Denis Msaki ni nani Katika siasa za Tanzania?

Na huyu Ludovick wa Jacton Manyerere ambaye amewekwa front page na Lwakatare na gazeti la mwananchi kuonyesha eti ni mwanachadema kwa kuonyesha alama ya vema yenye vidole vilivyobananishwa
 
Sio kila aliye against na udiketa wa viongoz wa cdm ni mamluki, demokrasia ina mambo mengi...
 
Mwana JF

Tusipokuwa macho hawa CCM watatugawa kikabila na tutaanza kupigana,kunyanyapaawatanzania wenzetu na watu kama wakwere ,wazanaki,wandengereko,wamakua nawamwela hawatapata uongozi wa nchi kamwe kwa sababu makabila ni madogo,CCM sasahivi wametengeneza syndicate ya kumdharau Nyerere kumshusha hadhi nakumdhalilisha lakini ukweli kitu alichofanyia nchi yetu kizuri kulikuo yoteilikuwa ni kutuunganisha na kuondoa ukabila ,Je tumuulize Bulembo Kilimanjaroau Moshi ni Chadema peke yao au wako CCM na TLP ,NCCR iliwahi kuwa na wabungekule jamani inadhihirisha sasa kwamba kampeni zao zinafanikiwa Kikwetealipokuwa anapokea ushindi wa mwaka 2010 alisema uchaguzi ulitawaliwa na udiniakalalama kwamba ataumaliza sasa sikiliza alivyofanya

Raisi-Mwislamu
Makamu wa Raisi-Mwislamu
Jaji Mkuu-Mwislamu
Mkuu wa Usalama wa Taifa -Mwislamu
Waziri wa Ulinzi-Mwislamu
Mkuu wa Jeshi la Polisi-Mwislamu
Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu-Mwislamu
Kati ya wakuu wa mikoa -28- 19 waislamu
Matajiri Kumi wa Nchi hii-10 waislamu-1 Mkristo
Asilimia 78 ya wajumbe wa kamati kuu ya wajumbe wa CCM- waislamu
Asilimia 81 ya wajumbe wa tume ya katiba waislamu
Asilimia 66 ya wakuu wa wilaya waislamu
KIkwete ameingiza mfumo Islamu nina wasiwasi anaposema au anapotuma watu wakekusema huwa ameshaamua jambo fulani ameshatutenga kidini sasa atatutengakikabila si mtu mwema hata kidogo kwa mustakabali wa taifa hili kiongozi mzuriangemtuma mtu akanushe maneno ya Bulembo lakini yeye anashabikia kwa sababuanataka kuwanyanyapaa wachaga bila sababu,Nape alisema hivyo hivyo kamaBulembo,Kinana alisema hivyo hivyo kama Bulmbo,Mwigulu alisema hivyo hivyo kamaBulembo Mtoto wa Kikwete yeye ndie aliyeapa kwamba Haitakaa itokee kaskaziniitoe raisi ,Mtanzania mwenzangu tafakari

wakristo wamenyanyapaliwa kwa kweli huyu Kikwete kumbe yeye ndo anayetuletea mambo ya udini hapa nchini..... wengine tunaongea kimaneno yeye amefanya kimatendo...
ndio maana anawaambia waislam wapige kelele mfumo kristo ili tusichunguze huu udini wake...Tumeshatambua aendeleze Mfumo Islam wake... na nyie mnaolalamika mfumo kristo hebu tuhakikishieni hizi habari hapa juu ni za kweli???? hapo hatujaweka UDOM?????
 
Kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo huko nyuma kama miaka miwili hivi gazeti la Mwanahalisi liliweka hadharani habari za huyu jamaa hasa uhusiano wake na Zitto na mawasiliano yao kupitia emails. Sijui ni kweli kiasi gani juu ya yote yaliyosemwa lakini walau binafsi nilimfahamu Msacky kupitia ile stori. Itakumbukwa pia baada ya mawasiliano yake kuwekwa hadharani kwa mtindo ule ulitoumika kuweka habari za Mchange akitoa rushwa kwa MPESA kwenye uchaguzi wa Bavicha, Zitto akiwasiliana na Jack Zoka wa TISS na Ramadhani Inghondu wa TISS, Zitto anadaiwa kulalamika kuingiliwa mawasiliano yake ya siri kwa njia ya emails kwenda kwa Msacky. Naweza kuwa sijakidhi haja yako lakini walau hayo machache ni mazingira ya huyo Msacky kwenye saisa za Tanzania. Haya hayajaanza wakati wa Tido Mhando ni mambo yaliyotokea kipindi kirefu kilichopita

[h=1]Siri za Zitto nje[/h]
picture-4.jpg

Na Saed Kubenea - Imechapwa 09 December 2009

Mawasiliano yake yanaswaAponzwa na mwandishi wa habari


zitto_2.jpg



SIRI kubwa kuhusu mwenendo wa Zitto Kabwe (Mb) ndani ya chama chake zimeanikwa mitaani na zinaweza kumzamisha kisiasa, MwanaHALISI sasa linaweza kuripoti.
Siku nne baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Willibrod Slaa kusema wamenasa taarifa za mawasiliano ya Zitto, baadhi ya taarifa zimepatikana jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Zitto ananukuliwa akiapa kusaidia wagombea uongozi katika vyama vingine; na katika moja ya taarifa ananukuliwa akisema atasaidia David Kafulila kupata ubunge “hata kabla ya akina John Mnyika…”
Mnyika ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA na Kafulila alikuwa Afisa Habari ambaye baada ya kuondolewa wadhifa huo amekimbilia NCCR-Mageuzi. Mnyika anatarajia kugombea ubunge jimbo la Ubungo.
Naye Zitto amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la Jumatatu akilalamika kuwa ameingiliwa katika mawasiliano yake ya baruapepe (e-mail); jambo ambalo Mkurugenzi wa Upelelezi, Robert Manumba, amedakia haraka na kusema Zitto akiwapelekea malalamiko watashughulikia.
Kwa mujibu wa mpangilio wa taarifa husika, lazima aliyezitoa amepata ufunguo wa baruapepe (password) wa ama Zitto au mwandishi wa habari wa Mwananchi, Denis Msacky.
Karibu mawasiliano yote ni kati ya Zitto na Msacky juu ya “ushujaa” wa Zitto na jinsi anavyopendwa nje ya chama huku “akichukiwa” na viongozi wake wakuu.
Katika moja ya mawasiliano, inaonyeshwa kuwa Msacky alimwandikia Zitto akieleza, “Leo hii Mrema (Augustine Lyatonga) anasema anakuheshimu wewe, lakini si Mbowe; hivyo hivyo, Lipumba (Profesa Ibrahim) na James Mbatia wanasema wewe una visheni.”
Katika mawasiliano hayo ya Jumanne, 1 Desemba 2009, saa 6.45 adhuhuri, Msacky anaonyeshwa kumwambia Zitto pia kuwa, “CCM nao…wanakusifu kwamba pamoja na kwamba unawaliza sana, lakini ni kiongozi shupavu.”
“Leo hii siasa za CHADEMA zingekuwa zinatisha kama ungekuwa mwenyekiti wa CHADEMA, vijana nchi nzima wangejiunga na chama, uko nao karibu, unaongea nao, una elimu nzuri, unajua mambo, unasoma sana,” imeeleza sehemu ya mawasiliano kutoka kwa Msacky kwenda kwa Zitto.
Kinacholeta wasiwasi ndani ya CHADEMA kinaweza kuwa lugha inayotumiwa katika mawasiliano hayo. Kwa mfano, katika waraka huohuo, Msacky ananukuliwa akiandika:
“Wanataka kukumaliza, nami sitakubali mtu ammalize rafiki yangu nikiangalia…wanasema Mbowe hata Mbatia akikaa vema anaweza kumpita kama siasa za kufukuza zitaendelea. Muhimu, usisikilize watu, tulia, urudi tupange tufanye nini? Lakini ukweli ni kwamba sasa wanakuogopa…Mwenyekiti Mtarajiwa…”
Mawasiliano yanaonyesha kuwa Zitto hakufurahishwa sana na taarifa za Mwananchi kuwa amemsaidia Kafulila magari matatu kwenda Kigoma kufanya kampeni chini ya NCCR-Mageuzi, lakini Msacky anaonyesha kumfariji.
“Kaka, mimi nimeiona story, haina matatizo zaidi ya kuwafanya akina Mbowe kusitisha mpango mbaya dhidi yako maana wanaanza kuogopa. Hata Mrema Lyatonga amesema kwamba Zitto huwa unamsaidia akiwa na shida. This shows that ur a leader katika opposition, wewe ni mtu wa maridhiano, unakuza upinzani Kigoma,” anaeleza.
Anasema, “Leo nasikia akina Mnyika wanahaha sana, waambie familia yako wasiingie katika mtego wa kuanza kuhojiwa na akina Kubenea (Saed wa MwanaHALISI), watawachanganya. Wewe usiongee kitu chochote, wabaki wanahaha, lakini for sure you are safe, na hizo kampeni za Mnyika kukuchafua huku akitaja majina ya Kafulila, ataziacha.”
Akionyesha juhudi za kushawishi, kuliwaza au kufarakanisha, Msacky anaandika, “Katika hili Zitto, mimi niko na wewe, huna kosa ambalo umefanya, na wala usihofu maana wewe utakuwa nguzo ya upinzani Tanzania…Wanakupa majina ya ajabu, wanakuita Mr Dowans, wanatumia akina Halima Mdee kukuchafua katika magazeti…”
Awali Zitto alikuwa amemwandikia Msacky akisema, “Stori niliyoiona kwenye mwananchi itaniletea matatizo sana.” Hiyo ilikuwa Jumatatu 30 Novemba 2009, saa 5.21 asubuhi. Baruapepe hiyo ilikuwa na kichwa kisemacho: “Muhimu na haraka.”
