DCB Commercial Bank imechakachua faida ya Mwaka 2011?

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,452
3,065
Naomba ufafanuzi kwa wale wenye taarifa sahihi. Kila mwaka benki ya DCB hutoa gawio la 50% ya faida baada ya kodi.

Mwaka jana kulingana na document zilizokuwa published kwenye magazeti kama taarifa za benki (balance sheet, income statement and cash flow) zilionesha hadi 31dec2011 benki ilikuwa na faida baada ya kodi ambayo gawio kwa hisa lilikuwa 110TZS

Mwaka 2010 gawiwo kwa hisa baada ya kodi lilikuwa 99TZS, kutokana na policy ya 50% kutolewa kwa wanahisa, kila mwanahisa alipata 48TZS kwa hisa moja. Hivyo hivyo miaka 2008 ambapo gawio lilikuwa 20TZS kwa hisa, 2009 lilikuwa 28TZS kwa hisa moja.

Je mwaka huu kuna nini, maana kutokana na mahesabu hayo, ya mwaka 2011 ambayo yalitoka baada ya siku 60 baada ya dec 31, 2011. 50% ya 110TZS ilikuwa 55TZS gawio kwa hisa moja. Sasa wameka kimya muda mrefu na hivi karibu wameibuka na pendekezo la gawio la 50TZ kwa hisa moja, hiyo 5TZS kwa kila hisa imeenda wapi?

Katika shehere ya kufunga mwaka CEO alionesha kuwa kunauwezekano wa kupata gawio la 57TZS kwa hisa moja kutoka na hali ya faida baada ya kodi; taarifa hizo zilikuwa kwenye website yao ya zamani ambayo imetolewa hewani ndo wakaja na mambo mapya; pamoja na kuweka mazingira kuwa website mpya inatokana na kubadilika kwa jina na leseni kuwa commericial bank, je ni sawa kuja na taarifa zinazotofautiana na zilizokuwepo?? kama faida kupungua, gawio kupungua etc. wakati hizi ni official documents za bank??


Naomba ufafanunuzi suala hili likoje
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom