Daraja la Kigamboni - Mkurugenzi wa NSSF amwaga neema!

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
31,635
37,849
Mkurungezi wa NSSF Anasema:-

"Nawasihi waajiri kulipa michango ya wafanyakazi kwa wakati ili wanufaike na shirika letu pia tunajitahidi kukamilisha miradi ya ujenzi wa daraja la Kigamboni na kujenga upya makazi kuanzia Mchikichini, lengo likiwa ni kubomoa nyumba mbovu na kujenga mji wa kisasa unaojitegemea - Satellite City".

----------------------------


Wananchi wa Kgamboni neema inakuja hiyo, nasikia mna wiki na zaidi pantoni lenu kubwa limekufa, poleni kwa maumivu tupo pamoja. hapa nimewaletea kipande tu cha neema kutoka NSSF kama haya anayosema mkurungezi ni kweli basi NEEMA imefunuliwa kwa watu wa kigamboni, kilio chenu cha karne kimesikika.
 
Na ile public notice juu ya kuzuia ujenzi KIBADA kigamboni kupisha mradi mpya wa Kigamboni NEW CITY ile notice imesha expire tangu 31st Dec 2010- mradi upo tia maji tia maji - kweli kila kitu Tanzania ni siasa tu.
 
story zile zile toka kwa watu wale wale hakuna jipya....kigamboni daraja nimesikia now is more than 5 years. wwwhhhhhhhhi mpaka nilione otherwise ni uzugaji kama kawa
 
Wametuchosha na ahadi zao. Toka mwaka 2000 wanasema Daraja litajengwa, mwaka wa 11 sasa No utekelezaji. Wamefulia kwelikweli hao.
 
story zile zile toka kwa watu wale wale hakuna jipya....kigamboni daraja nimesikia now is more than 5 years. wwwhhhhhhhhi mpaka nilione otherwise ni uzugaji kama kawa

Maji ya uhakika hata kwenye hili tunaloliita jiji letu kuu - Yametushinda
Umeme wa Uhakika - Aibu tupu
Miundombinu hasa barabara kwenye jiji letu ni AIBU - mtu unatoka Mwenge kwenda posta unachukua masaa mawili foleni
Ujenzi Holela - utafikiri hatuna wizara na idara za upimaji - mambo hovyo hovyo tu

Haya nayo yanataka wazungu waje watusaidie? huo uhuru wenu mliulilia wa nini sasa?

Mengine namezea yatanipandishia hasira zangu bure.
 
We yaelekea huwajui wabongo! Longolongo nyingi visingizio kibao.


Umesahau kale ka usemi wa maisha bora kw kila mtanzania? Siku hizi unakasikia tena?


Ukisikia mtu anatoa ahadi hapa bongo sio kwamba amedhamiria bali huenda kabanwa anatafuta pa kuchomokea au analake jambo kichwani.

Shauri yako, hii ndo bongo bwana!. Ukisubiri kunawa hukuti chakula wenzako wanakula hivo hivo.
 
hizo ni propaganda ili wananchi watulie c mnajua tena watanzania tunaongozwa kwa matukio?bora angekuwepo presdaa wa awamu ya 3 na cyo huyu mkwere ambaye anapenda starehe bila kuangalia walet inasomaje mfukoni
 
Toka hilo daraja limeanza kuhubiriwa, kama wangekuwa serious tungekuwa tushasahau.... nina wasiwasi kama kweli litajengwa :twitch: !!!
 
hiyo pesa ya daraja kwa nini isiwekezwa kwenye umeme?

Mkuu hizo pesa zinazojenga daraja la Kigamboni si za serikali ni za NSSF. Pamoja na hivyo, NSSF wamesema kuanzia Disemba mwaka huu wataanza kuzalisha MW 300 za umeme na kuziingiza kwenye grid ya taifa kupunga makali ya ukosefu wa umeme nchini.

Toka hilo daraja limeanza kuhubiriwa, kama wangekuwa serious tungekuwa tushasahau.... nina wasiwasi kama kweli litajengwa :twitch: !!!

Ni kweli mkuu mpaka inakatisha tamaa, lakini mwaka huu kila dalili inaonekana ya kuwa daraja litaanza kujengwa. Magufuli alishawaambia NSSF kama hawako tayari waseme yeye aombe pesa BoT daraja lijengwe. Ila kwa kauli ya Dau (Mkurungezi mkuu wa NSSF) aliyoitoa hivi karibu huko Arusha ni kwamba ujenzi utaanza wakati wowote.
 
...... Ukisubiri kunawa hukuti chakula wenzako wanakula hivo hivo.[/SIZE]
Kweli tumekwisha kama mtu unatokoka choo mkono kwenye chakula la sivyo chakula inaisha basi nchi imekwisha maana watu wanatafuna kama mchwa , hakibakizwi kitu wakigundua kuna mtu amewaona wanakimbilia kupiga vijembe huku nyuma ya pazia wakicheza na sheria ili iwalinde (ihalalishe),
Mfano mtu anaibuka na kusema ........., "watu wanasema Dowans ni batili kwa kuwa ilirithi mkataba wa Richmond ambayo ni kampuni ya mfukoni, wanasahau kuwa wameutumia umeme wa Dowans kwa miezi tisa " hivi miezi tisa hiyo Dowans walikuwa wana supply bure !!!!
 
Back
Top Bottom