Aidha, katika mawasiliano mengine, Zitto anaendelea kuonyesha kutofurahishwa na taarifa juu ya magari matatu kwa safari ya Kafulila.
Naye anaandika kwa Msacky, “tatizo la stori ni wingi wa magari, itaonekana mimi nina magari mengi na ni fisadi unajua? Hilo ndio tatizo.”
Saini ya Zitto inatofautiana katika baadhi ya baruapepe. Pengine anaandika “zitto” na kwingine anaandika “Zi.”
Moja ya mawasiliano ambayo yanazua mashaka yanaonyesha Zitto akikiri kuwa na mawasiliano na waasi nchini Kongo akiandika, “take it from me (niamini), nina contacts nyingi sana Congo na hao rebels (waasi) huwa wananiomba sana ushauri na kutaka kuwaunganisha.”
Katika moja ya mawasiliano, Msacky anamwonya Zitto kutotumia baruapepe ya “CHADEMA kwa mawasiliano ya siri” na kutaka amwambie mama yake Shida Salum akatae kuongea na waandishi wa habari. “…nasikia Mbowe anataka mama awe akiongea na waandishi, usikubali,” alieleza.
Zitto alipoulizwa kuhusu taarifa ya Mwananchi kuwa anatembea na barua mfukoni ya kujiuzulu uanachama CHADEMA, alisema “Sina la kusema.”
Alipong’ang’anizwa kwamba imekuwaje hawezi kuzungumzia suala hilo ambalo ni muhimu kwa mustakabali wake wa kisiasa kwa chama chake, Zitto alisema, “Ni kwa sababu sitaki kuingia katika malumbano na katibu mkuu wangu (Dk. Willibrod Slaa) kwani malumbano hayo hayataijenga CHADEMA.”
Alipotakiwa kueleza juu ya baruapepe ambazo zinadaiwa kuwa mawasiliano kati yake na Msacky, haraka alijibu, “Sina la kusema.”
Alipoelezwa umuhimu wa yeye kueleza msimamo wake juu ya baruapepe hizo, Zitto alijibu, “Chochote nitakachosema sasa hivi, kitawachanganya Watanzania.
“Sitaki malumbano. Hakuna sababu ya kuwachanganya Watanzania. Hiyo haina maana yoyote,” alisema Zitto kwa sauti ya ukali. Zitto alikuwa akiongea kutoka Ujerumani kwa simu Na. +4915222493231.
MwanaHALISI ilimtafuta Msacky. Baada ya kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa, hatimaye aliandika ujumbe “Kaka, niko katika kikao. Tuma ujumbe.”
Msacky aliulizwa, “Kaka, tumesikia kwamba umetajwa katika sakata la Zitto na chama chake na kwamba wewe ndiye mtibuaji. Je, ni kweli?” Hakujibu ujumbe na alipopigiwa simu ilikuwa inaita hadi kukatika.
Gazeti lilipowasiliana na Mnyika na kumueleza kwamba amekuwa akitajwa katika ujumbe wa Zitto na Msacky, alikiri kupokea ujumbe huo wa baruapepe uliotoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni “Mtanzania mwema.”
Alisema alipoona ujumbe mmoja unahusu Zitto kushauri Msacky kutochapisha habari za mkutano wake na waandishi wa habari, ndipo aliamua kupeleka ujumbe huo kwa Zitto.
“Nilimuuliza kuna hiki kitu nimetumiwa. Je, haya ni maandishi yako au kuna mtu ameingilia emaili yako na kujiandikia haya? Hadi leo hii, bado sijapata jibu,” alisema Mnyika kwa sauti ya masikitiko. Alisema yeye hana cha kusema na kuongeza, “labda umuulize Zitto.”
Alipoulizwa anachukuliaje suala hilo, Mnyika alisema, “Ukiniuliza mimi kwa upande wangu, nilitegemea mambo hayo yangemalizwa katika vikao vya chama na si kwa vyombo vya habari. Lakini kwa hatua ya hivi sasa, nadhani Zitto bado anayo fursa ya kulieleza hili.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe alipoulizwa juu ya madai ya kuwapo njama za kuhujumu chama chake zinazofanywa na Msacky kwa kumtumia Zitto, haraka alijibu, “tuna utaratibu wetu wa kushungulikia mambo ndani ya CHADEMA.”
Alisema, “Sina la kusema. CHADEMA ina utaratibu wake wa kushughulikia mambo yake.”
Kwa kadri mawasiliano ya Zitto na Msacky yanavyoonyesha na iwapo yatathibitishwa kuwa kweli, jambo ambalo linaanza kuthibitishwa na Zitto kwa kulalamika kuingiliwa kwenye faragha, basi uhusiano wake katika chama utakuwa umepata nyufa.
Wachunguzi wa siasa za upinzani nchini wanasema kwa hali hii, uwezekano wa Zitto kubaki ndani ya chama chake ni mdogo. “Ama atajiondoa mwenyewe au hatimaye atafukuzwa,” ameeleza mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Hata hivyo, Zitto amenukuliwa na Mwananchi akisema, “Sitaki kugombana na mtu mimi. Wala msiniweke kwenye kifungo cha siasa. Ni bora niishi huru kuliko katika mateso ya siasa za kipumbavu kabisa. Nitafanya maamuzi ambayo hayajawahi kufikiriwa.”
Wiki iliyopita Kafulila aliwaambia waandishi wa habari kwamba Zitto atafanya maamuzi makubwa ambayo hawakutegemea.
 
