Dawa ya kudumu ya Halmashauri zetu ni kuzifuta

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
15,861
20,714
Dawa ya kudumu ya Halimashauri zetu ni kuzifuta.Mwaka 1972 serikali ilizifuta,tatizo moja wapo kubwa likiwa ubadhirifu wa fedha na kutowajibika ipasavyo kwa wananchi.Matatizo hayo yapo hata sasa!We can do it again.

Serikali za Mitaa ni vyombo vya wananchi ambavyo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huundwa, huendeshwa na huwajibika kwa wananchi.

Hata hivyo kumekuwapo na malalamiko mengi ambayo yamethibitishwa na taarifa za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuhusu matumizi mabaya ya fedha na mali za halmashauri.
Dhumuni la kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi. Hii ni kwa kuwa wananchi ndio chimbuko la mamlaka yote katika nchi yetu na ili wananchi waweze kuchangia kikamilifu katika maendeleo yao.

Katiba inaelekeza pia kwamba vyombo vya Serikali za mitaa vitakuwa na haki na mamlaka ya kushiriki na kuwashirikisha wananchi katika kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo na utoaji wa huduma maeneo yao nchini kote kwa ujumla.

Serikali za mitaa nchini zilikuwepo hata kabla ya wakoloni hawajatawala nchi hii.

Utawala wa Mjerumani haukutambua serikali za wenyeji na badala yake ukaweka mawakala wake.
Utawala huu wa Mjerumani ulikuwa wa kikatili mno,ndiyo maana wananchi walianzisha vita kupambana nao.

Kwa upande mwingine, utawala wa Mwingereza ulitambua utawala wa wenyeji na ukauhalalisha kwa sheria Na.72 ya mwaka 1926. Vilevile, utawala wa Mwingereza ulitunga sheria Na.333 ya mwaka 1953 katika jitihada zake za kuendeleza mfumo wa serikali za mitaa nchini. Dosari kubwa inayojitokeza katika serikali za mitaa zilizoundwa ni kwamba, wajumbe walioingia katika mabaraza hayo moja kwa moja hawakuwawakilisha wananchi,hivyo, demokrasia ya kweli haikuwepo.

Jambo hili lilirekebishwa na serikali ya wananchi mara baada ya uhuru, ikiwa ni pamoja kufutwa kwa utawala wa machifu mwaka 1963.

Kutokana na matatizo yaliyozikumba serikali za mitaa ya kukosa fedha, watumishi na utadilifu, zilifutwa mwaka 1972 na badala yake ulianzishwa mfumo wa madaraka mikoani.

Hata hivyo, utaratibu huu wa madaraka mikoani ulidumu kwa karibu miaka kumi tu, na mwaka 1982 serikali za mitaa, zikarejeshwa tena, baada ya kudhihirika umuhimu wa Serikali hizo, kisha uliingizwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na sheria Na. 7 na 8 za mwaka 1982 za Bunge na hivyo kuhalalisha uwepo kwake.

Kuanzia miaka ya 1990 na kuendelea, harakati mbalimbali zilifanyika ili kuboresha serikali za mitaa nchini. Uboreshaji ulianza rasmi mwaka 2000 na awamu ya tatu ya uboreshaji huu ilianza mwaka 2011 na kuendelea.

Pamoja na jitihada zilizofanywa hadi sasa, bado kuna malalamiko mengi ya ukosefu wa utawala bora katika Halmashauri zetu,matumizi mabaya ya fedha,na kutowashirikisha wananchi ipasavyo katika maamuzi yanayohusu maendeleo yao. Maelezo yafuatayo yanafafanua angalau kwa kifupi, hali halisi ya utawala bora ilivyo hivi sasa katika Halmashauri zetu.

Ubadhirifu

Kumekuwapo na malalamiko mengi ambayo yamethibitishwa na taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuhusu matumizi mabaya ya fedha, watumishi na mali za halmashauri.

Mara nyingi ubadhirifu huu umetokana na uamuzi mbaya ya halmashauri zenyewe na mara nyingine kutokana na kutojali kwa watumishi wa halmashauri. Matokeo ya ubadhirifu huu yamekuwa yakidhoofisha halmashauri husika; kudorora kwa huduma muhimu kwa wananchi na kupoteza imani ya wananchi kwa Serikali yao na hivyo kususia wajibu wao wa kulipa kodi na kushiriki katika shughuli za maendeleo ya kijamii.



