Dira Na Utume

Blah blah blah blah Watu wana njaa ya mabadiliko wewe unaleta theories za vision mision kwani tuko shule hapa.Watu washike silaha waingie mitaani,hiyo ndio sulihisho.

Hilo sio suluhisho bwana Sozi. Hiyo njaa ya mabadiliko walikuwa nayo wasomali kwa kumchoka sana Gen Mohammed Siad Barre, na kweli wakamng'oa. Kilichofuata baada ya hapo sote tunakiona hadi leo, hakuna utulivu. Kosa lao? Waliung'oa utawala bila maandalizi makini ya kuweka utawala mwingine, likawepo ombwe (vacuum) ambalo factions nyingi zikawa zinagombea kulijaza, ikawa anarchy hadi leo.

Kama tumemchoka mbebaji wa chungu chetu cha asali, tuandae mbebaji mwingine kabla hatujamnyang'anya huyo chungu hicho, la sivyo tukisema tumnyang'anye kwanza ndipo tutafute mbebaji, anaweza akakosekana, matokeo yake tunamwaga kila kitu.

Tuandae kwanza timu yenye uwezo wa kuchukua madaraka, yenye acceptance nchi nzima, na yenye vision inayokubalika, ndipo tushawishi watu jamani ondoeni CCM madarakani wekeni chama B kwa sababu kadha kadha kadha.

Unapowaambia watu waikatae CCM wakati hawaoni alternative, hawawezi kukukubalia. Pengine baadhi yetu wanaamini alternative ipo, lakini wapiga kura walio wengi hawajaliona hilo! Kazi ya kufanya ni kuwaonesha hiyo alternative na kuwashawishi juu ya suitability yake, na jinsi ilivyo bora kuliko utawala uliyopo.

Nina mfano rahisi. Kipindi fulani huko Bongo nilishiriki katika kampeni moja ya utunzaji wa mazingira, na mojawapo ya ujumbe tuliokuwa tunawapa watu ni kupunguza idadi ya mifugo na kuachana na ufugaji wa kuhamahama. Walikuwa wanatusikiliza tu, hawasemi kitu. Lakini baadae mzee mmoja akanifuata na kuniambia "mmekuja tu kutembea, hakuna kitakachobadilika hapa!" Sababu aliyonipa ni kuwa wao hawajui kazi nyingine, na namna ya kufuga wanayojua wao ndio hiyo, sasa tunataka waache halafu wataishije? Ile kampeni kusema kweli tulifeli kwa sababu ya kukosa maandalizi makini.

Nataka tuelewe kwamba watanzania wanao uwezo wa kutathmini na pale wanaporidhika na kitu huwa wanakichukua. Mifano ipo mingi. Katika majimbo ambayo wananchi waliridhika kwamba alternatives walizopewa ni bora kuliko CCM, walichagua hizo. Tumeyaona hayo Karatu, Kigoma, Tarime, Pemba, Biharamulo, Moshi mjini na sehemu nyingine ambako wananchi wamechagua upinzani. Hata sehemu ambazo mchuano wa uchaguzi ulikuwa mkali (tuseme ambako upinzani ulipata 40% ya kura au zaidi), tunaweza kusema gauge ya kukubalika ilikuwa inapanda, na kuna matumaini ya chama kilichopata kiasi hicho kwamba kina nguvu pale, nina uhakika yapo majimbo ambayo upinzani haukushinda lakini ulikaribia sana, hayo pia ni matumaini makubwa yanayopaswa kulelewa ili next time ushindi upatikane. Changamoto iliyoko kwa upizani ni kuzalisha wagombea wengi wenye uwezo wa kuichachafya CCM nchi nzima, yaani majimbo yote nchini CCM wawe wanahangaika kama walivyoangaika Kigoma, Moshi mjini, Karatu, Pemba, Ubungo nk, hapo wananchi wataona kweli kuna uchaguzi. Maana uchaguzi unapaswa uwe fursa ya kuchagua kimoja kati ya kadhaa ambavyo vyote vinafaa, lakini mwananchi anatafuta chenye kufaa zaidi. Sasa iwapo mwananchi ataona anapaswa kuchagua kati ya gari bovu linalotembea na kitu kingine ambacho hana uhakika kama ni gari au kibanda, basi anaona bora hilo gari bovu, atasogea sogea!

Kama huko Lindi, Mtwara na kwingineko hawajapata kuona mgombea wa upinzani wa kukaribia kufanana na kina Zitto, Ndesamburo, Wangwe, Mnyika na wengine wa namna hiyo, tuna haki gani ya kuwalaumu kwa kuichagua CCM? Vyama vya siasa vina wajibu wa kujijenga nchi nzima na kuwa na "bank" ya wagombea wazito na wazuri nchi nzima, hapo hata wananchi wanaelewa tukiondoa CCM tunaweka hawa hapa tunawaona. Hii ndio changamoto tuliyonayo kabla ya kuzungumzia kumng'oa rais wa CCM (maana kuna wanaodhani ati kuchagua rais wa upinzani ndio kuiondoa CCM madarakani! bado kabisa!) Kuiondoa CCM madarakani ni kuondoa mfumo wote, na ili hilo lifanikiwe tunahitaji mfumo mbadala ulio tayari kuchukua nafasi hiyo mara. Tujenge na kuuimarisha huu mfumo mbadala kwanza.
 
Kithuku

Asante sana kwa hoja zako nzito.

Kama nimekuelewa vizuri, dira/ujumbe wa ukombozi unaopendekeza wewe ni: "kujenga mfumo mbadala wenye viongozi bora katika ngazi zote"

Nashukuru. Bado naendelea kusibiria michango ya wote. Hatimaye baada ya siku kadhaa nitaweka hizi hoja zote pamoja kupata 'dira/ajenda/ujumbe' unaopeswa kubebwa na chama au vyama mbadala vinavyolenga kuomba ridhaa ya wananchi kuongoza dola mwaka 2010.

Tuendelee na mjadala mpaka kielewe

JJ
 
Hivi kwa nini tunaogopa mijadala? Tatizo liko wapi kama mjadala utakuwa academic? Mimi binafsi ningefurahi kama mkitueleza mtatufikishaje huko mnakotaka kutufikisha kwa kutumia rasilimali ambayo tunayo. Ningependa mtueleze mtatuondoaje kwenye ujinga uliotanda kwa kutumia kipato chetu wenyewe. Mtueleze vipi mtatuhakikishia wake zetu na watoto wetu hawafi wakati wa uzazi. Mtueleze vipi mtaulinda urithi (mbuga za wanyama, mazingira masafi, miji yetu ya kihistoria n.k.)tulioachiwa na babu zetu ili na wajukuu wetu waweze kuufaidi. Mtueleze mtatuhakikishiaje kuwa haki inatolewa kwa wote bila upendeleo wa aina yeyote. Mtueleze vipi mtakuwa nasi katika safari hii ndefu kutoka hapa tulipo bila wenzetu kutuacha sis tukisukuma gari kwenye matope wakati wenzetu mmekaa ndani kwenye kiyoyozi. Mtueleze mtafanyaje yote haya kwa kutumia kipato tulichokuwa nacho na si ndoto za alinacha. Mtueleze mtafanya nini ili makosa ambayo wenzenu wameishayafanya hayatarudiwa.