sielewi kwanini mpaka leo Zitto bado yupo CHADEMA! huyu jamaa ni agent wa TISS lakin wamezidi kumlea sana, Haaminiki hata kidogo na ipo siku atakuja kuiacha CHADEMA pabaya alafu itakuwa too late.
Mzee cool down Chadema is a phenomenon note a personality
 
mbivu na mbichi.madaraka bado hawajapata wanakuja na mikakati kabambe ya mauaji,je wakipewa si watazalisha M24 ndan yao
 
Sote tunatambua JF ni kisima cha taarifa, watu wanafahamu mambo mbalimbali ambayo kwa kweli yamefanya Jamvi hili kuwa ndio kitovu cha habari nchini kwa sasa kwa namna nyingine naweza kusema ndio CCN yetu manake tukio linaripotiwa papo papo naombeni wana JF wenzangu nimfahamu Denis Msaki
Ni na Nani kwenye siasa za Mtanzania
Je gazeti la Mwananchi baada ya TIdo Mhando limeamua kujiingiza kwenye siasa za Tanzania mlengo wa CCM
Je Lwakatare angepanga kumgaidi sijui ndio tafsiri raisi au kumpa sumu kwa sababu zipi
Je sheria ya ugaidi ni hii ya watanzania kwa watanzania kutaka kuweeana sumu
Je Denis Msaki huko nyuma amewahi kuwa mwanachama wa chadema

haya basi nifahamisheni mwana JF mwenzenu

First on the left

DENIS+MSAKI,+BAKARI+MACHUMU,+KULWA+JACKSON+MKUTANON+WA+MCT+NA+WAHARIRI+WA+VYOMBO+VYA+HABARI+MORO+PIUX+NO+1.jpg
 
lwakatare gaidiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

ahasiwe ili ataje mtandao wake. nasikia viongozi wengi wa chdm sasa hivi wanaharisha
 
