Dereva fahamu HAKI na WAJIBU wako unapokutana na Traffic Barabarani kuepusha Migogoro

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,268
Wadau wenye usafiri tuweze shirikishana mambo mbalimbali ambayo madereva wanapaswa kuzingatia barabarani hasa kwa upande wa Haki na Wajibu wao.

Na sisi tusio na magari pia tutapata darsa hapa.maana nakumbuka miaka ile sisi tunasoma tulijifunza kwenye Geography Kilimo cha Mahindi USA lakini hatukuwa wakulima.

Napenda tuweze shirikishana mambo kadhaa hasa Dereva anapokamatwa na Traffic au anapofanya kosa. Kwa wenye uelewa hasa kwa kuzingatia Sheria tuelekezane haya.

1. Dereva anapokuwa hana leseni (amesahau kubeba) sheria inamtaka ai present/wasilishe kwa traffic ndani ya masaa 72. Wakati huo je ataondoka na gari yake au gari itakuwa kituo cha polisi? Mfano umekamatwa kwa kosa au ktk ukaguzi.ukagundua hukubeba leseni. Nini kinafuata?

A. Je unamwachia gari?(unaacha na funguo/au unaondoka nazo)
B. Unaondoka na gari anabaki na namba za gari
C. Gari unaipeleka kituo cha polisi

2. Je ni sahihi mtu kuwasha hazard anaposimama kwenye zebra/alama ya pundamilia ili na wenzie nao wasimame?ni kwa mujibu wa sheria?

3. Je mtu anapovuka kwenye junction ni sahihi kuwasha hazard kuonesha kuwa ananyoosha na haingii kulia wala kushoto?

4. Inapotokea mtu yupo kwenye foleni ya mataa taa ikabadili njano then red akiwa katika mwendo amefika katikati ya barabara tayari.je asimame arudi nyuma au amalize kuvuka. Anapokamatwa na traffic aandikiwe au aonywe?

5. Ni makosa gani ya dereva ambayo akifanya anaweza elimishwa tu na asiandikiwe na anaweza goma kuandikiwa kisheria kabisa bila kuonekana amemkosea traffic

6. Je traffic anaruhusiwa kuchomoa bima ya gari na kuondoka nayo? Kwa sheria ipi?

7. Je traffic anaruhusiwa kuchomoa plate number kuondoka nayo au kuishikilia?kwa sheria ipi?

8. Je traffic anaruhusiwa kuchomoa funguo ya gari kuishikilia?kwa sheria ipi?

9. Je traffic anaruhusiwa kubaki na kadi ya gari ikiwa huna leseni au umegoma kumpa leseni?kwa sheria ipi?

10. Ikiwa traffic kaomba leseni yako akague ukampa akakutafutia kosa ambalo hujaridhika nalo akuandikie.ufanye nini?

11. Je inawezekana traffic akakuandikia kosa bila kutumia leseni?

12. Kama hujaridhika na kuandikiwa kosa na limeshaandikwa ufanye nini?

13. Unaendesha gari imefika jioni unawasha taa. Taa moja imeungua je traffic akuandikie kosa? Ikiwa taa ilikuwa nzima before.

14. Umegongwa ukiwa parking taa imepasuka huna uwezo wa kununua taa muda huo je traffic akikukamata akundikie kosa?

15. Ni kosa lipi ambalo traffic atakuwa ONYO TU au ELIMU na kukuruhusu uondoke pasipo kudai Rushwa au Kutaka kukuandikia kosa.

Na mengine mengi sana... Tuweze kuelimishana itusaidie tunapokuwa barabarani kuepuka migogoro isiyo na faida.

NB. WAPO TRAFFIC WENYE AKILI NZUERI NA WASTAARABU SANA MPAKA UNAJISIKIA VIBAYA KWA KUKOSEA. HAO TUWAHESHIMU SANA
 
2. Je ni sahihi mtu kuwasha double hazard anaposimama kwenye zebra/alama ya pundamilia ili na wenzie nao wasimame?ni kwa mujibu wa sheria?

Si sahihi kuwasha double harzad unaposimama kwenye zebra, unapotaka kunyoosha njia panda au unapovuka reli.
Kuwasha double harzad unamaanisha umepata matatizo kwa hiyo una ruhusu gari zilizo nyuma yako zipite
 
Hili limewahi nitokea nikataka overtake gari nakuta mbele kuna watu wanavuka...ananipigia kelele huoni nimewasha hazard nami nikamwambia kuwasha hazard maana yake gari inashida so sisi wengine tuendelee na issue zetu... Mijitu imeanza tu kuiga hili jambo miaka ya karibuni.sisi kipindi tunaendesha gari miaka ya 90 hili jambo halikuwepo kabisa.

2. Je ni sahihi mtu kuwasha double hazard anaposimama kwenye zebra/alama ya pundamilia ili na wenzie nao wasimame?ni kwa mujibu wa sheria?

Si sahihi kuwasha double harzad unaposimama kwenye zebra, unapotaka kunyoosha njia panda au unapovuka reli.
Kuwasha double harzad unamaanisha umepata matatizo kwa hiyo una ruhusu gari zilizo nyuma yako zipite
 
Double hazard kwenye junction kuonesha unanyoosha ni kuiokosea sheria ya usalama barabarani, matumizi yake ni parking ya dharula tu.

Kwenye junction yenye makutano ya njia nne na wewe uelekeo wako ni mbele, hauwashi chochote, bali kabla ya kuingia kwenye hiyo junction, pepesa macho kulia kuona kama kuna mtu ashaingia usubiri, baada ya hapo kanyaga wese kunyooka mwanawane.
 
Back
Top Bottom