Fundi Mchundo.

Tuendelee na mjadala. Ila niseme hapa kwamba utaona mwanzoni nimeweka CHADEMA itafanyaje? Falsafa, itikadi na ilani yetu ya mwaka 2005. Lakini nikaweka bayana kwamba lengo la mjadala huu wa sasa si sisi kusema tutafanyaje? Ni wananchi kusema chama au vyama vitakavyochukua dola mwaka 2010 vifanyaje? Ni wasaa wa kusikiliza sauti ya wananchi.

Kama nimeisikia vizuri sauti yako. Wewe unataka chama au vyama hivyo viwe na dira/ujumbe/ajenda ifuatayo: serikali yenye kuweza kulinda na kutumia urithi wa taifa kujitegemea na kuhakikisha haki na usawa ikiwemo katika kutoa fursa za elimu na afya kwa wote
 
Kama nimeisikia vizuri sauti yako. Wewe unataka
chama au vyama hivyo viwe na dira/ujumbe/ajenda ifuatayo: serikali yenye kuweza kulinda na kutumia urithi wa taifa kujitegemea na kuhakikisha haki na usawa ikiwemo katika kutoa fursa za elimu na afya kwa wote

Na "justice" kwa wote bila kupendelea. Pamoja na wazo lako zuri nadhani kuna umuhimu nyie mtueleze mtatupelekaje huko mnakokusudia. Tuachane na platitudes, tuelezane ukweli. Tuwaige wamarekani kwenye hili; unatoa proposal, unaulizwa utailipia vipi? Nakataka kujua mtatekelezaje ilani zenu? Mtalipia vipi? kwa kuongeza kodi n.k? Nimechoka kuwa condesceded to! Tunahitaji specifics na sio generalities.
 
Kama nimeisikia vizuri sauti yako. Wewe unataka

Na "justice" kwa wote bila kupendelea. Pamoja na wazo lako zuri nadhani kuna umuhimu nyie mtueleze mtatupelekaje huko mnakokusudia. Tuachane na platitudes, tuelezane ukweli. Tuwaige wamarekani kwenye hili; unatoa proposal, unaulizwa utailipia vipi? Nakataka kujua mtatekelezaje ilani zenu? Mtalipia vipi? kwa kuongeza kodi n.k? Nimechoka kuwa condesceded to! Tunahitaji specifics na sio generalities.

Fundi Mchundo

Nashukuru

Mtalipia vipi? Hii ni upande wa jinsi ambavyo tungeweza kuongeza mapato ya serikali; baadhi ya mambo ambayo yangefanyika ni pamoja na:

1. Kwa kubadili mfumo wa utawala na kuunda serikali ndogo adilifu yenye kuwajibika zaidi kwa wananchi; tungepunguza matumizi ya serikali na kuondoa gharama za anasa- hii ingebakiza fedha kwa ajili ya vipaumbele vingine vya serikali. Pia kwa ujumla tungeshughulikia rushwa ikiwemo zile kubwa kubwa ili kuhakikisha fedha zinazofujwa kutokana na ufisadi zinaelekezwa katika matumizi yenye kuboresha maisha ya wananchi.
2. Kupitia sera yetu ya uchumi- tungepunguza kiasi cha kodi kama VAT zinazogusa watu wengi na hivyo kuongeza kodi kupitia kwa ongezeko la walipaji kodi na na ulipaji kodi(widening tax net and ensuring tax compliance). Tungepunguza misamaha ya kodi, na kuweka mamlaka ya kupitisha misamaha ya kodi kwa bunge- hapa tungepata mapato makubwa toka kwa walipa kodi wakubwa ambao hawalipi kutokana na mianya na misamaha.
3. Tungepitia upya mikataba yote mikubwa ya uwekezaji yenye utata- hii ni ikiwemo mikataba katika masuala ya rasilimali kama madini nk. Kwa ujumla tungeweka mifumo ya kisheria na kuingia mikataba ambayo ingeleta mapato kwa serikali na hata kwa wananchi waliopo katika maeneo yenye maliasili/rasilimali hizo.

Baadhi ya vyanzo mbadala vya mapato tulivitumia wakati wa kuandaa bajeti mbadala ya kambi ya upinzani- unaweza kusoma hapa: http://www.chadema.net/hotuba/misc/hotuba_1.html

Lakini, la msingi zaidi; tungeunda serikali ambayo inaweka mazingira bora ya kisera kwa wananchi kuweza kupata fursa za kimaendeleo kila mtu kadiri na kipaji na uwezo wake; hapa nazungumza suala zima la uwezeshaji. Maeneo ambayo yangewekewa mkazo ni elimu, kilimo , ajira na afya. Tazama ilani fupi hapa http://www.chadema.net/maoni/ilani.php utaona kwa kila eneo tulipanga kufanya nini. Na ieleweke kwamba hii ni ilani fupi ambayo ilijumuisha masuala kadhaa kipaumbele, ipo ilani pana ambayo iliingia kwa undani zaidi kwa kila eneo kutoa ufafanuzi. Hii ilani fupi iliandaliwa kama muktasari wa vipaumbele na ikazalishwa kwa wingi kwa ajili ya kusomwa na watu wengi zaidi. Ilikuwa fupi na ilinakshiwa kwa picha ili hata mwananchi wa kawaida aweze kuvutika kuisoma na kuielewa.

Naamini maelezo haya yamekupa picha; lakini hiyo ni dira/ajenda/ujumbe wa 2005; tunapoelekea 2010 lazima tupate maoni ya wananchi wanasema nini pia badala ya wanachama pekee wa vyama kujifungia na kuandaa bila kushirikisha umma. Turudi kwenye mjadala wetu.

JJ
 
Mada nzuri na imekuja wakati mwafaka hasa wakati huu Wakenya wakituonesha namna ya kukomesha ufisadi.

Bila kuingia kundani kwenye suala zima la "dira na utume" napenda kuonyesha wasiwasi na masikitiko yangu kuhusu CHADEMA ambayo katika sehemu kubwa ya 2007 iliweza kuwashawishi Watanzania kuwa sio kila chama cha upinzani ni mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya.Lakini baadhi ya matukio ya hivi karibuni ndani ya chama hicho yameniacha nikiwa na wasiwasi kuwa kama hatua madhubuti hazitachuliwa basi kinaweza kujikuta kinaparaganyika kama NCCR ya Mrema na Marando,et al.

