DC aliyetenguliwa katika uteuzi adai aliogopa kumdhalilisha rais

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,149
DC aliyetenguliwa katika uteuzi adai aliogopa kumdhalilisha raisNa Pdidy wetu


MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera, Anatory Choya, ambaye uteuzi wake wa Mkuu mpya wa Wilaya ya Kishapu ulitetenguliwa, Rais Jakaya Kikwete muda mfupi baada ya kumtangaza, amesema alishidwa kukataa kushika nafasi hiyo kwa kuhofia kumwaibisha Rais.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu akiwa njiani kurejea Biharamulo akitokea Dodoma jana, Choya alisema kama angekataa uteuzi wa rais ni sawa na kumwaibisha mkuu wa nchi.

Alisema yeye kama Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hawezi kamwe kutakaa uteuzi wa rais ambaye pia ni Mwenyekiti wake wa CCM taifa.

"Nilishindwa kuapishwa baada ya kushauriana ili tupishe kesi iliyopo mahakamani," alisema Choya ambaye nafasi yake imechukuliwa na Abdul Suleiman Lutavi.

Alisema ana aamini kesi hiyo itaisha mapema na ndipo atajua hatima yake katika nafasi hiyo ya ukuu wa wilaya.

Choya alisema kuwa aliamini kuwa mamlaka zilizomchagua zilimchagua zikijua kesi hiyo ipo na kwamba huenda zilijua kuwa kesi hiyo ingeisha mapema zaidi.

Choya na mbunge wa zamani wa Biharamulo Magharibi, mkoani Kagera alikuwa akijibu hoja za baadhi ya watu nchini kwamba kwa nini hakutaa uteuzi wakati alijua kuwa ana kesi mahakamani.

Takukuru ilimfungulia kesi baada ya kumtuhumu kutumia rushwa wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Biharamulo mwaka 2007, nafasi ambayo alishinda.

Kesi yake namba 270 ya mwaka 2008 inaendelea katika Mahakama ya Wilaya ya Biharamulo na Aprili 17 mwaka huu ilitajwa na inatarajiwa kutajwa tena Mei 11 mwaka huu.

Wiki iliyopita wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Shinyanga, pamoja na wananchi waliohudhuria hafla ya kuapishwa kwake walipigwa butwaa baada ya kushuhudia akiapishwa Lutavi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Dk Yohana Balele badala ya Choya.

Choya alipewa taarifa ya kutenguliwa uteuzi wake kutoka Ikulu akiwa njiani na familia yake kutoka wilayani Biharamulo kwenda katika kituo chake kipya cha kazi Machi 27 mwaka huu Rais Jakaya Kikwete alifanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya nchini na kuwastaafisha saba, akiwamo Choya, kuwateua wapya 15 na kuwabadilisha vituo vya kazi 54.
 
Back
Top Bottom