Rushwa

Siyo jambo la siri kuwa rushwa imetanda na kushamiri katika halmashairi zetu, hasa katika masuala yanaohusu utoaji wa huduma muhimu kama tiba, elimu, leseni za biashara, ugawaji wa viwanja, utoaji wa zabuni na ajira za watumishi.

Vitendo vya rushwa vinafanyika wazi bila aibu, na vinachukuliwa kama vitendo vya kawaida vinavyoendana na wakati. Matokeo yake ni wananchi kunyimwa haki zao za kimsingi, na kutokwa na imani na hata huichukia kabisa serikali yao.

Unyanyasaji wa wananchi

Baadhi ya viongozi katika halmashauri zetu wamepoteza dira ya uongozi. Badala yake wamekuwa wakitumia nafasi zao kuwakandamiza na kuwanyanyasa wananchi ili tu kuonyesha nguvu na uwezo wao bila kujali matokeo ya vitendo vyao kwa Serikali na kwa watu wasio na hatia.

Vitendo hivi vinajitokeza waziwazi katika baadhi ya mbinu zinazotumika katika ukusanyaji wa kodi na aina nyingine za mapato, na pia katika utekelezaji wa Sheria Ndogo za Halmashauri.

Huduma duni

Kero nyingine ni ile inayohusu huduma duni zinazotolewa kwa wananchi kutokana na uzembe na kutojali kwa viongozi na watendaji. Licha ya kutambua hali ngumu ya kiuchumi na upungufu wa mapato, wananchi wanategemea viongozi wao kuhakikisha kuwa rasilimali iliyopo inatumika kikamilifu katika utoaji wa huduma za msingi kama tiba, elimu na huduma za maji na pia katika kuweka miundombinu itakayowawezesha kuimarisha shughuli zao za kiuchumi na maendeleo.
 
Sema mnatarajia kuzifuta ili msetrolaizi kila kitu kwani kipi kimebaki? Maana mmepokonya vyanzo vyote muhimu vya mapato,halmashauri zimekua pararalized,kama mnaona zimekuwa ni kero zifuteni tuu, kitachotokea mje mtupe mrejesho.
 
Sema mnatarajia kuzifuta ili msetrolaizi kila kitu kwani kipi kimebaki? Maana mmepokonya vyanzo vyote muhimu vya mapato,halmashauri zimekua pararalized,kama mnaona zimekuwa ni kero zifuteni tuu, kitachotokea mje mtupe mrejesho.
Eeh lazima tuzifute nyinyi si wezi?
 
Sema mnatarajia kuzifuta ili msetrolaizi kila kitu kwani kipi kimebaki? Maana mmepokonya vyanzo vyote muhimu vya mapato,halmashauri zimekua pararalized,kama mnaona zimekuwa ni kero zifuteni tuu, kitachotokea mje mtupe mrejesho.
Kwani sabubu ya kuzifuta hazipo.Nadhani tujadili hilo.
 
Katika serikali, watumishi wanaoongoza kulipwa mishahara midogo ni wa hizi Halmashauri, hiyo ndiyo inayopelekea yote hayo (rushwa na kutojali utu), wamekuwa ni wababe kwa kupora viwanja vya watu bila kutoa fidia au kwa kutoa fidia ndogo sana huku wakijinasibu kuwa wao ndio serikali..

Waliopata nafasi za uongozi ndio wamekuwa wezi wa waziwazi. Wazo la kuwa na serikali za mitaa lilikuwa bora sana sema usimamizi ndio umekuwa mbovu mpaka kuharibu uwepo wa hizo halmashari, zifanyiwe marekebisho/maboresho ila ziendelee kuwepo maana kwa kiasi kikubwa zimerahisisha upatikanaji wa huduma kwa ukaribu.
 
Hivi mawazo ya kijima siku hizi yameibukaje kwenye Tanzania mpya?
Mkuu unaweza kudhani ni mawazo ya kijima lakini sio.Kama watu hawawezi kujidhibiti,what do you do.Kiukweli halimashauri zetu zina matatizo makubwa,kwa hiyo kuna haja ya either kuzifanyia marekibisho makubwa ili kuwe na checks and balances za kuweza kudhibiti matatizo yaliyoko sasa, au kuzifuta kabisa.Na kama katika miaka yetu yote ya uhuru tumeshindwa ku-introduce appropriate checks and balances,sidhani kama tunaweza kufanya hivyo sasa.Ndio maana nikasema dawa ya kudumu ni kuzifuta kama tulivyofanya 1972.
 
Back
Top Bottom