kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,319
- 12,622
Iko hivi,
Pale kijiji cha Kibindu, Handeni kulitokea ajali ya mtoto mdogo kugongwa hadi kufa na mwendesha pikipiki . Mtoto alikufa mara tu baada ya kufikishwa Hospitali ya Wilaya ya Handeni. Tukio hili lilitokea tarehe 29 Decemba, 2019 na msiba ulimalizwa kijijini hapo siku ya Jumatano trh 01 January 2020 nyumbani kwa babu yake Mzee "Afande".
Issue yenyewe ni kuwa kijana aliyemgonga alitoroshwa eneo ya tukio na kijijini hapo na pikipiki iliyogonga ilitoweka eneo la tukio kwa dhamira ya kuficha tukio lisionekane machoni mwa vyombo vya usalama na vya kutoa haki. Maana inasemekana kuwa familia ya mtoto aliyegongwa na ya aliyegonga ni ndugu hivyo wanataka kufunika kombe ili mwanaharamu apite (eti marehemu hana haki na eti ndiyo ahadi yake hiyo huyo mtoto).
Mzee Godwin Gondwe, DC tafadhali tupia jicho la huruma, kitaaluma yako ya uandishi wa habari na ukuu wa usalama Wilayani kwenye tukio hili ovu lililoyagharimu maisha ya mchanga huyo aliyegongwa wakati akienda kununua maandazi mtaa wa jirani.
Kila mwanakijiji yuko tayari kufanya lolote ili haki ya mtoto huyo isipotee bure hata kwa kufikisha jambo hili ofisi namba 01.