Dhambi ya kuutelekeza ujamaa ndio,inaitesa nchi yetu ya tanzania!

MKWECHE

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
299
64
ANDIKO LA MWA-MKWECHE!
Jamani Ujamaa Umejengwa na Msingi wa Kuheshimu UTU wa Binadamu!
Kwa wale wanaosoma biblia Kuna Neno linasema Amri kubwa Kuliko zote ni UPENDO!
Waasisi wa Taifa hili walipigania sana ujamaa HASA MISINGI yake kwa ajili ya Kupenyeza kwenye akili zatu.Dhana ya Kuheshimu UTU Uwa Mtu ndio inatuelekeza kwenda kwenye USAWA WA BINADAMU na ndani ya USAWA huo UNAMWEKA binadamu mwenzako wa Kwanza alafu wewe mwenyewe unafuata!
Misingi ya UJAMAA ndio Silaha ya Uzalendo!Kiwa MZALENDO utakumbuka kwamba cheo au nafasi uliyonayo siyo ya kuponda raha bali ni ya kuwatumikia wananchi waliokuamini na Kulinda rasilimali zote za nchi ambazo tumazirithi kutoka kwa Mababu zetu!
Mkweche Sililii SIASA ya UJAMAA bali Nashupalia MISINGI YA UJAMAA!Asili yetu sisi watanzania ni ujamaa wa toka enzi na enzi!Tunapojaribu Kuuchepuka na Kuiga Ubepari Uchwara Ambao si Asili yetu Matokeo yake ndio Haya Yanayotutesa!
Misingi ya Ujamaa ndio Ingetuwezesha kuwa na Uchumi Imara!Leo hii Tanzania Imekalia Uchumi!Rasilimali zimejaa lakini tunashindwa kuzigawa kwa Kuzingatia Misingi ya Ujamaa!Ukikwepa misingi ya Ujamaa Unakosa Uzalendo na unapata Ugonjwa wa Upungufu wa Uzalendo kwenye bongo.
Ubongo Ukikosa Uzalendo Unajaa UBINAFSI!Ukishakuwa Mbinafsi Unakuwa MWONGO!UONGO Huo ni wa Kuwahadaa Wenye nchi(Watanzania) Ili wewe Upate Utajiri kwa njia ya Mishahara Minono,marupurupu,mikataba ambayo Nchi na Mwananchi(Mwenye Mali) Hafaidiki!
Nje ya Misingi ya Ujamaa Mambo haya hujitokeza:
1)Uchumi wa takwimu ambaza hazishabihiani na Hali halisi za maisha ya wananchi
2)Huduma za Kijamii Kudorora(elimu,Afya nk)
3)Mgawanyo wa fedha bajeti kuelekezwa kwenye matumizi ya Anasa
4)Anasa kuonekana Ndio Hadhi ya Kiongozi,Msomi na Mwenyenazo
5)Tofauti ya Kipato kati ya Mwenye nacho na asienacho!Na mwenyenacho kutaka Zaidi yeye bila kumjali
6)Ubinfsi na Migomo,migomo yetu leo imejengwa kwenye misingi ya Ubifsi zaidi!Mfano huu wa Madaktari,siku za nyuma
nilisikia Madakitari Walitoka na kukataa kikao kilichojumuisha na kada zingine za sekta ya Afya!Ati madai yao yajitegemee!UBINAFSI MTUPU!Hospitali yoyote Dunia haiendi bila ya Combination ya Madaktari na Kada zingine za Afya!Ukiona Makundi haya ndani ya Hospitali kila mtu anajipigania Jua Ubinafi Umewekwa mbele
7)Siasa kuwa na Kipato Kikubwa Kuliko wataalamu,matokeo wataalamu wanakimbia Maofisini kwenda kwenye kupiga siasa.Mwanasiasa Mshahara wa nini!wakati wataalamu wapo ngazi zote
8)Tofauti kubwa Mishahara ya watumishi wa UMMA(Uwiano hauzingatiwi matokeo na lawama)
9)Ahadi ziizotekelezeka na Kupimika
10)Kutoheshimu sheria za nchi
11)Ulegevu ktk kusimamia sheria na Haki za watu
12)Kila Jukumu la Kutatua matatizo kuonekana ni la viongozi na serikali
13)Kusemea wengine(Kila mtu kujinasibu anapigania watanzania na wamemtuma)
14)Kutohamisisha wananchi kuchangamkia Fursa zilizopo!(NHIF,CHF,Sasa Kujiunga na Mifuko ya Akiba za Uzeeni hata kwa watu waiojiari!
15)Kudhibiti mauzo ya mazao ya wakulima!Madalili wanafaidi wakulima wana MASKINIKA
16)Usimamizi wa Ruzuku za Pembejeo kuwa hafifu!WAKALA AFAIDI(Ubinafisi) Mkulima Ana maskinika!
17)Bohari la Madawa Kushindwa Kusambaza madawa wakati Budget yote ya Dawa ya Serikali inatumbukizwa humo!kwanini hela yao haizunguki!
18)Kodi Anatozwa zaidi Mlaji badala ya Tajiri Mwenye Kampuni
19)Vivutio Kibao kwa wawekezaji hata kwa Malighafi Ambazo zinapatikana Tanzania!(AJABU YA TANZANIA)
20)Vyanzo vya Umeme lukuki lakini Umeme Hakuna!Makaa ya Mawe chungu nzima,Upepo wa kutosha,gesi na Sasa Uranium!wote huu ni Urithi wa nchi!
21)Reli imejengwa na wajerumani sisi Tunaitelekeza
22)Bandari tegemeo la nchi zaidi ya 8 lakini inasuasua
23)Ardhi Kubwa na Mabonde Lukuki lakina Tunanunua chakula toka nje
24)Wasomi kibao na wamekua wapiga siasa
25)Mbunge unamtegea anategea apiganie sheria na kukutetea yeye Mwenyewe hata Dereva Wake anamkandamiza!
kama anemwendesha na kulinda uhai wake amjali je wewe asie kijua inakuwaje!

Atakae ona Mkweche kapotea,Shauri yake!Atakae sema mkweche anapewa posho, pole yake,kwasababu haumjui mkweche kwamba ni "MGAYA SIDA"(kwa Tafsiri uliza Mnyalukolo)
MWISHO:
Maneno matupu hayatajenga nchi Yetu,Madakitari Rudini Kazini sisi watanzania ndio waajiri wetu na wazazi wanu tulio wasomesha,Wanasiasa Misingi ya Ujamaa ni Jibu,wafanyakazi waliotuajiri ni watanzania tuwatumikie na kulinda Rasilimali zao!
HAKUNA MADAI MAKUBWA YANAYOKUBALIKA KUDAIWA KWA GHARAMA YA UHAI!Madai yanalipika ila UHAI UKITOKA NIPENGO KWA FAMILIA NA TAIFA!
TANZANIA NI YETU SOTE NA TUILINDE KWA AJILI YA HESHIMA YA WALIO TUACHIA NA KWA MUNUFAA SISI,WANETU NA VIZAZI VIJAVYO!
Msemo wa Mh.Nasari unaihamasishaga sana TUMEANZA NA MUNGU TUMALIZE NA MUNGU!
MKWECHE NASEMA "TANZANIA TUMEPEWA NA MUNGU,TUUENZI MPANGO WA MUNGU"
Mkweche mambo ya SIASA siyajui!Na siamini katika vyama!bala nchi ni watu na maslahi ya nchi na dhamana zake ni za wananchi!
 
Back
Top Bottom