduli Julius Kalanga ametangaza rasmi kumfuata rafiki yake Nillya Chadema. Kwenye FB yake aliulizwa na mtu fulani kama atamfuata rafiki yake Millya Chadema au la yeye akajibu, siwezi kumwacha rafiki yangu aende mwenyewe huko. Itakuwa pigo jingine kubwa kwa CCM kwani jamaa ni kichwa yaani jembe la nguvu na ana ufuasi mkubwa sana Monduli. Yeye atachukua Monduli, Millya Sumanjiro, jamani Rahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!

anguko la ccm limefika, kosa ni kukumbatia matajiri na kusahau wanyonge
 
Roma yenyewe ilianguka sembuse MAGAMBA,Mungu kasikiliza maombi ya walio wengi. Na iwe hivyo kama ilivyosemekana,tunasubili uthibitisho
 
Ngome ya Lowassa iko Monduli si rahisi kiasi hicho

Kila ngome ina mwisho mkuu kwani ulitegemea mwisho wa ngome ya lowassa uweje tena zaidi ya tunachokishuhudia. Hata Gaddafi na Al-seif hawakuamini kwamba mwisho wao umefika hadi pale Gaddafi alipolambwa risasi na kufa. Ni bora uone mwisho wako ukaanza mbele mapema kuliko kukejeli alama zinazoashiria mwisho na kusubiri kwani hutajua utaangukia nyuma au pua au kwa kishindo kikubwa namna gani.
 
Nimesoma kwenye wall yake anaifagilia ccm kuwa ni chama kubwa.
 
Julius Kalanga, Diwani wa Monduli, M/kiti wa UVCCM Wilaya ya Monduli na kada mtiifu wa Lowassa sema jambo braza watanzania wanaisubiri kauli yako
 
M4C milele

Ibarikiwe Chadema, wabarikiwe wanyonge wa nchi hii, abarikiwe Mzee Mustafa SABODO yule mzalendo shupavu wa Taifa letu.

Huko uliko, upate rehema upumzike kwa amani Mwl. Taifa uliloliacha kwa manyang'au wachache linaelekea kupata wakombozi sasa.
 
source kasema ni kupitia mtandao wa kitabu cha uso


FACEBOOK!

nimeongea naye hivi karibuni kwa simu anasema hakuna kitu kama hicho na wala hana mpango huo ili kwa kuwa millya ni rafiki yake masuala ya tofauti za kiitikadi haziwezi kuwatenganisha ili mradi lengo lao ni kuwatetea vijana,wasilisha
 
Ili taarifa ithibitike kuwa ya kweli shusha ushahidi hapa. kwa sababu,"No research no right to speak / write".
 
Back
Top Bottom