Calling a spade a spade,kama CHADEMA haitoweza kumdhibiti Wangwe basi lolote linaweza kutokea.Uongozi ni pamoja na nidhamu na sio kuropoka kila ovyo.Nimesoma katika gazeti flani ambapo Bw Mnyika umetetea uhuru wa kukosoana hata hadharani,lakini mnafanya hivyo kwa manufaa ya nani?Kama unafikiri kukosoana hadharani ni suala jema,then mna umuhimu gani wa kuwa na vikao vya chama?Pamoja na ufisadi na ubabaishaji wake uliobobea,CCM ina sifa moja kuu ya nidhamu miongoni mwa viongozi wake.Whether nidhamu hiyo ni ya lazima (udikteta) au ni ridhaa ya viongozi,la muhimu hapa ni kwamba viongozi wasio na nidhamu miongoni mwao watawezaje kuonyesha nidhamu ya kuongoza nchi pindi wakikabidhiwa jukumu hilo?

Kwanini,naizungumzia CHADEMA na sio chama kingine cha upinzani?Jibu ni kama nilivyosema hapo awali,chama hiki kimetuaminisha wengi in 2007 kwamba kina viongozi wenye uchungu na nchi na ujasiri wa kuwafumbua macho wananchi namna nchi yao inavyotafunwa na mafisadi.Unfortunately,in the past few weeks CHADEMA imekuwa ikisikika zaidi kwa kinachodaiwa kuwa ni clash of interests miongoni mwa viongozi wake wakuu.Tatizo hapo ni ubinafsi,na kama sote tunavyofahamu,ubinafsi unaweza kuzaa lolote lile including ufisadi.

Bila kuleta hisia za ukabila,yayumkinika kusema kwamba baadhi ya wenzetu wanaotoka mkoa wa Mara wana kasumba ya kusukumwa na emotions,ambazo si ajabu zikaishia infront of common sense.Sikubaliani na Zitto kwa kauli yake kuwa uchumi unakua,na naafikiana na Wangwe kumpinga katika hilo.Lakini ilihitajika busara katika kupingana huko,just like K alivyowapinga akina Sitta,Mudhihir,Karamagi,nk katika uamuzi wao wa kitoto wa kumfungia Kabwe.Hakuwaumbua hadharani bali kwa kumjumuisha Zitto kwenye kamati ya Madini aliwaonyesha wapi walipokosea,na ujumbe umefika.Wangwe alikuwa na kila fursa ya kumpinga Zitto kwenye vikao vya ndani vya CHADEMA lakini sio kwenye media.Msipokuwa makini katika kuelewa "another" motive ya kila mwandishi kumhoji mwanasiasa (which is to sell news,especially if it smells like a scoop) mtaishia kuonekana ni wababaishaji just like hao CCM mnaodhamiria kuwaondoa madarakani.Controversy makes and sells news,na kwa watu kama Habari Corporation walio tayari kusaliti dira ya msingi ya magazeti yao ili kuwafurahisha watawala,mmegeuka kuwa chanzo kizuri cha habari kwao,huku mkijikaanga kwa mafuta yenu wenyewe.

Ni wazo zuri ku-seek mawazo ya Watanzania kuhusu dira na utume wa chama,pasipo kujali itikadi zao za kisiasa.Lakini,ili mawazo hayo yawe na maana,hamna budi mturidhishe kuwa hatupotezi muda wetu kuwashauri watu manaoshindwa kushauriana wenyewe kuhusu umuhimu wa nidhamu katika medani ya uongozi.

Wakati napatwa na matumaini kwa kuona upinzani unavyojitutumua kuiondoa serikali madarakani huko Kenya,nabaki uncertain kama hilo linawezekana huko nyumbani hasa kutokana na mwenendo wa CHADEMA hivi karibuni (CHADEMA because binafsi naamini kilianza kujiweka katika nafasi nzuri ya kutengeneza formirdable opposition wakati wananchi wengi wanatafuta mbadala wa CCM).

Finally,Mnyika,nadhani umesoma ushauri wa Mwanakijiji hasa umuhimu wa neno "NO COMMENT" pale mnapoandamwa na waandishi wa habari kuhusu mambo ambayo yakitafsiriwa vibaya kidogo na consumers wa habari,yatawaaminisha wananchi kuwa nanyi"hamna mpango".It can be done,kwani iliwezekana Ghana na sasa inaelekea kujirudia tena Kenya,kwa chama serious cha upinzani kukiondoa madarakani chama kilichochoka kuongoza kama CCM.As to DIRA na UTUME,nadhani la muhimu ni kuweka mbele maslahi ya nchi.Bila hilo,tunaweza kukesha hapa kuwapa ushauri na mkaishia kung'oana meno kwenye vikao na majukwaani kwa minajili ya umaarufu (ubinafsi).
 
Kithuku, kweli hatutaki kumwondoa Alhji Siad Baare na kumweka Farah Ideed, wala Dr.Kaunda na kumweka Chiluba kisa tu mabadiliko. Myika hapa sio platform ya kupandia, JF ni upupu unawasha! naona umeshaanza kuomba msaada wa Admn abadilishe mada, bado hujatuambia ilikuwaje Tarime wakakosa nafasi ya viti maalumu.
 
Eddy

Ulisema ukimaliza kutazama mwelekeo wa uchaguzi Kenya utakuja na hoja ambazo si za 'kitoto'! Ndio hoja hii uliyoleta?

Hapa si platform ya kupandia, ni jukwaa la kujadiliana. Tuendelee na mjadala.

Nionyeshe wapi nimeomba msaada wa Adm abadili mada? Nilichoshauri ni kubadilishwa kwa kichwa cha habari cha mada sio mada yenyewe. Hivyo mada hii itaendelea kuwepo hata kama itabadilishwa kama nilivyopendekeza.

Hilo la Tarime kukosa viti maalumu nimelieleza bayana hapa na nimesema wazi kwamba kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi iliyotungwa na Bunge la CCM majina ya wabunge wateule wa viti maalum yanapaswa kuwasilishwa na chama kabla ya matokeo ya uchaguzi kufahamika, katika mazingira hayo- hata kama uteuzi ungekuwa ni kwa mujibu wa majimbo ambayo chama kimeshinda hakuna ambaye angekujua kwamba kwa hakika kama tungeshinda Tarime. Kwa hiyo kama kigezo cha kugawa viti maalumu ungependa kiwe ni maeneo ambayo chama kimeshinda inabidi kwa kweli ushawishi kwanza CCM waongoze marekebisho ya sheria ya uchaguzi. Mambo hayo nimeyajadili maeneo mengi, pitia michango yangu utapata majibu- hapa nimegusia kidogo http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=113490#post113490. Na ukitaka mjadala kuhusu mwelekeo wa CHADEMA per se nashauri uingie hapa: http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=8326 ama kama ni kuhusu mikakati ya kampeni ingia hapa:http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=8283. Hii thread hii tuendelee na mjadala kuhusu dira/ajenda/mwelekeo. Kama una hoja kuhusu hili zimwage tujadili, kama una hoja tofauti ziweke kwenye thread zinazohusika ama fungua thread tofauti nitakufuata huko tujadili pia.

