Dereva wa maisha bora kashindwa kutufikisha: Huyu wa matumaini ataweza?

Chademakwanza

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
6,346
1,871
Dereva wa safari ya matumaini atakuwa hana leseni au hana uhakika na chombo chake. Dereva huyu hana tofauti na yule aliyetuendesha kwenye basi la maisha bora kwa kila Mtanzania.

Kumbe alikuwa haijui njia akawa anapuyanga tu porini na kuliharibu basi kwenye visiki vya EPA, Radar na magogo makubwa kama Richmond na Dowans. Wenzetu wamekatika miguu, viuno na wengine hata uhai wakapoteza.

Dereva alitudanganya hivihivi mara ya pili kwamba sasa amepata uzoefu na njia amekwisha isavei na ameielewa sasa ana ari zaidi, kasi na nguvu ya ajabu. Tukamkubalia tena tukapanda basi lake likiwa bovubovu ila hatukujali tulivutiwa sana na utamu wa kauli zake.

Mama yangu, mara hii ndo katumaliza kabisa kumbe bado jamaa ni learner sasa katutumbukiza kwenye mto mrefu wa Escrow, sasa tunaangamia huku tunajiona.

Mtoni hali ni mbaya kuna ambao vichwa vimetenganishwa na viwiliwili na ambao bado tunapumua bado hatuna nafuu humu kuna wanyama wakali na majoka ya ukubwa wa ajabu kuna sauti za mizuka na mizimu yote haya yanatamani damu zetu.

Sasa hali ni mbaya maradufu; hospitali hakuna madawa na madaktari hawana pesa, wamegoma. Wanafunzi huko vyuoni hali ni ngumu eti wengine wanajaribu kujiuza na wakuwanunua hawapo.

Walimu walishajikatia tamaa siku nyingi sana hafundishi anasubiri saa nne awauzie wanafunzi wake ubuyu na viazi vya kuchoma, atafanyaje mshahara mdogo unakata siku tatu baada ya kuupokea.

Polisi na raia sasa wanaviziana, polisi akikutwa amezubaa anauawa, na raia akijiingiza ndani ya kumi na nane za polisi lazima amkutanishe na mtoa roho fasta.

Wakulima nao wanakopwa na serikali mazao yao mwaka wa tatu bado wanadai. Kila kitu ni kinyume nyume badala ya serikali kuwakopesha wakulima sasa wao ndo wanaidai serikali, makubwa haya.

Hata huyu hakimu ambaye nilikuwa namtegemea kupata haki yangu jana tu aliniambia hakuna cha bure tena hata haki yangu ananiuzia kama sina dau la kutosha basi anamuuzia adui yangu kama atanipiku dau.

Jamani mliopo nchi kavu njooni mtusaidie huku dereva wetu hakuwa anaijua njia sasa anatuangamiza

Ila hatutaki tena dereva wa matumaini, aje wa uhakika ili atuvushe salama. Au abiria wenzangu wahanga wa safari ya maisha bora kuna mmoja wetu bado anatamani safari ya matumaini?

Jibuni haraka kabla madereva hawajafika ili tukubaliane dereva wa kuondoka naye.
 
Dereva wa uhakika hatutaki tena dozi ya Matumaini.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Hatutaki maamuzi magumu tunataka maamuzi SAHIHI. Lowassa kamwe hawezi kuwa rais wa nchi hii, labda rais wa manzese....
Namfananisha Lowassa na wanyonya damu (vampires)
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Hatutaki maamuzi magumu tunataka maamuzi SAHIHI. Lowassa kamwe hawezi kuwa rais wa nchi hii, labda rais wa manzese....
Namfananisha Lowassa na wanyonya damu (vampires)
Hatutaki kupiga kura tena kabla ya miaka mitano kuisha.
 
Dereva anaemaliza muda wake aliwekwa na dereva wa matumaini, na ndie alikua dereva msaidizi kabla hajastukiwa nia yake ovu.

Matumaini ni matumaini tu, not necessary yaje kua kweli. Hata watu wanaosemekana kuishi kwa matumaini sio kwamba ndio wamepona kabisa.
 
Sasa tatizo la lowasa ni lipi hapa, aliwachia serikali mwendeshe imewashindeni mnataka kumlaumu, kwa lipi? Hatutaki marais wanaona ulofa ni kitu cha maana na wanataka watu wote tuwe nalofa, hapana. Tunahitaji mtu anaeweza kutuondoa kwenye huu umasikini na anayeweza kutuonyesha namna ya kuondokana na ulofa kwa yeye binafsi kukataa kuwa lofa wala kuitwa lofa. Naye ni lowasa pekee.
 
Dereva wetu gari lilipokwama kwenye visiki kondakta wake aliruka akatuacha. Sasa kondakta anataka kuchukua nafasi ya dereva si itakuwa balaa na kama ujuavyo makondakta wengi hujifunzia udereva juu kwa juu hata sheria za barabarani hawazijui vizuri.Je tutafika kweli safari ya matumaini? Gari hili ni bovu, tairi zimechakaa, gear box choka mbaya, body imechakaa wanatuambia engine bado mpya ya kweli hayo? Kwani hakuna gari jipya? dereva mwingine mwenye taaluma ya kutufikisha huko tuendapo? Mbona kuna lundo la madereva wasio na leseni wanaling'ang'ania hilo gari lililochakaa tena kwa gharama kubwa? Kwanini tusipige simu namba 0800757575 ili hawa madereva washughulikiwe na vyombo husiika vya usalama barabarani kwani uendeshaji wao ni hatima yetu.
 
Hahaha kwel ccm Noma kutoka Maisha Bora mpaka Matumaini how

Only happen in Tz , Omg Nyerere come nd take ur Tanzania

Slogans zao kama maandishi ya kiarabu kutoka kulia kwenda kushoto
 
Back
Top Bottom