David Kafulila: Ukitaka kuondoa rushwa na Mikataba mibovu, cha kwanza ni uwazi. PPP ina malengo Makubwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
Kamishna wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (Public-private partnerships - PPP), David Kafulila amezungumzia mambo kadhaa kuhusu uwekezaji na ubia:

Ufafanuzi wa ubia
Akifafanua kuhusu ubia ameeleza unatangenezwa katika mkataba wa uendeshaji wa jambo fulani, ambapo inaongozwa na Sheria inayosimamia.

Amesema “Kwa Tanzania tuna Sera ya PPP mwaka 2009 na Sheria Mwaka 2010 na Kanuni zikatangenezwa Kanuni Mwaka 2011, zikarekebishwa Mwaka 2014 na Mwaka 2018, kwa sasa kuna marekebisho mengine ili kufanya kuwa na Sheria inayoweza kuwa na faida kwa wengi.”

Ameeleza kuwa mabadiliko hayo yanatokana na mabadiliko ya Dunia, hali inayochangia mabadiliko ya Sheria pia.

Mabadiliko ya Sheria za mikataba ya uwekezaji
Amesema moja ya mabadiliko ya Sheria ni kufuta kifungu cha kuwa mwekezaji akiwekeza Tanzania, ikitokea mgogoro maamuzi yafanywe kwa Sheria za Tanzania na katika Mahakama za Tanzania.

Kinawekwa kifungu kuwa ikitokea mgogoro kati ya Serikali na mwekezaji mkataba uweze kusema kuwa utaratibu wa kushughulikia migogoro inaweza kuwa katika Baraza la Usuluhishi Duniani au watakayokuwa wameamua katika mkataba husika.

Maamuzi hayo yatampa mwekezaji nafasi ya kuamua kuwa anaweza kuamua kusuluhisha mgogoro wake ndani ya Sheria za ndani ya Nchi au za Kimataifa.

"Ubia ni Pande mbili, kuna maslahi ya mwekezaji na kuna maaslahi ya nchi, kwa hiyo tunadhani mabadiliko haya ya sheria ambayo tunayaleta, ni mabadiliko ambayo kwa kiasi kikubwa yatalinda maslahi ya pande zote mbili.”

Si mara ya kwanza kuwa katika nafasi ya utendaji
Alipouliwa kuhusu nafais yake kuwa ya utendaji wakati yeye ni Mwanasiasa, amesema "Rais Samia aliniteua kwenye nafasi ya Siasa, lakini pia ameniteua kwenye nafasi ya utendaji, nafasi ambayo nimepata kuteuliwa na Rais wa Awamu ya Tano.

“Sio mara yangu ya kwanza kufanya nafasi ya utendaji, ni jambo ambalo linawezekana kikubwa Watanzania wanataka matokeo, wanataka kuona mambo yanasukumwa, mambo yanatokea.”

Siasa na Utendaji
Kutenganisha Siasa na Utendaji ni rahisi, Watanzania wanataka kuona matokeo, ndio maana ndani ya muda mfupi kuna mambo kadhaa tumeyafanya ikiwemo ya miradi kadhaa ya uwekezaji wa ubia.

Uwazi wa mikataba
Uwazi unaweza kusaidia kuondoa mazingira ya rushwa katika mikataba, hapa sizungumzii siku ya kusaini mkataba bali ni mchakato kablaya siku ya kusaini mkataba, kwa mfumo inayotumika kuandaa miradi ya PPP hakuna nafasi ya kutengeneza mikataba yenye mianya ya rushwa.
 
Ila bila upendeleo Kafulila ni mtendaji mzuri, kiongozi mwenye maono. Ninakumbuka kuna jamaa mmoja (mpigaji) alimwita "tumbili" Ni katika harakati zake za kutetea masilahi ya wanachi bungeni.
 
Nimemuelewa sana. Kafulila ana madini sana. Huyu ni Mtendaji japo watu wanataka kumeletea mambo ya siasa. Uzuri anawapuuza.

Na sasa kakomaa.
 
Back
Top Bottom