JJ
 
Mada nzuri na imekuja wakati mwafaka hasa wakati huu Wakenya wakituonesha namna ya kukomesha ufisadi.

Bila kuingia kundani kwenye suala zima la "dira na utume" napenda kuonyesha wasiwasi na masikitiko yangu kuhusu CHADEMA ambayo katika sehemu kubwa ya 2007 iliweza kuwashawishi Watanzania kuwa sio kila chama cha upinzani ni mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya.Lakini baadhi ya matukio ya hivi karibuni ndani ya chama hicho yameniacha nikiwa na wasiwasi kuwa kama hatua madhubuti hazitachuliwa basi kinaweza kujikuta kinaparaganyika kama NCCR ya Mrema na Marando,et al.

Calling a spade a spade,kama CHADEMA haitoweza kumdhibiti Wangwe basi lolote linaweza kutokea.Uongozi ni pamoja na nidhamu na sio kuropoka kila ovyo.Nimesoma katika gazeti flani ambapo Bw Mnyika umetetea uhuru wa kukosoana hata hadharani,lakini mnafanya hivyo kwa manufaa ya nani?Kama unafikiri kukosoana hadharani ni suala jema,then mna umuhimu gani wa kuwa na vikao vya chama?Pamoja na ufisadi na ubabaishaji wake uliobobea,CCM ina sifa moja kuu ya nidhamu miongoni mwa viongozi wake.Whether nidhamu hiyo ni ya lazima (udikteta) au ni ridhaa ya viongozi,la muhimu hapa ni kwamba viongozi wasio na nidhamu miongoni mwao watawezaje kuonyesha nidhamu ya kuongoza nchi pindi wakikabidhiwa jukumu hilo?

Kwanini,naizungumzia CHADEMA na sio chama kingine cha upinzani?Jibu ni kama nilivyosema hapo awali,chama hiki kimetuaminisha wengi in 2007 kwamba kina viongozi wenye uchungu na nchi na ujasiri wa kuwafumbua macho wananchi namna nchi yao inavyotafunwa na mafisadi.Unfortunately,in the past few weeks CHADEMA imekuwa ikisikika zaidi kwa kinachodaiwa kuwa ni clash of interests miongoni mwa viongozi wake wakuu.Tatizo hapo ni ubinafsi,na kama sote tunavyofahamu,ubinafsi unaweza kuzaa lolote lile including ufisadi.

Bila kuleta hisia za ukabila,yayumkinika kusema kwamba baadhi ya wenzetu wanaotoka mkoa wa Mara wana kasumba ya kusukumwa na emotions,ambazo si ajabu zikaishia infront of common sense.Sikubaliani na Zitto kwa kauli yake kuwa uchumi unakua,na naafikiana na Wangwe kumpinga katika hilo.Lakini ilihitajika busara katika kupingana huko,just like K alivyowapinga akina Sitta,Mudhihir,Karamagi,nk katika uamuzi wao wa kitoto wa kumfungia Kabwe.Hakuwaumbua hadharani bali kwa kumjumuisha Zitto kwenye kamati ya Madini aliwaonyesha wapi walipokosea,na ujumbe umefika.Wangwe alikuwa na kila fursa ya kumpinga Zitto kwenye vikao vya ndani vya CHADEMA lakini sio kwenye media.Msipokuwa makini katika kuelewa "another" motive ya kila mwandishi kumhoji mwanasiasa (which is to sell news,especially if it smells like a scoop) mtaishia kuonekana ni wababaishaji just like hao CCM mnaodhamiria kuwaondoa madarakani.Controversy makes and sells news,na kwa watu kama Habari Corporation walio tayari kusaliti dira ya msingi ya magazeti yao ili kuwafurahisha watawala,mmegeuka kuwa chanzo kizuri cha habari kwao,huku mkijikaanga kwa mafuta yenu wenyewe.

Ni wazo zuri ku-seek mawazo ya Watanzania kuhusu dira na utume wa chama,pasipo kujali itikadi zao za kisiasa.Lakini,ili mawazo hayo yawe na maana,hamna budi mturidhishe kuwa hatupotezi muda wetu kuwashauri watu manaoshindwa kushauriana wenyewe kuhusu umuhimu wa nidhamu katika medani ya uongozi.

Wakati napatwa na matumaini kwa kuona upinzani unavyojitutumua kuiondoa serikali madarakani huko Kenya,nabaki uncertain kama hilo linawezekana huko nyumbani hasa kutokana na mwenendo wa CHADEMA hivi karibuni (CHADEMA because binafsi naamini kilianza kujiweka katika nafasi nzuri ya kutengeneza formirdable opposition wakati wananchi wengi wanatafuta mbadala wa CCM).

Finally,Mnyika,nadhani umesoma ushauri wa Mwanakijiji hasa umuhimu wa neno "NO COMMENT" pale mnapoandamwa na waandishi wa habari kuhusu mambo ambayo yakitafsiriwa vibaya kidogo na consumers wa habari,yatawaaminisha wananchi kuwa nanyi"hamna mpango".It can be done,kwani iliwezekana Ghana na sasa inaelekea kujirudia tena Kenya,kwa chama serious cha upinzani kukiondoa madarakani chama kilichochoka kuongoza kama CCM.As to DIRA na UTUME,nadhani la muhimu ni kuweka mbele maslahi ya nchi.Bila hilo,tunaweza kukesha hapa kuwapa ushauri na mkaishia kung'oana meno kwenye vikao na majukwaani kwa minajili ya umaarufu (ubinafsi).

Mlalahoi

Nakushukuru kwa kuona chama mbadala na tumaini jipya kupitia CHADEMA. Utaona katika mchango wangu wa kwanza kabisa wakati naanza mjadala huu nilitambua uwepo wa mjadala kuhusu hayo uliyoyasema na nilikiri kwamba ujumbe umefika. Kisiasa najua unaelewa maana ya 'ujumbe umefika kwa wahusika'. Nikuhakikishie kwamba nimesoma ukurasa kwa ukurasa yaliyosemwa na mwanakijiji na wote waliochangia- tutayafanyia kazi. Kama una lolote la ziada ni vyema ukaliweka kwenye hii thread hapa: http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=8408 ili hapa tusipoteze lengo la mjadala huu.