Msaki ni mtanzania huru na mhariri mtendaji wa gazeti la mwananchi. Kosa lake ni kuwa na urafiki na zitto. Alitakiwa awe na urafiki na mbowe au slaa

Kwa hiyo unataka kusema kwamba Chadema wana-gaidiana au kujigaidisha wenyewe? Kama ndivyo mungu epushia mbali.
 
Mwana JF
Raisi-Mwislamu
Makamu wa Raisi-Mwislamu
Jaji Mkuu-Mwislamu
Mkuu wa Usalama wa Taifa -Mwislamu
Waziri wa Ulinzi-Mwislamu
Mkuu wa Jeshi la Polisi-Mwislamu
Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu-Mwislamu
Kati ya wakuu wa mikoa -28- 19 waislamu
Matajiri Kumi wa Nchi hii-10 waislamu-1 Mkristo
Asilimia 78 ya wajumbe wa kamati kuu ya wajumbe wa CCM- waislamu
Asilimia 81 ya wajumbe wa tume ya katiba waislamu
Asilimia 66 ya wakuu wa wilaya waislamu

Na wakati tunagombania uhuru wazee wa TANU waliompa shavu Nyerere karibu wote walikuwa waislam wavaa baraghashia wa Dar Es Salaam mbona hilo nalo hulalamiki??

Kweli kuna watu wanatumia vichwa vyao kufuga nywele...
 
Mwana
JF
[FONT=Times New
Roman][/FONT]
Tusipokuwa

macho hawa CCM watatugawa kikabila na tutaanza
kupigana,kunyanyapaawatanzania wenzetu na watu kama wakwere
,wazanaki,wandengereko,wamakua nawamwela hawatapata uongozi wa nchi
kamwe kwa sababu makabila ni madogo,CCM sasahivi wametengeneza syndicate
ya kumdharau Nyerere kumshusha hadhi nakumdhalilisha lakini ukweli kitu
alichofanyia nchi yetu kizuri kulikuo yoteilikuwa ni kutuunganisha na
kuondoa ukabila ,Je tumuulize Bulembo Kilimanjaroau Moshi ni Chadema
peke yao au wako CCM na TLP ,NCCR iliwahi kuwa na wabungekule jamani
inadhihirisha sasa kwamba kampeni zao zinafanikiwa Kikwetealipokuwa
anapokea ushindi wa mwaka 2010 alisema uchaguzi ulitawaliwa na
udiniakalalama kwamba ataumaliza sasa sikiliza alivyofanya

Raisi-Mwislamu
Makamu wa Raisi-Mwislamu
Jaji Mkuu-Mwislamu
Mkuu wa Usalama wa Taifa -Mwislamu
Waziri wa Ulinzi-Mwislamu
Mkuu wa Jeshi la Polisi-Mwislamu
Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu-Mwislamu
Kati ya wakuu wa mikoa -28- 19 waislamu
Matajiri Kumi wa Nchi hii-10 waislamu-1 Mkristo
Asilimia 78 ya wajumbe wa kamati kuu ya wajumbe wa CCM- waislamu
Asilimia 81 ya wajumbe wa tume ya katiba waislamu
Asilimia 66 ya wakuu wa wilaya waislamu
KIkwete ameingiza mfumo Islamu nina wasiwasi anaposema au anapotuma watu
wakekusema huwa ameshaamua jambo fulani ameshatutenga kidini sasa
atatutengakikabila si mtu mwema hata kidogo kwa mustakabali wa taifa
hili kiongozi mzuriangemtuma mtu akanushe maneno ya Bulembo lakini yeye
anashabikia kwa sababuanataka kuwanyanyapaa wachaga bila sababu,Nape
alisema hivyo hivyo kamaBulembo,Kinana alisema hivyo hivyo kama
Bulmbo,Mwigulu alisema hivyo hivyo kamaBulembo Mtoto wa Kikwete yeye
ndie aliyeapa kwamba Haitakaa itokee kaskaziniitoe raisi ,Mtanzania
mwenzangu tafakari

