Dedan Kimathi alivyoigusa Tanganyika 1950s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,975
30,321
DEDAN KIMATHI ALINYONGWA SIKU KAMA YA LEO 1957

Nimeona hapa barzani imewekwa taarifa ya kunyongwa Dedan Kimathi siku kama ya leo mwaka wa 1957.

Taarifa hii imenigutua na nimefunua kitabu cha Abdul Sykes kuangalia kile nilichoandika kuhusu Dedan Kimathi.

Naweka hapo chini yale ambayo nimeandika katika kitabu cha Abdul Sykes kuhusu Dedan Kimathi kama alivyohusishwa na harakati za uhuru Tanganyika:

"Minong’ono ilikuwa ikisikika kutoka kanda ya ziwa kuwa kiongozi wa wapiganaji wa Mau Mau, Dedan Kimathi alikuwa anaonekana mjini Mwanza.

Wakati ule pale Mwanza kulikuwa na Wakikuyu wengi wakifanya biashara sokoni.

Ilivumishwa kuwa Dedan Kimathi alikuwa akiwasiliana na Wakikuyu wenzake na wao walikuwa wakimkusanyia fremu za baiskeli za zamani ili zitumike kutengenezea magobole ili zitumiwe misituni dhidi ya majeshi ya Waingereza.

Mapigano yalipoonza kati ya Mau Mau na Waingereza kulikuwa na Wakikuyu kama 16,000 wakiishi na kufanya kazi kaskazini ya Tanganyika.

Kama tahadhari, Wakikuyu wachache walioonekana kuunga mkono Mau Mau, walikamatwa na kupelekwa Kenya ambako waliwekwa kizuizini katika kambi mbali mbali.

Wakati Budohi na Wakenya wengine walipopita Korogwe wakati wakirudishwa Kenya kupitia Taveta, Ally Sykes, ambaye alikuwa amehamishiwa Korogwe, alikwenda hadi stesheni ya reli kuwaaga.

Watuhumiwa hawa wa Mau Mau walikuwa wametiwa katika mabehewa ya kubebea ng'ombe huku wamefungwa minyororo.
Dome Budohi na wazalendo wengine waliwekwa kizuizini kwa miaka saba.

Dome Budohi wakati anakamatwa 1955 alikuwa mwanachama wa TANU na kadi yake ya TANU ni no. 6 na alipata kuwa pia Secretary General wa TAA 1953 Julius Nyerere akiwa President wake.

Budohi alisalitiwa kwa Special Branch na Mkenya mwenzake aliyejulikana kwa jina moja Martin na alifungwa Lamu hadi mwaka wa 1962.
Kilichomkamatisha ni barua kutoka Kenya iliyogusia harakati za siasa.

Inasadikika kuwa wapo wanawake ambao walishiriki katika harakati za ukombozi wa Kenya katika Mau Mau lakini walioshika madaraka hawataki kuwapa hadhi wanazostahili kama mashujaa wa uhuru.

Halikadhalika shujaa kama Dedan Kimathi hajapewa heshima anayostahili kama mzalendo aliyepigania uhuru wa Kenya na akanyongwa na wakoloni wa ajili hiyo.

Hadi leo kaburi lake bado lipo ndani ya jela aliyonyongewa.
Picha: Nakala ya gazeti kutoka Maktaba ya Mzee Kissinger.

1645248411491.png
 
Dedan Kimathi, the warrior!! huyu jaamaaa namkubali sana!...mwagika zaidi babu una mpaka magazetiiii!!! km unakijua hata kitukuu tu cha huyu jamaa nitonye!! halafu wakikuyu na wakurya damu moja wale!
 
Halikadhalika shujaa kama Dedan Kimathi hajapewa heshima anayostahili kama mzalendo aliyepigania uhuru wa Kenya na akanyongwa na wakoloni wa ajili hiyo.
Sina hakika ni heshima ya aina gani ambayo unadhani anastahili, lakini kitendo cha Kenya kukipa chuo kikuu nchini humo tena kinajumuhisha masuala ya kihandisi katika viwango vya kimataifa binafsi nadhani mchango wa Dedan Kimathi unakumbukwa kwa heshima.
 
Back
Top Bottom