Mambo yote uliyashauri ni hoja ambazo CHADEMA inapaswa kuzifanyia kazi, nimezichukua kama zilivyo. Ndio maana umeona katika mjadala huo japokuwa kuna mengi ya kusema ukimya wangu unaonyesha kuwa nimemua kuchukua msimamo wa 'no comment'. Uamuzi wangu wa kutumia mfano wa uteuzi Zitto kwenye kamati ya madini (ambao wengi walidhani CHADEMA ingeparanganyika) ulikuwa na nia ya kuonyesha kwamba hiki ni chama kinachoongozwa na timu yenye dira na malengo yanayoshabihiana hivyo utofauti wa kimaoni kuhusu masuala mbalimbali haupaswi kuchukuliwa ni mgogoro kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vinavyojaribu kujenga taswira hiyo kwa nguvu. Nilieleza bayana kwamba CHADEMA ikishakaa katika vikao vya maamuzi tunatoka na msimamo wa pamoja na ndio ambao tunausimamia kwa pamoja. Lakini kauli yangu hii haiondoi umuhimu wa kuwa na utaratibu katika kuzungumza na vyombo vya habari, na masuala ya kanuni za uwajibikaji wa pamoja kupitia vikao kwanza. Ila cha msingi hapa kwanza ni kuondoa hisia zote zinazojaribiwa kujengwa mbele ya umma kwamba tuna mgogoro na makundi, kwa sisi tuliondani tunajua kwamba hakuna na ni wajibu wetu kusema ukweli kwamba hakuna. Kadiri tunyamazavyo hisia za kwamba tuna mgogoro umma utaaminishwa kuwa ni za kweli na matokeo yake yatakuwa hayo uliyoyasema. Fahamu kwamba tumedhamiria kuilinda taasisi inayoitwa CHADEMA kwa gharama zote watanzania waendelee kuwa na chama mbadala. Nisingependa tujadili hili hapa zaidi. Turudi kwenye mjadala wetu wa msingi. Nini unadhani serikali mpya ya mwaka 2010 inapaswa kufanya? au ungependa kuona inaleta? Nini Dira/ajenda/mwelekeo?

JJ
 
Mh Bwana mdogo, inaonekana hata urais wa daruso hukuwahi kugombea, dalili zilishaonekana mapema kuwa tarime itaangukia upinzani kutokana na mvutano ndani ya ccm tarime! kwahiyo chadema waliamini kilimanjaro was stronghold.

ccm waliamini kushinda pempa ilikuwa kazi! bado walipendekeza wajumbe toka pemba. cuf nao wanauwakilishi bungeni kutoka mwanza japo haikuwa stronghold yao, kaka kagomee ushinde kwanza ndio utuletee hizo slogan.
 
Eddie,

Dalili zingeonyesha vipi wakati sheria inataka majina yawe yamewasilishwa zaidi ya mwezi mmoja kabla ya tarehe ya kupiga kura? Kama CCM ingeshinda viti sita kama CHADEMA je, ingegawa vipi kimikoa au kijumuia za vyama hivyo viti? Inabidi kufikiria katika picha pana zaidi. Leo CCM inapata urahisi wa kugawa kwa kuwa inapata viti vingi kuliko idadi ya mikoa ndio maana kanuni yao ya mgawanyo wa mikoa inaonekana kuwa bora. Ngoja upinzani ushinde viti vingi zaidi mwaka 2010 kiasi kwamba CCM ipate viti vichache kuliko idadi ya allocation ya mikoa ama jumuia za chama ndio utajua upana wa huu mjadala. Ndio maana nikashauri ingie hapa ukaendeleze huu mjadala: http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=113490#post113490 . Kumbuka haya malalamiko yalikuwepo pia UVCCM baada ya nafasi ya marehemu Amina Chifupa kuzibwa na mwakilishi toka UWT badala ya vijana. Hivyo, mjadala wa viti maalum ni mpana sana. Na mimi maoni yangu wakati wote yamekuwa ni katiba na sheria ya uchaguzi vifanyiwe marekebisho kuruhusu mfumo mpana zaidi wa uwakilishi wa uwiano(PR). Hata sisi orodha yetu ya viti maalumu iliyoko Tume ya uchaguzi inajumuisha mpaka waombaji wateule kutoka mara, pemba nk; kwa maneno mengine kwa mujibu wa sheria akipungua mmoja kati ya sita waliopo kwa sababu yoyote basi anatangazwa anayefuatia katika orodha. Kama tungepata viti maalumu sawa zaidi ya 35 ni wazi kwamba mikoa mbalimbali ingekuwa na uwakilishi. Kawaulize CUF kwamba kigezo kilikuwa ni mikoa- kama ingekuwa hivyo mbona mikoa mingi haijawakilishwa?

Hapa sizungumzii mimi kugombea kwa kweli, slogan yangu pale ubungo ilikuwa bayana: Kizazi Kipya, Maisha Mapya, Ubungo Mpya. Lakini haya si tunayojadili hapa kwa kweli. Hapa tunajadili taifa. Bado nasubiria hoja zako za 'kiutuuzima' kuhusu dira na utume kama ulivyoahidi.

Tuendelee na mjadala: Nini iwe dira/ajenda/mwelekeo wa serikali mpya itayoingia madarakani 2010?

JJ
 
SISIEMU wana migogoro kibao, kuimaliza wanafunga watu midomo kwa vitisho na kugawa vyeo. Ukijifanya kusema ukweli na kuwa mtetezi wa hoja unaondolewa kwenye system, ukikaa kimya bila kupinga unaachwa uendelee kula.Ukimya ulioko SISIEMU ni sawa na ile kitu tunaita Latent Heat of Vaporation. Majiyafikapo 100 Centigrade na yageukapo kuwa mvuke lakini joto lake halibadiriki, hata hivyo mvuke huwa na nguvu kubwa ya kuunguza kuliko maji yenye joto lilelile. Ndani ya SISIEMU kuna Fukuto liongezalo ukubwa matatizo bila kutoa mikwaruzo nje ya system.

Kuhusu Sera. Moja ya mambo makuu yanayo daiwa yamo katika Sera ya SISIEMU na ambayo yamekuwa yakiimbwa majukwaani kila siku ni Utulivu na Amani.

Utulivu na Amani ni sera ya chama fulani au ni Matokeo ya kila kitu ndani ya nchi?

Kifupi ni kwamba SISIEMU hawana Sera, kwa hiyo huku kulilia sana kwamba vyama vya upinzani havina sera ni kuficha Donda Ndugu waligangalo kwa miaka mingi sasa.

SISIEMU wana Viraka vya mawazo ya hapa na pale vilivyojengwa juu ya siasa potofu ya kujenga ujamaa kwa mtindo wa ubepari; Siasa ambayo hata wao wenyewe SISIEMU wanakiri kwamba haitekelezeki ila wameiweka kwa vile hawana kingine wakijuacho.

