Darasa adaiwa kuiba beat ya wimbo wake mpya (hasara roho)

Kama hauamini zisikilize nyimbo zote mbili halo chini. Ni ukweli usiopingika kuwa Darasa ameiba biti iliyotumiwa na msanii underground sana katika muziki Wa bongo fleva. Kama wasanii wakubwa wanakopi kwa wasanii wadogo kama hawa ambao hata hawajavuma kimuziki, tutafika kweli?
Beat ya darasa
https://www.jamiiforums.com/attachments/darassa-hasara-roho-mp3.505376/

Beat anayodaiwa kuiba
https://www.jamiiforums.com/attachments/dogo-iringa_bit-roho-darasa-mp3.505377/
Nakubaliana na wewe kuwa darasa amepotea kwa maana mbali na kuiba beat zake na kuimba nyimbo zakufanana lakin awamu hii amedhihirisha ubovu wake kwakuimba methali za mtaan ambazo kila moja inamaana tofaut na nyenzie yaan katika mistar miwili unapata maana zakutofautiana kila mstar na maana yake.
Mfano elimu bure maana yake ni kutandika kitanda nakukaa nakuongea kikawaida .
 
Darasa kaanza kazi ya u-producer lini mpaka Leo awe kaiba Beat ya watu?!
 
Nakubaliana na wewe kuwa darasa amepotea kwa maana mbali na kuiba beat zake na kuimba nyimbo zakufanana lakin awamu hii amedhihirisha ubovu wake kwakuimba methali za mtaan ambazo kila moja inamaana tofaut na nyenzie yaan katika mistar miwili unapata maana zakutofautiana kila mstar na maana yake.
Mfano elimu bure maana yake ni kutandika kitanda nakukaa nakuongea kikawaida .
kaiba beat kwani Darasa ni producer?!

kama unaona kuimba na kutunga rahisi ebu achia ngoma yako tuisikie.
 
Sasa nani anatafuta kiki kati ya dogo na Darasa? Maana dogo ndo aliyeanza kutoa muziki kitambo
Sasa Darasa anaanzaje kutafuta Kiki kwa msanii anaejulika Iringa tu tena kwa baadhi ya watu wenye husuda kama wewe.

Inaonekana wazi wewe bibie ndio unatafuta Kiki kwa Darasa
 
Tatizo mkiachwa lazima mkimbilie kwenye mitandao ya kijamii kuunda mazengwe sijui mnapata nini ni bora usonge mbele utampata zaidi ya Darasa.
 
kaiba beat kwani Darasa ni producer?!

kama unaona kuimba na kutunga rahisi ebu achia ngoma yako tuisikie.
Ndugu tusijenge mabishano yasio na misingi sikiliza mashairi ya nyimbo hii mpya then njoo tuambie ameifikishia nn jamiii au anasema nn?
 
Ukweli lazima usemwe...Darassa kakopi beat la Neyba basi,hakuna ubunifu wala maajabu yeyote katika hiyo nyimbo,Neyba yuko chini ya Abbah na Abbah huyohuyo ndie Producer wa Darassa.

Ladha ile ile,amepuyanga safari hii darassa,nimeisikiliza nyimbo tangu jana labda nitaielewa lakini wapi
 
Naona mkuu umemkomalia darasa kwa kuanzisha nyuzi za kumponda kulikoni tena amekufanya nin huyo kijana darasani maana siyo kwa juhudi hizi unazofanya
 
Mwanamume kuwa na umbea kama mwanamke nao ni...... Nitarudi
 
Wewe unajua biti ni mali ya nani kati ya prodyuza na msaniii?
Alafu nyimbo ngapi biti zinaendana? Diamond platnumz ameimba nyimbo ina vionjo vya Saida Karori kwenye biti mbona hapakua na tatizo sasa kama Darasa katumia biti ina vionjo vinavyofanana na wimbo mwingine tatizo nini?

Yaani kijana unawezaje kumuandama kijana mwenzako mtafutaji kama wewe?
Promoter anabeep : professor J = Napokea sim: Mangwair.

Nitoke vip: bwana misosi = Mipango: Man x.

Anayeibiwa beat ni producer tu. Msanii anaibiwa vipi.
 
Ndugu tusijenge mabishano yasio na misingi sikiliza mashairi ya nyimbo hii mpya then njoo tuambie ameifikishia nn jamiii au anasema nn?
We unafikiri kila wimbo unahitaji kupeleka ujumbe kwa jamii kwani imekuwa Kwaya ile?!
 
Wabongo bwana badala kujadili hoja mnamzungumzia mtoa hoja jinsia yake.... Nimesikiliza nyimbo zote mbili ni kweli zina beat moja.
 
Darasa si/sio Mwanamuziki wa kiwango cha SIFA mnazo mpa.

Nyimbo yake iliyompa jina na sifa kubwa ya Muziki na Maisha amekopi kwa asilimia kubwa kutoka kwa MWANAMUZIKI wa Msumbiji ambaye aliimba katika lugha ya KIRENO...

ALIKOPI ZAIDI SOUND FLOWS.

Kwa hii nyimbo mpya sina shaka wala mshangao yaweza kuwa ni muendelezo...

Ndio maana hata Flows zinafana na nyimbo yake ya awali MUZIKI NA MAISHA...

Kaishiwa UBUNIFU..
 
Wabongo bwana badala kujadili hoja mnamzungumzia mtoa hoja jinsia yake.... Nimesikiliza nyimbo zote mbili ni kweli zina beat moja.
Ndio nyimbo ya kwanza kufanana beat?

Tatizo sio beat tatizo mleta mada kaileta mada kwa kumshambulia Darasa kama vile wana bifu, mleta mada huyo huyo jana peke yake kaanzisha mada zaidi ya mbili kumponda Darasa sasa unadhani tutakomenti nini sisi maana tushaona anajitahidi kumchafua pasipo ulazima.
Mtu anapoleta mada asiandike kishabiki ili watu wajue ni mada ya kawaida sio bifu baina yao
 
Ndio tatizo tunalo wabongo, uchawi sio kwenye muziki tu, unaweza ona watu wanaleta uchawi hadi kwenye siasa, jambo jema likifanywa na serikali kuna wachawi watatokelezea tu.
Na likifanywa baya nyinyi msio wachawi mnafanyaje?
 
Back
Top Bottom