Dhana ya ukeketaji

badshah

Member
Mar 16, 2013
51
32
DHANA YA UKEKETAJI
Ni moja ya tatizo sugu sana linalowakabili wanawake katika jamii nyingi. Imekadiriwa ulimwengu mzima kuwa wanawake takriban milioni 120 wamekumbwa na tatizo hili. Wanaounga mkono ukeketaji husema kuwa ni sehemu muhimu sana katika maisha ya kiutamaduni na kidini, na wengine hulinganisha na ile hali ya kutahiriwa mwanaume ambayo haipingwi hata kidogo na ni halali. Lakini wale wanaopinga dhana ya ukeketaji husema kwamba, sio tu kwamba ukeketaji hutishia maisha ya wanawake, bali pia ni moja ya njia za unyanyasaji wa wanawake. Katika baadhi ya nchi ambazo ukeketaji hufanyika sana utakuta ni kinyume na sheria – wale wanaong’ang’ania kufanya uchafu huu katika nchi hizo sasa wanaweza kushitakiwa na kufungwa, lakini bado hufanyika kimya kimya ndani ya familia na mbali na macho ya vyombo vya sheria. Ukeketaji hufanyika sehemu kubwa magharibi na kusini mwa Asia, Afrika ya kati na Mashariki na sehemu nyingi za Afrika. Pia huonekana kufanyika baina ya wahamiaji katika nchi ya USA, Canada, France, Australia and Britain, mahali ambapo ni kinyume na sheria. Kwa ujumla imekadiriwa kuwa zaidi ya wasichana milioni 2 hukeketwa ndani ya mwaka mmoja. Kuna aina mbili kuu za ukeketaji.
  1. Uondoaji wa ncha ya kisimi (The removal of the tip of the clitoris)
  2. Uondoaji wa Kisimi(clitoris) na Labia na ushonaji wa uke, kwa kuacha njia ndogo tu ya mkojo na damu ya hedhi. Mchakato huu hujulikana kama ufyataji (hali ya kufunga uke kwa bizimu/kushona kuzuia kujamiiana.) – Infibulation.
Hakuna faida yoyote ile ya kiafya isipokuwa ni madhara Ukeketaji hauna faida za kiafya hata kidogo, na inawaathiri wanawake na wasichana katika njia nyingi sana. Inahusisha kuondoa na kuharibu sehemu na tezi muhimu katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na kuzuia utendaji kazi wa asili wa mwili. Huweza kumsababishia maumivu makali, homa, mshtuko, uvujaji wa damu, ugonjwa wa pepopunda (tetanus), kufunga njia ya mkojo. Pia humondolea hamu yakufanya tendo la ndoa. Madhara ya muda mrefu ni kama yafuatayo:
  1. Maradhi ya mara kwa mara ya kibofu na njia za mkojo
  2. Uvimbe katika kibofu
  3. Ugumba
  4. Matatizo katika kujifungua hasa kumuua mtoto anayezaliwa kulingana na njia kubanwa na mishono ya ukeketwaji.
Ikiwa elimu ya hili itawafikia wahusika wa kazi hizi, na hatua kali za kisheria kuchukiliwa ipasavyo dhidi ya wanaounga mkono pamoja na kutenda, basi ukeketaji unaweza kumalizika kwa haraka kabisa.

KWA MAKALA TOFAUTI TEMBELEA: Staryte - Education, Entertainment & Development - Elimu, Burudani na Maendeleo

Kukeketwa ni kweli ni jambo la aibu na kufedheheshwa kwa wanawake. Ila sabubu zinazotolewa hazikidhi kuelimisha jamii ubaya wake. Wanawake wengi wa kabla ya 1970 walikeketwa na madhara yake hatujui. Kama ni kujifungua walijifungua salama na tena majumbani mwao. Waliweza kupata watoto hadi wengine kufikia 11. Swala la kujamiana waliweza ishi ndani ya ndoa zao kwa raha zote na heshima kubwa.
Wateteaji wa haki waende ndani zaidi kulimisha jamii madhara yatokanayo na ukeketaji.
 
Swala zima la ukeketaji wanawake ni mitazamo potofu ambayo ilikuwepo kwenye jamii nyingi za Kiafrika ambazo zinajaribiwa kurekebishwa. Mambo haya yalifanyika wakati huo ambapo waliofanya unyama huo dhidi ya wanawake walifikiri kuwa wanawasaidia hao kina mama "kutunza heshima" ya kutofanya ngono ovyo ovyo. Pamoja na kuwa na campaign zenye msukumo mkubwa katika jamii yetu bado kuna wachache wanaoendeleza hii dhana potofu.
 
Kukeketwa ni kweli ni jambo la aibu na kufedheheshwa kwa wanawake. Ila sabubu zinazotolewa hazikidhi kuelimisha jamii ubaya wake. Wanawake wengi wa kabla ya 1970 walikeketwa na madhara yake hatujui. Kama ni kujifungua walijifungua salama na tena majumbani mwao. Waliweza kupata watoto hadi wengine kufikia 11. Swala la kujamiana waliweza ishi ndani ya ndoa zao kwa raha zote na heshima kubwa.
Wateteaji wa haki waende ndani zaidi kulimisha jamii madhara yatokanayo na ukeketaji.
Unauhakika gani kama waliishi kwa raha zote,mwanamke wa miaka hiyo hata kama alikuwa anapata tabu alikuwa hana uhuru wa kujieleza kama ilivyo miaka ya sasa,go google uangalie umbile la Vagina,including labia majora,labia minora na clitoris utagundua kuwa kuviondoa kunawasababishia kukosa raha ambayo angeipata kama angekua navyo kwani vimeumbwa in such a way that ile kitu inapoingia kuna mgongano wa moja kwa moja ambao ndio unaowaletea raha wakati wa kujamiiana.
 
Kukeketwa ni kweli ni jambo la aibu na kufedheheshwa kwa wanawake. Ila sabubu zinazotolewa hazikidhi kuelimisha jamii ubaya wake. Wanawake wengi wa kabla ya 1970 walikeketwa na madhara yake hatujui. Kama ni kujifungua walijifungua salama na tena majumbani mwao. Waliweza kupata watoto hadi wengine kufikia 11. Swala la kujamiana waliweza ishi ndani ya ndoa zao kwa raha zote na heshima kubwa.
Wateteaji wa haki waende ndani zaidi kulimisha jamii madhara yatokanayo na ukeketaji.

YOU ARE RIGHT!!!!! nakuunga mikono mpaka miguu...
 
Back
Top Bottom