Kwa lugha nyingine ni kwamba ukitoa maelezo yote ambayo SISIEMU wanadai ni sera na kuweka maelelezo tofauti yasiyo na uhusiano na siasa,kwa mfano maelezo yenye kuelezea namna ya kupika Pombe ya Kindi au Komoni, bado SISIEMU wataendelea na kazi zao za kila siku.Kwa sababu kitu wakiitacho sera katika maandishi na utekelezaji wa sera kivitendo ni vitu viwili visivyo na uhusiano.
 
Madela wa Madilu

Nashukuru sana.

Kwa kweli hoja zako nzito zinaelimisha lakini pia zinaburudisha. Ubarikiwe.

Niliwahi kuchangia mahali. Suala la UVCCM kulalamikia kwamba kiti maalumu cha hayati Amina Chifupa kipewe kijana, kama ingekuwa ni malalamiko ndani ya upinzani basi magazeti yangeandika 'mgogoro mkubwa' chama so and so. Lakini kwa SISIEMU(naomba niazime kwa muda hii trademark yako) utaitwa tu ni malalamiko. Lakini kubwa zaidi, kwa kuwa upinzani hauna dola na vijazawadi- mjadala unakuwa wa hoja, na haufunikwi kirahisi rahisi kwa vitisho na ahadi. Ni ishara ya demokrasia. Lakini kadiri mijadala kama hiyo iendeleavyo, ndivyo wengine hupuliza matarumbeta pembeni kwamba kuna 'mgogoro' bila kujua undani wa yanayoendelea. Lakini kubwa zaidi, kwa vijana wa UVCCM ilikuwa rahisi mjadala kunyamazishwa kutokana na 'nidhamu ya woga'. Kwa ujumla, baada ya vikao kufikia maamuzi ya pamoja baada ya mjadala na kukubaliana. Walewale wanaoanzisha hoja ya kuwepo kwa 'mgogoro' ndio wanaokuwa wakwanza kukimbia kutangaza 'bahati yao, bado kidogo wangevunjika'. Hizi siasa za 'hide and seek' hazina maana yoyote kwa demokrasia na maendeleo nchini. Mafukuto yaliyomo ndani ya SISIEMU kama isingekuwa dhibiti ya dola, na wahusika wengi wa mafukuto hayo kuwa na 'skeletons' kwenye makabati yao ambazo wanahofia zisimwagwe hadharani, hakika tungeona mambo tofauti. "The latent heat of fusion"! Lakini kwa upinzani, leaders are not robbed off their free will to think! CHADEMA kama taasisi, is a going concern.

Tuendelee na mjadala wa kuziba ombwe la kidira, kisera na kimwelekeo lililoachwa na SISIEMU. Je, serikali mpya ya 2010 iongozwoje?

JJ
 
Sera/Dira ni maneno ambayo siku zote yataishia kwenye ku-generalize issues ambazo CCM are very good at.

Tunataka chama mbadala 2010 watuelezee specifically matatizo tuliyonayo watayatatua vipi na kwa kutumia resources zipi.
 
Kithuku

Asante sana kwa hoja zako nzito.

Kama nimekuelewa vizuri, dira/ujumbe wa ukombozi unaopendekeza wewe ni: "kujenga mfumo mbadala wenye viongozi bora katika ngazi zote"

Nashukuru. Bado naendelea kusibiria michango ya wote. Hatimaye baada ya siku kadhaa nitaweka hizi hoja zote pamoja kupata 'dira/ajenda/ujumbe' unaopeswa kubebwa na chama au vyama mbadala vinavyolenga kuomba ridhaa ya wananchi kuongoza dola mwaka 2010.

Tuendelee na mjadala mpaka kielewe

JJ

Mukhtasari mzuri. Hicho haswa ndicho nilichomaanisha.
 
Mnyika mara nyingi nazikubali hoja zako mkuu,lakini ni lazima ukumbuke ya kuwa mijadala mirefu haitusaidii sana ktk nchi hii katika kuleta mabadiliko.Tuna ugonjwa wa kusahausahau wapi tumeanzia na sasa tuko wapi tuwapo katika mijadala hiyo hasa kunapokuwepo na uvurugaji wa makusudi toka kwa watawala.Mabadiliko thabiti yanataka nia na mkakati wa kimapambano kama wenzetu wa Kenya walivyojipanga na sasa wao wananchi ndio wenye mamlaka na sio watawala.
JM,sikatai, mijadala ni kama chachu ya harakati mbalimbali lakini hayo tusubiri 2010 ili tufanye yale ambayo watawala wetu hawayategemei (kuwang`oa)kisha tuanze hiyo mijadala kwa manufaa ya nchi yetu.
Kumbuka baada ya Zitto kusimamishwa Bungeni,hakukuwa na mijadala ila ujumbe ulienezwa kwa waTZ kwa style ya kimbunga jangwani na madhara iliyopata CCM waulize Mawaziri na Wabunge watakueleza.
Muhimu watu wahamasishwe kuchukia tawala fisadi na Kitaeleweka tuu.

Chakaza,

Wakati tunagombea Uhuru, harakati zilanza kwa muda mrefu. Kulikuwa na majadiliano, vikao, mikutano na mpaka mikakati. Kadiri safari ya kuelekea Uhuru ilivyokuwa inapamba moto, mawazo na tathmini ziligeuka kwa kuboreka na hata kasi kuongezeka au kupunguzika.

Mtoto huzaliwa baada ya yai na mbegu kuungana na hutumia miezi tisa, ndipo mtoto (mtu) huzaliwa. Mimea hupandwa kwanza katika ardhi kama mbegu, nayo huchipua, hupewa mbolea, maji na madawa kukinga maradhi. Aidha hupaliliwa kuondoa magugu na kulelewa ili zao/tunda bora litokee.

Kwangi mimi, nia yangu si kuing'oa CCM tu na utawala wake, bali ni kujenga Taifa ambalo litabadilisha mtazamo wake si kwa ajili ya Uchaguzi au Chama, bali ni kwa manufaa ya kila Raia wa Tanzania. Safari ya kushinda Ujinga, Umasikini na Maradhi, ni ndefu na mabadiliko ya Wanasiasa pekee hayatoshi.

Kwanza Raia ni LAZIMA wajue haki yao Kikatiba na kujua kuwa ni KATIBA ya nchi ndiyo itakayo toa muongozo thabiti wa Siasa Safi na Uongozi Bora ili kuhakikisha kuwa maendeleo ya Wananchi ni ya kweli na ni kwa faida yao na si kwa faida ya kikundi fulani au Chama.

