Dawa ya mba

Wakuu habari za majukumu, binafsi ninasumbuliwa sana na mba kwa miaka mingi ni mba wa kichwani unashuka hadi usoni. Nimeshatumia dawa za pharmacy zinanisaidia kwa muda mfupi then unarudi tena.

Kwa ambae anajua mafuta/dawa itakayoweza kuutibu naomba anisaidie.

Asanteni.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Umejaribu sonaderm pia!!?

Ile tube ile,HEBU kaulize mkuu!!
 
Za vidonge na ya kupaka nimeisahau jina lake

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Tatizo la dawa za mba inaweza ikatibu kwangu kwako isikutibu.

Nenda pharmacy iliyopo karibu nawe waambie unahitaji mafuta ya mba yapo kwenye kikopo cha kijani hayo mafuta yanatengenezwa South Africa Bei yake haizidi 10,000/- nadhani ni 6,000/- labda yawe yamepanda, sikumbuki jina ni km mafuta ya mgando hivi kikopo chake ni km cha Baby Care Ila chenyewe ni cha kijani ukiwaeleza pharmacy km nilivyokueleza wanayajua

Unapaka pia unamix na mafuta fulani hivi ya Tube hio ndio dawa ndani ya wiki 3/4 mba umeisha

Mafuta ya tube haya hapa kawaonyeshe pharmacy watakupa yanaitwa VIRGIN HAIR FERTILIZER
0525431834633ed794f41475a64a20a5.jpg
 
Chukua kitunguu maji kikubwa 1, tangawizi moja, kiazi ulaya(vile vya chipsi) kimoja kikate nusu.
Tumia vile vidude vya kukwangulia karoti, kwangua kitunguu, tangawizi na kiazi, changanya kwa pamoja then tafuta kitambaa kisafi ikiwezekana nunua zile leso nyeupe za miatano, chuja mchanganyiko wako kwa kitambaa safi upate majimaji yake.paka huu mchanganyiko kwenye ngozi ya kichwa na nywele then funika kichwa chako kwa kofia ya plastiki kwa dk 45.
Baada ya hapo osha nywele zako vizuri kwa kutumia shampoo(shampoo zipo Hadi za 2000 nenda dukani tu utachagua).ukimaliza kuosha Sasa nywele ikikauka chukua mafuta yanaitwa virgin hair fertilizer ( Kama uchumi hauruhusu nunua tu mengine yanaitwa sulphur ya kampuni ya movit ni 1500) paka kwenye ngozi ya kichwa, zingatia upake kwenye ngozi.Fanya hii routine ya kitunguu atleast Mara moja kila wiki tatizo la mba utalisahau kabisa.
 
Tatizo la dawa za mba inaweza ikatibu kwangu kwako isikutibu.

Nenda pharmacy iliyopo karibu nawe waambie unahitaji mafuta ya mba yapo kwenye kikopo cha kijani hayo mafuta yanatengenezwa South Africa Bei yake haizidi 10,000/- nadhani ni 6,000/- labda yawe yamepanda, sikumbuki jina ni km mafuta ya mgando hivi kikopo chake ni km cha Baby Care Ila chenyewe ni cha kijani ukiwaeleza pharmacy km nilivyokueleza wanayajua

Unapaka pia unamix na mafuta fulani hivi ya Tube hio ndio dawa ndani ya wiki 3/4 mba umeisha

Mafuta ya tube haya hapa kawaonyeshe pharmacy watakupa yanaitwa VIRGIN HAIR FERTILIZER View attachment 2739623
Shukran mkuu

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Chukua kitunguu maji kikubwa 1, tangawizi moja, kiazi ulaya(vile vya chipsi) kimoja kikate nusu.
Tumia vile vidude vya kukwangulia karoti, kwangua kitunguu, tangawizi na kiazi, changanya kwa pamoja then tafuta kitambaa kisafi ikiwezekana nunua zile leso nyeupe za miatano, chuja mchanganyiko wako kwa kitambaa safi upate majimaji yake.paka huu mchanganyiko kwenye ngozi ya kichwa na nywele then funika kichwa chako kwa kofia ya plastiki kwa dk 45.
Baada ya hapo osha nywele zako vizuri kwa kutumia shampoo(shampoo zipo Hadi za 2000 nenda dukani tu utachagua).ukimaliza kuosha Sasa nywele ikikauka chukua mafuta yanaitwa virgin hair fertilizer ( Kama uchumi hauruhusu nunua tu mengine yanaitwa sulphur ya kampuni ya movit ni 1500) paka kwenye ngozi ya kichwa, zingatia upake kwenye ngozi.Fanya hii routine ya kitunguu atleast Mara moja kila wiki tatizo la mba utalisahau kabisa.
Shukran mkuu

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Nunua mafuta ya kondoo yachemshe na dawa moja ya kimasai inaitwa loduwaa,baada ya hapo kunywa kikombe kimoja cha mafuta,hio inatibu kila kitu, utakuja kunishukuru,na ukinywa ukaona labda matokeo ni negative basi ujue mwili wako una maradhi mengi yaan zaid ya hilo
 
Tumia Sofn free super dawa ile ya nywele ya wanawake za curls na tumia kila wiki mara moja, zitaisha kabisa kichwani, dawa ya nywele iko kwenye kopo la kijani.
 
Back
Top Bottom