[FONT=Times New
Roman][/FONT]

Ulikuwa unatiririka vizuri lakini kwa sasa umeamua kutoa lako la rohoni,
nalo si lingine ni chuki yako kwa waislam na uislam. wakristo wapagani
na waislam tumeishi kwa maelewano, kwa nini kutokuaminiana kunaenda sambamba na umaarufu wa CDM? Je kuna watu kama wewe wanatufitinisha
 
Na wakati tunagombania uhuru wazee wa TANU waliompa shavu Nyerere karibu wote walikuwa waislam wavaa baraghashia wa Dar Es Salaam mbona hilo nalo hulalamiki??

Kweli kuna watu wanatumia vichwa vyao kufuga nywele...

Ni kweli waislam wa Dar walipigania uhuru toka kwa mkoloni lakini pia kwenye maeneo mbalimbali ya nchi wazee wenzao walihusika kuhakikisha wanawapa nguvu wenzao waliokuwa karibu na Gavana historia uzuri wake huwa haifutiki
 
Ulikuwa unatiririka vizuri lakini kwa sasa umeamua kutoa lako la rohoni,
nalo si lingine ni chuki yako kwa waislam na uislam. wakristo wapagani
na waislam tumeishi kwa maelewano

Hapana nilikuwa na mjibu yule aliyehusisha swali langu kutaka kumfahamu Denis Msaki na Chadema kuwa chama cha kidini,ukanda,ukabila ndio nikasema tukienda huko hatutafika mbona Kikwete kwa miaka mitatu amechagua safu yake ya uongozi katika nyanja mbalimbali je pia tuite mfumo Islamu bado lengo langu ni kumfahamu vizuri Denis Msaki ni nani mwanachama wa chadema,au kiongozi wa nchi na kama ni mwandishi habari zak zinahatarisha vipi chama cha demokrasia na maendeleo kaka
 
lwakatare gaidiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

ahasiwe ili ataje mtandao wake. nasikia viongozi wengi wa chdm sasa hivi wanaharisha
Kaka swali langu hujanijibu Denis Msaki ni nani katika siasa za Tanzania tafadhali jibu swlali langu usianze matusi
 
Mku unatufanya Watanzania tuonekane ni watu wa ajabu sana. Je, umewahi kujiuliza ni mara ngapi gazeti hili unalolituhumu hapa limeweza kutishiwa na serikali ya CCM kwa madai kuwa linaipendelea Chadema? Unakumbuka lilipotishiwa mufutwa wakati wa kampeni za 2010? Ni bora kutenganisha urafiki binafsi wa Denis na Zitto kwa upande mmoja na Chadema na Mwananchi kama taasisi kwa upande wa pili. Hapo ndipo nitakapoamini kuwa hili ni jamvi la Great Thinkers. Binafsi si mwanachama wa chama chochote cha siasa ila ni mfuatiliaji na msomaji mzuri sana wa gazeti la Mwananchi

Sote tunatambua JF ni kisima cha taarifa, watu wanafahamu mambo mbalimbali ambayo kwa kweli yamefanya Jamvi hili kuwa ndio kitovu cha habari nchini kwa sasa kwa namna nyingine naweza kusema ndio CCN yetu manake tukio linaripotiwa papo papo naombeni wana JF wenzangu nimfahamu Denis Msaki
Ni na Nani kwenye siasa za Mtanzania
Je gazeti la Mwananchi baada ya TIdo Mhando limeamua kujiingiza kwenye siasa za Tanzania mlengo wa CCM
Je Lwakatare angepanga kumgaidi sijui ndio tafsiri raisi au kumpa sumu kwa sababu zipi
Je sheria ya ugaidi ni hii ya watanzania kwa watanzania kutaka kuweeana sumu
Je Denis Msaki huko nyuma amewahi kuwa mwanachama wa chadema

haya basi nifahamisheni mwana JF mwenzenu
 
Back
Top Bottom