Hivyo, kusubiri siku ya Uchaguzi kuzungumzia mambo ya msingi ambayo ni ya kila siku na ni ya lazima kwa mwananchi, ni kupotoka na upofu usioponeka.

Tumepanda mbegu ya mawazo, tunaingia katika kuangalia utendaji na utekelezwaji sambamba na kutathmini mawazo na mienendo ya utendaji ili kuweza kuwa na zao lililo nono na bora!
 
Lakini baadhi ya matukio ya hivi karibuni ndani ya chama hicho yameniacha nikiwa na wasiwasi kuwa kama hatua madhubuti hazitachuliwa basi kinaweza kujikuta kinaparaganyika kama NCCR ya Mrema na Marando,et al.

Calling a spade a spade,kama CHADEMA haitoweza kumdhibiti Wangwe basi lolote linaweza kutokea.Uongozi ni pamoja na nidhamu na sio kuropoka kila ovyo.Nimesoma katika gazeti flani ambapo Bw Mnyika umetetea uhuru wa kukosoana hata hadharani,lakini mnafanya hivyo kwa manufaa ya nani?Kama unafikiri kukosoana hadharani ni suala jema,then mna umuhimu gani wa kuwa na vikao vya chama?Pamoja na ufisadi na ubabaishaji wake uliobobea,CCM ina sifa moja kuu ya nidhamu miongoni mwa viongozi wake.Whether nidhamu hiyo ni ya lazima (udikteta) au ni ridhaa ya viongozi,la muhimu hapa ni kwamba viongozi wasio na nidhamu miongoni mwao watawezaje kuonyesha nidhamu ya kuongoza nchi pindi wakikabidhiwa jukumu hilo?

Unfortunately,in the past few weeks CHADEMA imekuwa ikisikika zaidi kwa kinachodaiwa kuwa ni clash of interests miongoni mwa viongozi wake wakuu.Tatizo hapo ni ubinafsi,na kama sote tunavyofahamu,ubinafsi unaweza kuzaa lolote lile including ufisadi.

Sikubaliani na Zitto kwa kauli yake kuwa uchumi unakua,na naafikiana na Wangwe kumpinga katika hilo.Lakini ilihitajika busara katika kupingana huko,just like K alivyowapinga akina Sitta,Mudhihir,Karamagi,nk katika uamuzi wao wa kitoto wa kumfungia Kabwe.

Wangwe alikuwa na kila fursa ya kumpinga Zitto kwenye vikao vya ndani vya CHADEMA lakini sio kwenye media.

Mlalahoi,

Pamoja na kukubaliana kimsingi na hoja yako, lakini naomba nipingane nawe katika haya machache niliyokunukuu.

Mwanzoni hata mimi nilikuwa katika kulaani kuchafuana hadharani. Lakini naungana na Mnyika na kusema kuwa kilichotokea kati ya Wangwe na Zitto, ni kuwepo kwa UHURU wa wanachama wa chama kimoja kukosoana hata hadharani na kutuachia Wananchi uamuzi kung'amua ni yupi anayetufaa.

CCM alimkasirikia Butiku na barua yake si kwa sababu eti ni kukosa adabu au kutofuata vikao, bali ni kutokana na ile tabia iliyojengeka miaka nenda rudi ya Usiri na Vitisho ambavyo vilitumika kufunika na kuzika Uhuru wa Mawazo na Maoni na kuondoa Demokrasia.

Mtamkasiikia Wangwe kwa kuhamaki na wengine mnamhoji eti kama yeye ni msemaji wa Chama. Wangwe ni mkubwa kicheo na alichokifokea yeye ni kule kuendelea kukosekana kwa kutumia Busara kunakofanywa na Zitto kwa kuendelea kutumika kama chombo cha kumsifu Kikwete na uongozi wake. Matamshi ya Zitto (pamoja na kujitetea hapa kuwa yeye ni mchumi) kisiasa ni matamshi na maneno ya kikuwadi. Kitila kalizunumzia vizuri na kumuasa Zitto.

Kuwepo kwa tofauti katika nyumba ni jambo la kawaida. Katika Siasa, Chadema inawezekana ikawa Chama pekee ambacho misuguano kama hii inawezekana ikakijenga Chama kwa Wanachama wake kuona kuwa wana uwezo wa kupingana na uongozi hadharani bila kuwa na woga wa kuchukuliwa "hatua za kichama"

Kama mafahali hawa wawili Zitto na Wangwe ndio wanapigana mieleka, basi nasi tutafuatilia na kutathmini mieleka hiyo na kubaini ni nani kati yao ni bora kwa chama.

Hadi sasa hivi hapa JF tuna mitazamo ifuatayo kuhusiana na hawa mafahali;-

  • Wangwe anaonekana ana hasira na anahamaki hovyo mpaka kutoa maneno yanayoashiria kuwa Chadema hakimhitaji Zitto kufanikiwa. Wengine wanona kuwa alichofanya ni sahihi kuzuia kuendelea kwa Wananchi kufikiri kuwa Chadema kina afikiana na Kikwete.
  • Zitto anaonekana ni msaliti, aliyejaa kiburi mpaka kuitwa haambiliki. Wengine wanaona kuwa ni shupavu na msomi aliyebobea.
Hivyo basi, nasi kama Taifa na wale ambao ni wanachama wa Chadema, wana haki kuonoa mambo haya kwa ukweli na si kwa usiri wa vikao vya chama hata kama misuguano hii ita "hatarisha" sura ya chama. Mwisho wake, mchele utatengana na pumba.
 
Wakuu heshima mbele, siuelewi vizuri huu mjadala, lakini ninauliza hivi, Kabwe na Wangwe, wanapopigiana makelele kwenye media za Rostam, tutegemee wataandika nini kwenye magazeti yao?

I mean ninaziona hoja nyingi sana hapa za kuhamasisha na kuamsha muamko wa wananchi kuhusiana na haki zao kikatiba, hilo ndilo hasa tatizo la taifa letu, lakini kusema eti CCM nayo pia ina matatizo ya ndani, I am not sure kama inapaswa kuwa an ishu kwa taifa at large, kwa sababu at the end of the day, CCM wameshaonyesha kuwa wanaweza kutatua tatizo lolote ndani yao iwapo tatizo hilo litaonekana kujaribu kuwaweka out of place na power,

Ndio maana Lowassa hakupewa umakamu, Rostam akanyimwa ujumbe wa NEC na kuweka hazina, Kingunge, akanyimwa ujumbe wa cc, mtandao wakanyimwa ujumbe wa NEC, mbunge wa zamani Nyimbo akafukuzwa chama CCM, yote haya ni katika ku-eliminate anything a threat to their hold of power, ndio maana magazeti hayawezi kupiga sana kelele maana ni mazoea haya ndani ya CCM, tatizo ni kwamba Mrema ameweka a very bad taste na mifarakano ya upinzani, magazeti yanakuwa mstari wa mbele kuwapigia kelele Chadema kwa sababu haijawahi kutokea migogoro huko upinzani bila kumeguka kwa chama, na sasa kwa sababu wanaona Wangwe na Zitto, wanapigizana makelele kwenye media ndio mana yanashabikia sana, yakiwa na goals mbili muhimu, kwanza ni agenda za watu flani, pili ni kuuuza magazeti, ambayo ni hoja ya msingi, magazeti hayawezi kuuzwa kwa nice nice stories,

Cha muhimu ni wananchi kujua haki zao kisheria, kwamba sio lazima waipigie kura CCM, lakini lazima wapewe sababu muhimu na upinzani ili wawapigie kura, haya sio makosa ya CCM ni yetu sisi wananchi na vyama vyetu vya upinzani.
 
