DC Rungwe atoa onyo kwa wanaotaka kutorosha vyandarua vya bure kwenda nchi za jirani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu, leo tarehe 31.10.2023 amezindua zoezi la ugawaji wa vyandarua bure kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi lengo likiwa ni kutokomeza kabisa Ugonjwa wa Malaria kwa kuzuia visumbufu (Mbu) na maambukizo kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Zoezi hili limezinduliwa katika Shule ya Msingi Tukuyu na kuratibiwa na Bohari ya Dawa (MSD), uzinduzi ukienda sambamba na Kauli mbiu "Malaria Sasa Basi".
a53cd523-4644-4821-81e0-c17a8ec62611.jpeg

2b865f94-85d5-404f-85cc-708686588954.jpeg

Haniu ameshukuru kwa jitihada zinazofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Afya kuhakikisha afya za wananchi zinalindwa na hivyo kupanua nguvu kazi ya taifa.

Amesema vyandarua hivi vinatolewa bure kwa wanafunzi, hivyo asingependa kuona wazazi wanavitumia kinyume na malengo mahususi ikiwemo kuvulia samaki na wigo wa bustani dhidi ya ndege na wanyama wengine.

Haniu ameonya watu wanaotoa elimu potofu kuwa vyandarua hivi vina madhara na kuwa kufanya, hivyo kunarudisha nyuma juhudi za Serikali kwani vimefanyiwa utafiti na vinafaa kwa matumizi na kinga ya maralia kwa watoto na jamii kwa ujumla.

Aidha, amemwagiza Kamanda wa TAKUKURU pamoja na Police Rungwe (OCD) kuhakikisha wanakamatwa wote watakaojaribu kutorosha Vyandarua kwenda nchi za jirani.

Mfamasia kutoka MSD, Caroline Cornelius ametaja kuwa jumla ya vyandarua 43,149 na shule 150 zitanufaika na mpango huu na zoezi linatarajiwa kuanza kutekelezwa kesho.

Caroline ameomba Walimu wakuu, kamati za shule pamoja viongozi wa vijiji, kutoa ushirikiano wa kutosha ili zoezi hili likamilike kwa wakati na ufanisi mzuri.
 
Back
Top Bottom