DC wa Rungwe, Jaffar Haniu azindua ujenzi wa Barabara ya Ndulilo - Itete yenye urefu wa Kilometa 11.38

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua ujenzi wa barabara ya Ndulilo mpaka Itete kwa Kiwango cha Lami inayounganisha Kata ya LUFINGO na KYIMO yenye umbali wa KM 11.38 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 8.9, leo tarehe 24.8.2023.

Akimtambulisha Mkandarasi anayetekeleza Ujenzi wa barabara hiyo; Haniu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa kiasi hicho cha fedha na kuwa inaenda kufungua fursa za kiuchumi sambamba na usafirishaji wa watu na mazao mbalimbali ya kilimo.

Haniu.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu (katikati) akifafanua jambo.

Amesema Serikali imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikilenga kuwaondolea changamoto mbalimbali Wananchi ikiwemo usafirishaji, elimu, afya, maji na umeme.

"Leo tunashuhudia uzinduzi wa barabara hizi lakini vituo vya afya, madarasa pamoja na maji yanasambazwa kwa kasi huko vijijini na hizi ni juhudi za serikali yenu tukufu inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan," ameongeza.

Aidha, amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi anayetekeleza mradi huo na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kurudisha nyuma maendeleo ya mradi ikiwemo vitendo vya uwizi wa vifaa vya ujenzi.

Katika hatua nyingine DC Haniu ametoa rai kwa Wananchi kutojitokeza na kuomba fidia dhidi ya mradi na kuwa vikao vilishafanyika huko nyuma na wananchi kuridhia kuondoa mazao yao bila kufidiwa chochote.

Naye, Mwenyekiti wa Chama chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Rungwe, Mekson Mwakipunga ameishukuru Serikali kwa kutekeleza Ilani ya Chama Tawala na kumuomba Mkandarasi kutoa ajira kwa wazawa hatua itakayoongoza kipato na hivyo kuboresha maisha ya wananchi.
Wakati huohuo, Wakazi wa kata hiyo wameishukuru Serikali kwa kuwajengea barabara hiyo.

Joseph Mwakasungura Mkazi wa Kijiji cha Kali ameipongeza Serikali kwa hatua hiyo na kuwa itarahisisha usafirishaji wa mazao ya ndizi , Kahawa, maziwa, pamoja na parachihi kutoka Shambani Kuelekea sokoni.

Naye, Ana Aswile Mkazi wa kijiji cha Lufingo ameshukuru ujenzi huo na kuwa itawarahishia Kufika kwa urahisi katika vituo vya kutolea huduma ya afya hasa kwa Mama Wajawazito.

Barabara hiii inayojengwa na Kampuni ya Sigh&Sons Company kutoka Mkoa wa Kilimanjaro, chini ya Usimamizi wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA), inafadhiriwa na Mradi wa Agri-Connect na inatarajia kukamilika baada ya Mwaka mmoja kuanzia tarehe 01.9.2023
 
Naipongeza serikali ya CCM kwa ujenzi wa hizi bara bara.

Marekani wakati wanajenga bara bara ya kutoka Alaska kuja Marekani (kupitia Canada) yenye urefu wa km 2,000 walilemewa na gharama za ujenzi. Hivyo wakaamua kujenga kwanza one way.

Kama na sisi tumelemewa, badala ya kujenga km 100 za two way, ni bora tujenge km 200 za one way magari yapite kwa kupokezana.

Juma tatu yakipita magari ya kwenda, Juma nne yapite magari ya kurudi. Yani wajenge pembezoni na bara bara ya vumbi ili wale wa 'kwenda na kurudi' waendelee kutumia bara bara iliyopo.
 
Back
Top Bottom