Mnyika,

Samahani sana nimechukua muda kujibu hizo hoja mbili hapo juu na si kuchangia hoja kuu. Sikuwa na dhamira kuleta suala la Zitto na Wangwe humu ndani bali ni kubainisha kama ulivyozungumza tena kuwa ni sualal la kuwepo Demokrasia ya Kweli na si Vitisho.

Nikirudi kwenye hoja, kuna vitu kadaa ambavyo kwa maoni yangu mimi, ndio mihimili mikuu ya Maendeleo ya Mtanzania.

Kwanza ni lile tamko la "ili tuendelee tunahitaji Watu, Ardhi, Siasa safi na Uongozi bora" na la pili ni mfumo wa Ujamaa na Kujitegemea (ambao ulitumika kama siasa) mihimili hii ni sehemu kuu ya Azimio la Arusha.

Hivi ndivyo vya msingi, vinavyofuatilia ni Azimio la Musoma, Iringa, UPE, Maji Vijijini, Kilimo cha Kufa na Kupona na kadhalika.

Watu tunao, Ardhi tunayo, tunachogotagota ni Siasa Safi na tulipoboronga ni Uongozi Bora!

Nikinukuu na kurejea maneno ya Mwalimu Nyerere alipohojiwa na shirika la habari Marekani PBS kuhusiana na Azimio la Arusha mwaka 1996 na hotuba kadhaa alizozitoa baada ya kustaafu, Maazimio yote na misingi niliyoitaja hapo juu (kwa rangi nyekundu) kilichosababisha kuanguka kwake si kuwa ni sera mbovu, bali ni ukosefu wa utendaji makini (uongozi bora) kwa manufaa ya Taifa ama kwa uzembe wa makusudi au ufinyu wa upeo wa utendaji na ufuatiliaji.

Ukimsoma Mzee Mapesa katika hoja yake Bungeni November 4 2004 http://www.parliament.go.tz/bunge/ContrLst.asp?Menu=Contr&PTerm=2000-2005&vpkey=1247&page=2
utaona kwa dhati ni nini anachoashiria kuhusiana na Azimio na kipaumbele. Kwa matamshi ya Mzee Mapesa, ni utekelezaji na prioritization ndio kilichohitajika.

Nimetaja Siasa Safi na Uongozi Bora. Watanzania mahali tulipo, tumefikia kiwango kuwa tunataka viongozi wetu wawe ni malaika (pure with no imperfections), hili ni suala la kusadikika (UTOPIA) abalo haliishiii kwa viongozi tuu, bali hata katika nadharia ya Sera au Mfumo wa Jamii yetu (Puritans/Perfect).

Uongozi Bora hauna maana kuwa leo tutakuwa na Rais, Mawaziri, Wabunge, Majaji, Mapolisi au Watendaji wengine wote ambao ni sawa na Malaika Gabrieli au Mikaeli. Sisi ni binadamu na tumezaliwa na udhaifu. Hata Mwalimu Nyerere alikuwa na udhaifu wake na alifanya makosa (msicalculation) ambayo tunaendelea kuyapigia kelele badala ya kusawazisha.

Tunachohitaji katika Uongozi ni Viongozi ambao kwanza watashika yamini kulitumikia Taifa na Wananchi, watakuwa watiifu wa Sheria na Katiba, wenye kufuata na kutafuta Haki, walio tayari Kukosolewa, kukubali Makosa, wepesi Kujirudi na kuwa Wakweli kwa Taifa na zaidi kwa nasfi zao. Pili, viongozi hawa watakuwa ni wenye kujituma na kuwa mfano katika utendaji kazi, ufuatiliaji na hata kuwa na sera ambazo ni za lengo la kutimiza matakwa ya Wananchi na Taifa. Wawe viongozi hodari wa kazi na si maneno, shupavu na wazalendo wa kuigwa na jamii zao na Taifa kwa ujumla. Wawe na Juhudi na Maarifa ya kufanya kazi zao, kuendesha nchi na kupanga sera ambazo zitamshirikisha kila mwananchi na kwa faida ya Nchi na Wananchi wake.

Kama tukipata japo 50% ya watendaji wa Serikali na nchi (Bunge, Mahakama, Serikali Kuu, , Mashirika, Sekta Binafsi) ambao ni wa viwango vya uongozi bora kama nilivyotaja hapo juu, basi kazi ya kutekeleza maazimio yote na kufanikisha Siasa Safi yatakuwa yanakwenda kwa mwendo wa kuridhisha.

Usomi ni nafasi ya kupanuka mawazo kwa kujifunza ki-imla mambo tofauti. Elimu pamoja na kuwa ni nywele, si kigezo pekee kuwa mwenye elimu kubwa ndiye anayefaa kuwa kiongozi. Je ana sifa nilizozitaja hapo juu? au ni kichwa kilichojazwa mambo mengi lakini hakina uwezo wa kupembua na kutenda?

Azma ya kuleta maendeleo ya kweli kwa Taifa sasa hivi itatokana na Uongozi Bora, ni wajibu wetu kutafuta viongozi bora (wabunge, wawakilishi nk) ambao tutawaamini kama Taifa kuwa hawa wanaweza ufanikisha utekelezwaji wa Siasa safi ambazo zitamsaidia Mtanzania kuishi kwa Ujamaa (umoja) kujenga msingi imara wa Kujitegemea na hivyo kufanikisha Vita vya Ujinga, Umasikini na Maradhi ili kukuza Ustawi wa Jamii.

Suala hili si la CCM, Chadema au CUF na TLP, ni suala la Taifa. Aidha misingi niliyoiweka hapo juu Ujamaa, Kujitegemea, Maazimio na Ili Tuendelee, si mali ya chama kimoja, ni mali ya Taifa kwa Faida ya Taifa.

Swali ni kiongozi gani au chama gani kitakuwa tayari kuifanya kazi hii kwa faida ya Taifa na Wananchi wake?
 
Back
Top Bottom