Dar yaongoza kwa Wanawake kuharibikiwa mimba

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa mwaka 2022 yanaonesha kuwa 23% ya mimba katika mkoa wa Dar es Salaam ziliharibika na kufanya mkoa huo kuwa na kiwango cha juu zaidi cha kuharibika kwa mimba kuliko mikoa yote nchini.

Ripoti hiyo ya utafiti iliyozinduliwa Oktoba 28 mwaka huu na Rais Samia Suluhu Hassan imehusisha wanawake 15,254 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 kutoka kwenye kaya 15,705 waliofanyiwa mahojiano na kutolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya.

Matokeo yameonesha kuwa taarifa za ujauzito kwa wanawake wenye umri kati ya miaka 15 ha 49 kwa kipindi cha miaka mitatu kabla ya utafiti huo, 90% walijifungua watoto hai na asilimia 10 walipoteza ujauzito.

Aidha, kati ya waliopoteza ujauzito, asilimia nane mimba zao ziliharibika, 2% walijifungua watoto wafu na chini ya 1% walitoa mimba huku mkoa wa Rukwa ukiongoza kwa kiwango cha chini zaidi cha mimba kuharibika.
 
Si jambo la kuchekelea ila tuzidi kuwaombea heri Mama zetu maana hutuzalia Watoto na kutuimairishia afya Me kiakili katika familia zetu.
 
Back
Top Bottom